Naomba kujua EFD.mfumo wake

mbwili

Member
Feb 13, 2017
8
1
Je inakuaje kama nitanunua bidhaa bila vat mimi nikauza kwa kutumia Efd .ukizingatia kuna bidhaa zinapatikana kwa wamachinga.
 
Inategemea kama na wewe umesajiliwa na VAT basi efd yako nayo itakata VAT...kama haujasaliwa basi haitokata VAT..
 
Sawa@Babu Kivu lakini wamachinga hawajasajikiwa ktk VAT je, nkinunua bila EFD na nkauza kwa EFD huoni kwamba kuna uwezekano wa kupata loss mkuu
 
Tatizo kubwa sheria za kodi ya nhi yetu ni copy & paste kitu ambacho ni tatizo wawe wanaangalia hata uhalisia wa maisha ya mtanzania.
Kungekuwa na uwezekano ningeomba serikali ya awamu ya tano iangalie suala hili kwa jicho lingine na kufanyia marekebisho baadho ya vipengele vya sheria za kodi ili kuweza kuinua hata wafanyabiashara wadogo.
 
Kwanini makonda jamani huyu nani yupo yuma yake
 
Nunua bidhaa yako, ongeza bei, ujue kabisa kama ukiongeza VAT itakuwa how much..sioni kama kuna namna nyingine. Ukiangalia hata wanja wa machinga na shear illusions etc bei tofauti kabisaaa, ongeza tuu bei wananchi tukome
 
Hivi Kama haufanyi cash sales itakuwa ni efd receipt au invoice
 
utajaza mwenyewe ila tra mwisho wa mwezi wanataka vat yao! kama hujui kupanga bei ukajua faida yako ni ipi ndo utajiju
 
Kuna aina mbili za watumiaji wa EFD. Wale ambao wamesajiliwa na VAT na wale ambao hawajasajiliwa na VAT. Wale ambao wamesajiliwa na VAT nao pia wanaweza kuwa wanauza bidhaa ambazo zinatozwa VAT na nyingine hazitozwi na VAT, setting yake inafanyika kwenye mashine. Lakini kwa wale ambao hawajasajiliwa na VAT wao wananunua bidhaa zao wanaongeza faida yao wanauza kwa kutoa risiti za EFD na mashine zao hazikati VAT. TRA wanachohitaji ni kupata uhalisia wa mauzo yako ili kuepusha ukadiriaji wa kodi usiokuwa na uthibitisho. Na hii inamsaidia mfanyabiashara kujua amenunua kiasi gani, ameuza kiasi gani na amepata faida kiasi gani, alafu akiondoa gharama nyingine kama umeme, maji, muuzaji, usafirishaji nk. Unapata faida halisi ambayo ndo kodi inatozwa hapo.
 
Sawa@Babu Kivu lakini wamachinga hawajasajikiwa ktk VAT je, nkinunua bila EFD na nkauza kwa EFD huoni kwamba kuna uwezekano wa kupata loss mkuu
Utapataje hasara? EFD iko kuwarahisishia tra kujua umeuza kiasi gani. Kama umesajiliwa VAT itawasaidia wao na wewe kujua upeleke VAT kiadi gani.

Ukinunua kwa chinga au kwa mwenye VAT unachotakiwa kufanya ni kupanga bei itakayokupa faida.
 
utajaza mwenyewe ila tra mwisho wa mwezi wanataka vat yao! kama hujui kupanga bei ukajua faida yako ni ipi ndo utajiju

Aiseee, leo ndiyo nimeona ukimjibu mtu vibaya kiasi hiki.

Nawakataza waleta posa kuileta kwa wazazi wako, maana niliona kuwa "unatafuta bado uko miss"
 
Sawa@Babu Kivu lakini wamachinga hawajasajikiwa ktk VAT je, nkinunua bila EFD na nkauza kwa EFD huoni kwamba kuna uwezekano wa kupata loss mkuu
Unamaanisha ukanunue kwa Machinga ili nawe ukauze?...
Kawaida machinga anauzia mtumiaji si mfanyabiashara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom