Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,661
Jf nadhani hamshindwi jambo lolote ikiwemo pamoja maoni mbalimbali nataka kuanza biashara ya kuuza vyombo vya nyumbani mtaji wangu ni m3 sehemu ya kuuzia ninayo lakini naona ni bora nitafute kitu cha kuchanganya hapo angalau kila siku nipate elf50
================================
==========================================
MAJIBU
==============================
================================
Wadau wenye kujua biashara hii naomba watujuze undani wake, naona inawatoa watu wengi.
Kuna vitu vya lazima vinunuliwe mf. Glass, vikombe, vijiko, sahani, masufuria, mabeseni, ndoo, majagi n.k
Naomba kufahamu yafuatayo:
Je mtaji wake ni kiasi gani?
vitu vinavyotoka sana ni vp?
Vitu gani vya kuzingatia ili uifanye biashara hii kwa ukamilifu?
Asanteni
==========================================
MAJIBU
==============================
Mm nimefungua duka la vyombo huu ni mwaka wa tatu sasa ni biashara ambayo inauzika mda wote na ina faida kubwa ingawa ina changamoto zake kwa sasa hadi inafanya nianze kuiogopa.
Ina vitu vingi vya kuvunjika hivyo yakupasa kuwa mwangalifu sana ktk usafirishaji na upangaji wake, mizigo yake ni mikubwa ambayo inaumiza sana ktk transport unaweza safirisha mzigo wa thamani ndogo kwa bei kubwa kutegemea na ulivyokaa, mfano majaba, box za chupa ya chai, ni biashara ambayo ina lazima shamba uwe na store kwayo kama biashara yako haitembei sana utatumia pesa nyingi ktk kulipia fremu, kujaa kwa vyombo feki hasa vya plastic wachina,na wakenya wameteka bidhaa za plastic ambazo ni feki kwayo ukidill nazo ujue kila siku utapokea kesi, pia sasa na chupa za chai
Na wateja wakubwa wa vifaa vya jikoni mtumba ni middle class wa TZ,maskini wananunua vyombo made in TZ brand za CELLO na plastic products zilizotengenezwa tanzania.
Sababu kubwa ni kuwa vitu vya mtumba vina ubora,vitadumu muda mrefu etc.
binafsi sifagilii vitu vya mtumba kwani vinashusha UTU kiaaina,natumia vitu used kwa lengo la kuunga mkono Recycling for the environment.
Mtoa Mada, nenda mwenge kuna maduka ya vitu used vya jikoni. Watakupa muongozo.ila nahisi ulaya wanavichukua bure kwa lengo la kutoa misaada Africa