Madhara ya kukuwaza sana, nakutaka radhi mjoli wa Bwana. Hivi mulugo mzee wa zimbabwe walisema ulimi umeslide eh?
hahahaaaa.... umechelewa!
Sioni dhambi kabisa, kutokwenda kanisani si dhambi kwa jinsi nionavyo!
Hali zenu wadau wa MMU
Kwanza niwaombe radhi kwa yale ninayotaka kuuliza ili kupatiwa ufafanuzi....
Kwa utafiti mdogo niliofanya, nimegundua asilimia 99 ya ndoa za siku hizi hufungwa baada ya wanandoa hao watarajiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi... wengine mpaka wamekwenda mbali wakabeba mimba... wengine wameishi pamoja.
Swali langu ni kwamba huwa wanakwenda kuhalalisha mahusiano ama kufunga ndoa takatifu? kuna haja gani ya kufunga ndoa kanisani / msikitini wakati mshafunuana vya kutosha????
Kwa mawazo yangu nahisi hii ndo sababu ya ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu hazina mibaraka bali laana.....
charminglady
Namtakia kila lililojema aliekutwaa au atakaekutwaa nikiamini ndoa ilifungwa/itafungwa bila kujali nini kilitokea hapo kabla, maana
kutubu humtakasa mtu na kumfanya mpya.
kama kuishi pamoja ndio kufunga ndoa kanisani/msikitini huwa wanaenda kufanya nini??
Kitu alichouliza huyu dada ilikuwa ni rahisi sana, hakukuwa na kuweka strong words as if alimpointout mtu. Sioni kama mmemuelewesha zaidi ya KUMKARIPIA.
Ki ukweli siku hizi hakuna ndoa, zaidi ya ndoano, katika vitabu vya Mungu hakuna kinachohalalisha uasherati, ukizini na kuzaa kabla ya ndoa ni haramu. Mwenye kubisha abatilishe vitabu vya dini.
Kubariki ndoa.
Thank you! You hit the nail on the head.
Can't stand the holier than thou tone of this thread!
Huu utafiti wako ni feki na hizo sababu unazosema zinasababisha ndoa nyingi kuvunjika ni hisia zako kwa sababu hata huu uzi unaonekama sio unataka kufunguliwa macho ila kuna kitu kilichokusibu. Pole sana.Hali zenu wadau wa MMU
Kwanza niwaombe radhi kwa yale ninayotaka kuuliza ili kupatiwa ufafanuzi....
Kwa utafiti mdogo niliofanya, nimegundua asilimia 99 ya ndoa za siku hizi hufungwa baada ya wanandoa hao watarajiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi... wengine mpaka wamekwenda mbali wakabeba mimba... wengine wameishi pamoja.
Swali langu ni kwamba huwa wanakwenda kuhalalisha mahusiano ama kufunga ndoa takatifu? kuna haja gani ya kufunga ndoa kanisani / msikitini wakati mshafunuana vya kutosha????
Kwa mawazo yangu nahisi hii ndo sababu ya ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu hazina mibaraka bali laana.....
kufunga ndoa na kufanya harusi ni vitu viwili tofauti...
mkiishi pamoja ni 'kufunga ndoa'
iliyobaki ni kufanya harusi
the Boss bora uwafahamishe maana zamani watu walikuwa wanaoana bila kuvulumushana kulingana na maadili yaliyokuwepo, binti hajawahi kufanya tendo la ndoa na wanaume vile vile, ila ilikuwa ikifahamika kuwa jogoo la mwanaume halipandi mtungi basi binti atarudi kwao na ndoa inavunja immediatelly, sasa siku hizi utapata wapi mvulana ambae hafanya ngono au msichana ambae ni bikira ili waoane? na ilikuwa inatokea msichana labda ameenda kusenya kuni anakimbizwa na mvulana na akishamkamata tu harudi kwao inatumwa taarifa wanafuata mahali mambo ya ndoa baadae, so haya mambo ni kumwomba mungu tu unapokuwa katika hicho kipindi akuongoze ili ufunge ndoa kabisa kabla ya kukaa pamoja then baadae mnafunga ndoa, nimalizie kwa kusema kuwa hata hivyo ndoa nyingi zimefungwa kabla ya kukaa pamoja na zimevunjika na zipo zilibarikiwa baada ya miaka hata kumi na tano na wanaishi kwa furaha.