Kwa ushauri wangu mdogo sana, nadhani shida sio kuandika script ila shida ni kwamba unaandika nini? (Idea/content), cha kukifanya wewe wekeza kwenye tafiti ya muda mfupi angalia kwenye hiyo field yako tafuta tatizo ambalo lipo litengenezee content kwa kulisolve hicho ndo kitakupa kazi.
Hao target yao wanahitaji creative people ambao wanaenda kuongeza kitu kwenye media yao kitakacho wapa competitive edge sokoni dhidi ya wapinzani wao kama clouds etc. Chunguza ni kitu gani media nyingi za bongo hazifanyi na kinaweza kuwa current na kikapendwa na target population yao ambayo wameitarget wao then kitengenezee kama kipindi nenda kakipresent I'm sure kama ukiwa serious na kikiwa na contents za kutosha na ukakiwasilisha vyema unaweza ukapata mwanya, kama sio kupata nafasi ya utangazaji unaweza ukaingizwa hata kitengo cha uandaaji wa maudhui inategemea na utakavyo jiuza siku ukipata nafasi ya kuwasilisha