Naomba Kujiunga Nanyi

Simplelady

Member
Oct 26, 2009
44
22
Hello wana Jamii.

Mimi naitwa simplelady, napenda kujiunga kwenye forum yenu.

Napenda kuwafahamu na pia kujua taratibu za humu ndani.

Ahsante
 
karibu sana mkuu!naomba umpe nafasi shemeji chrispin ndani ya moyo wako!NAAMINI ATAKUPA KILE UNAKIOTA KILA SIKU.

jukwaa la mapenzi,na mahusiano.

hivi wewe ni HE?...AU SHE?
 
karibu sana mkuu!naomba umpe nafasi shemeji chrispin ndani ya moyo wako!NAAMINI ATAKUPA KILE UNAKIOTA KILA SIKU.

jukwaa la mapenzi,na mahusiano.

hivi wewe ni HE?...AU SHE?

Hahaha! Shemeji bana! Naamini bibie atakuwa amekuelewa na atatenda kama ulivyomshauri. (kama anataka mafanikio- siyo off point hii bwashee)
 
Hahaha! Shemeji bana! Naamini bibie atakuwa amekuelewa na atatenda kama ulivyomshauri. (kama anataka mafanikio- siyo off point hii bwashee)

naam!uzuri wa huyu mchuchu kwanza yupo simple!tatizo ni kwamba bado hajajua kutuma pm,lol!sijui tutampataje huyu leo aje tegeta by-night
 
naam!uzuri wa huyu mchuchu kwanza yupo simple!tatizo ni kwamba bado hajajua kutuma pm,lol!sijui tutampataje huyu leo aje tegeta by-night

Hahahahaha! Sasa hivi lile lijamaa letu litakuja huku kutuchokoza. (siyo off point hii, natahadharisha mapema kabisa)
 
wapwa leo JF ni neema kweli, yani huyo ni shori wa 3 anarejista leo!!., duh
 
Hahahahaha! Sasa hivi lile lijamaa letu litakuja huku kutuchokoza. (siyo off point hii, natahadharisha mapema kabisa)

kule nimempa kaunta-attack ya ajabu kama torress jana!lol.akija huku atakuwa anataka nimpige wash(hapa nazungumzia pool-table.NA SIO OFF-POINT)
 
Nina wasiwasi na huyu wa sasa hivi, anasound kama dume moja humu ndani.

duh, hebu ni-PM.
ujue siku hizi kuna ishu nyingi kama za kina semenya, kam za kenya hapo juzi, zingine pia indirect way zinaweza tokea hapa JF kwa dume kujifanya jike kwa kubadilisha jina!.
 
Hello wana Jamii.

Mimi naitwa simplelady, napenda kujiunga kwenye forum yenu.

Napenda kuwafahamu na pia kujua taratibu za humu ndani.

Ahsante

MIMI NITAKUSAIDIA SOMA MASHARTI YA HII JF Mkuu wangu MAGEHEMA,

Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti. Tukiwa na uwezo wa kufanya hosting hata BURE kwa website za watanzania.

Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni karibia $900 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili karibia 8,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 80,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

Benki zetu (hapa naongelea NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo wa Dar es Salaam.

Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

Njia ya nne ni kwa kutumia email ya macdemelo@gmail.com
kwenye hii link: https://www.payoneer.com/webapps/Load/LoadToPage.aspx

Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.
 
Hello wana Jamii.

Mimi naitwa simplelady, napenda kujiunga kwenye forum yenu.

Napenda kuwafahamu na pia kujua taratibu za humu ndani.

Ahsante

Karibu JamiiForums.com (A Welcome Note)
Tunafurahi umetutembelea. Ni faraja kuwa mwanachama wa bodi yetu. Heshimu uliowakuta kwenye bodi hii. Tunawaheshimu wanachama wetu na kuwapa thamani sawa.

Tunatoa UHURU WA KUONGEA. Kama mada inakukuna au kukugusa kwa kiwango ambacho unaona lazima utoe majibu jisajili na kutoa ufafanuzi yakinifu.

Ieleweke kuwa, Yaandikwayo hapa ni mawazo ya wateja wetu na si msimamo wa JamiiForums.com ama vinginevyo. Lugha za matusi hazitavumiliwa!

Tutashukuru pale ukiona jambo baya ukatufahamisha tulifanyie marekebisho haraka kabla hujakashifu au kutoa lawama. Sisi ni binadamu na tuna mapungufu yetu.

JamiiForums Administration
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom