Sio mwamba wa Networking ila nahisi nafahamu kitu kuhusu NAS.
Chukulia una PC yako desktop ya kawaida, ili u access vitu vyake lazima uwe nayo hapo, huwezi access mafile ukiwa mbali nayo.
Hilo tatizo likaja zibwa kwa kutumia NAS, Hapa unakua na PC yako unaweka Hard disk zako za kutosha au SSD zenye mafile yako yote mfano picha, nyimbo, movie, documents etc, then unaiconnect kwa internet ya nyumbani na kuiacha ifanye kazi masaa 24.
Wewe unakua na log in details za hiyo computer yako, so hata ukiwa mbali na PC yako ila una internet access unaingia tu na kucheki movie zako au nyimbo.