Naomba kujua ABCs za biashara ya vyombo vya nyumbani(jikoni)

Mm nimefungua duka la vyombo huu ni mwaka wa tatu sasa ni biashara ambayo inauzika mda wote na ina faida kubwa ingawa ina changamoto zake kwa sasa hadi inafanya nianze kuiogopa. Ina vitu vingi vya kuvunjika hivyo yakupasa kuwa mwangalifu sana ktk usafirishaji na upangaji wake, mizigo yake ni mikubwa ambayo inaumiza sana ktk transport unaweza safirisha mzigo wa thamani ndogo kwa bei kubwa kutegemea na ulivyokaa, mfano majaba, box za chupa ya chai, ni biashara ambayo ina lazima shamba uwe na store kwayo kama biashara yako haitembei sana utatumia pesa nyingi ktk kulipia fremu, kujaa kwa vyombo feki hasa vya plastic wachina,na wakenya wameteka bidhaa za plastic ambazo ni feki kwayo ukidill nazo ujue kila siku utapokea kesi, pia sasa na chupa za chai
 
Habari zenu Businessmen and Businesswomen

Mimi ni binti ninayependa sana kufanya biashara ya vyombo vya nyumbani. Nimehangaika nimefanikiwa kuhifadhi milioni kadhaa ambazo nimgependa kuziwekeza kwenye biashara hiyo.

Tatizo nililonalo ni kukosa mtu wa kunieleza biashara hii inaendaje. Nina ufahamu kuwa vyombo vingi hasa vya udongo vinakuwa imported kutoka nje ila sijui ni nchi gani na utaratibu wa kuvileta uko vipi.

Nitafurahi sana nikipata mtu aidha mwenye uzoefu na biashara hii na angependa kuona mwingine anafanikiwa katika biashara hii au anayeweza hata kunielekeza mahali nitakapoweza kupata taarifa sahihi.

Natanguliza Shukrani.
 
Ushauri wangu mimi, tembelea kwenye hayo maduka, omba ukutane na mwenye duka kisha muulize kuhusu biashara hiyo, akiwa na roho nzuri atakupa mchanganuo woooote bila uchoyo, hasa maduka ya Waha hawanaga roho mbaya wale.
 
Kuna sehemu naonaga watu wananunua kariakoo ,,kwa wachina hivi,,mitaa tatizo siijui majina,,ila ni kule wanauza vyombo,,karibu na depot ya azam
 
Nimetuma container 2 from Canada za Vyombo vya mtumba. Sikupata faida sababu ya mapungufu kadhaa. Moja ni mtaji ulikuwa mdogo hivyo container haikujaa. Mbili ni exchange rate kati ya dollar na shillingi. Tatu ni ushuru
 
Na wateja wakubwa wa vifaa vya jikoni mtumba ni middle class wa TZ,maskini wananunua vyombo made in TZ brand za CELLO na plastic products zilizotengenezwa tanzania.
sababu kubwa ni kuwa vitu vya mtumba vina ubora,vitadumu muda mrefu etc.
binafsi sifagilii vitu vya mtumba kwani vinashusha UTU kiaaina,natumia vitu used kwa lengo la kuunga mkono Recycling for the environment.

Mtoa Mada, nenda mwenge kuna maduka ya vitu used vya jikoni.watakupa muongozo.ila nahisi ulaya wanavichukua bure kwa lengo la kutoa misaada Africa
Good idea
 
Sorry make me understand! Kila siku update 50 as a profit au uuze si chini ya fifty?
 
Nimetuma container 2 from Canada za Vyombo vya mtumba. Sikupata faida sababu ya mapungufu kadhaa. Moja ni mtaji ulikuwa mdogo hivyo container haikujaa. Mbili ni exchange rate kati ya dollar na shillingi. Tatu ni ushuru
Mku naomba Msaada ktk hili Canada ulienda kununua mwenye na kusafirisha.
Mfano nilikuwa na rafiki yangu yeye alikuwa England alitafuta contena akawa anamka saa kumi na moja kwenda ktk vile vituo vidogo vya kukusanyia takataka kila alichokuwa anakikuta kama Radio, TV, Friza, Friji, Ovena, Pasi, Feni, compute, Print, Photocopy machine ,Deki za tv,projecta,Verehani,Mashine za Kukata miti yaani kila alichokiona kinafaa kwa huku kwetu.Akisha vikusanya anavitengeneza then anapanga ktk contena akawa anatuma ndugu zake wanauza.
Hata baadhi ya Wapemba wengi biashara hii waifanya sana lakini kwa sasa kwa England kama imeingiliwa na raia wa nchi nyingine. Huko Canada sijui ila ukiweza kufanya hii Issue utaniambia siku zote ulikuwa wapi
 
Habari Wana jamvi muhimu kwa vijana.

Natanguliza salamu za dhati kwenu...
Suala naloleta mezani ni kwa wenye uzoefu wa biashara ya vyombo vya ndani.

Nikimaanisha
Bakuli, vikombe
Mabeseni
Majaba
Na KADHALKA

Kwa wenye uzoefu tafadhali nina mambo naomba kuyajua na kama kuna mambo ya
Umuhimu mtaya analyse.
Kwa kuanzia nina capital ya 1m
Vyombo vya plastics mfano vikombe vyupa
Vya chai bakul na kadhalka naweza pata wapi kwa bei nzuri kariakoo pia kuna
Vijana wenzetu wanaofanya hii biashara utakuta wamevimwaga wanauza 200 kila kitu au 500 pia wao wananunua kwa bei ipi
Mpaka wanaeza fanya vile au pia mpangilio upi unawawezesha kupanga katika price zile na profit inakuaje kwa wale ( to which ukiwauliza hawasemagi, wengine watakuambia tu nimeshikiza ya mtu ).

Angalizo: kama hufaham kaa tusubiri mawazo pengine nawe utafaidika au mtag unaejua anafaham wote tufaidike.

Ahsanteni.
"business is life"
 
Back
Top Bottom