Naomba kujua ili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kujua ili.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Jaslaws, Jan 12, 2012.

 1. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,151
  Likes Received: 2,195
  Trophy Points: 280
  Wakuu nimesoma ibara ya 71(1) ya katba ya mwka 1977 inaorodhsha vgezo vinavo mnyanganya mbunge sifa ya kua mwakilishi katika bunge la jamhuri ya muungano.sasa swali langu,ni je wabunge wakipiga kula ya vote of no confindence kwa raisi bunge linavunjwa?na swali la pili ni je?mbunge atapoteza sifa ya kua mbunge pale raisi atakapolivunja bunge kama ilivoonyeshwe katka ibara ya 90(2)(a mpka e)? Ama kuna ukidhani ktka hzi provisions?
   
 2. J

  Jamuhuri Huru Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaslaws, mm ktk mada yako nina haya yakuchangia ktk kujibu maswali yako;-

  je wabunge wakipiga kula ya vote of no confindence kwa raisi bunge linavunjwa? - Hapana bunge halitovunjwa, sababu ili bunge livunjwe Katiba imetoa ni wakati gani Rais anaweza kulivunja Bunge kwa mujibu wa sheria ambayo ipo kwenye Ibara ya 90 (2). Hivyo basi mbali na hiyo Rais hawezi kulivunja Bunge kwa mujibu wa sheria, hata kama wabunge wamepiga kura ya kutokua na imani naye. Manake hapo Wabunge watakua wametumia haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara 46A ambayo imetoa mchakato mzima mpaka Rais anapotoka madarakani kwa kushitakiwa. Kwa faida yetu wote hapa Katiba inasema "......Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshitaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii"

  mbunge atapoteza sifa ya kua mbunge pale raisi atakapolivunja bunge kama ilivoonyeshwe katka ibara ya 90(2)(a mpka e)? - Hapana hawezi kupoteza sifa za kuwa Mbunge, sababu sifa za mtu kuwa Mbunge zimeelezwa kwenye Ibara ya 67 (1) na kwa Rais kulivunja Bunge hiyo haimuondolei mtu au mbunge sifa za kuwa mbunge. Sababu ambazo zinamfanya mtu kukosa sifa za kuwa Mbunge zimeainishwa kwenye Ibara ya 67 (2).
  Hivyo ndio navyoona kwa mujibu wa maswali yako.
   
Loading...