Mzembe flani
Senior Member
- Jul 1, 2019
- 190
- 208
Hapa umemshauri kimbio zaidi ila kwa maintainance nafuu ni heri achukue altezza yenye injini ya 1gFE, kwasababu spea zake zinapatikana kwa wingi kwakuwa injini hiyo ipo kwenye magari mengi tofauti mf;gx 100 zote (cresta, mark ii & chaser) mark ii grande gx 110, verossa na kadhalika ilhali injini ya 3sGE ipo kwenye toyota altezza tuu hivyo ni injini adimu na vipuli vyake ni ghali. Kwa mfano wiki iliyopita nimeulizia coil ya plug ya altezza 3sGE shaurimoyo ikawa inacheza kwenye laki ilhali coil za 1g ni elfu 40. Injini ya 3sGE used kutoka Dubai ni milioni 3, injini ya 1g used kutoka Dubai complete sina uhakika ni bei gani ila mswaki nasikia mpaka laki 5 unapata. Ila kwa mwendo 3sGE inatembea kuliko 1gfe na akipata yenye manual transmission basi hata crown za 4gr-fse atakuwa anazipa dozi.Altezza Toyota
Legacy Subaru
Wote ni Wajapani..ila wana philosophy tofauti..!
Toyota Altezza imekuja na options 2 za engine 4 cylinders 3S na 6 cylinders 1G..3S kwenye makaratasi ina nguvu zaidi ya 1G..ila 1G ni imara kweli kweli..!
Kama unachukua 3S jitahidi iwe manual..!
mimi sipo mjini ya dar mzee, niko mjini iringa mizunguko sio mingi, pia route za mkoa kwa mkoa ni moja ndani ya miezi miwili na haizidi 3. ndani ya miezi miwili.Alteeza ni Habari nyingine, iyo ni sport-car old fasion - tafuta ile ya engine ya YAMAHA G-20 Hutojutia Gari inakimbia mnoo. Ila jipange kwenye wese town trip daily Cost si chin ya mafuta ya Elf 30,000/=.
kwanini account isome 5M plus mkuu!?..Very simple, zote ni gari nzuri but nunua kama uta afford 40k each day ya mafuta na at list Bank account isome 5M plus as balance
“MANENO YANGU SIO SHERIA”
naomba uidadavue niifaham vyemaNenda na Subaru legacy
Kuna subaru zenye turbo na zisizo na turbo. Gari zenye turbo zina tabia tofauti kidogo na gari zisizo na turbo ni vyema ukafafanua legacy unayovutiwa nayo ni ipi kati ya hizo. Pia design ya injini ya subaru mpangilio wake wa piston ni tofauti (boxer) design hii inazisumbua hizi gari kwenye kutunza oil baadhi ya vifaa kwenye injini zake vikianza kuchoka haswa seals za oil hivyo ni makini kuwa unaichunguza kiwango cha oil mara kwa mara. Kuna baadhi ya matoleo ya subaru i.e wrx na wrx sti (imprezza zenye turbo) zina ugonjwa wa kuunguza cylinder head gasket japokuwa mara nyingi husababishwa na uendeshaji wa mtu japokuwa sina uhakika kuhusiana na tatizo hilo kwa subaru ambazo hazina turbo. Huo ndo ufahamu kidogo nilioung'amua kwenye subaru. Wajuzi wataongezea zaidi.naomba uidadavue niifaham vyema