Naona hapa unachanganya vitu viwili: umiliki wa chuo na utashi wa viongozi/watendaji wa chuo kuheshimu sikukuu za kitaifa. Kimsingi haya ni mambo mawili tofauti ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja. Tatizo hapa si nani anamiliki chuo, bali ni kwa nini uongozi wa chuo unashindwa kuheshimu sikukuu za kifaifa? Nafahamu IFM ni mali ya serikali chini ya wizara ya fedha. Sasa kwa nini mkuu wa chuo na management yake wameamua kesho muendelee na masomo ndio swali unaloweza kutafutia majibu kutoka kwenye uongozi wa chuo na sio JF