Naomba kufahamishwa

Naomba kufahamishwa

Nambayaya

Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
28
Reaction score
7
Ndugu wana JF naomba kufahamishwa kuhusu upatikanaji wa passport ya kusafiria kwenda nje ya nchi kama South Afrika. kwa muda gani naweza kupata passport na vip gharama zake zinakuaje? Kwa anaefahamu tafadhari anijulishe kwa hili.
 
kama upo dsm nenda ofisi za wizara ya mambo ya nje utapata maelekezo yote ila bei kamili ya passport ni shilingi 50000/=
 
Usi pm mtu yoyote. na usitoe rushwa hhata elfu moja kwani utakayempa hela hahusiki na pp. Nenda pale Kurasini uhamiaji. jaza fomu. lipa elfu hamsini na ndani ya siku saba za kazi utapata pasport halali. Jiepushe na walaghai utapewa pp pori. any problem please ni PM mimi nimuwashie mtu moto hatakaa aausahau mapema
 
Asante nashukuru kwa taarifa wakuu je? naweza kupata chini ya siku saba kama 3 au nne
 
Kama unacheti cha Daktari kwamba unakwenda kutibiwa au kusindiiza mgonjwa au barua yoyote ya kionyesha dharula hata ndani ya siku moja unapata PP. Idara ya uhamiaji imejirekebisha mno mkuu. na ukimpa mtu rushwa pale Kurasini nakuhakikishia atawatonya TAKUKURU pale pale.
 
kama upo dsm nenda ofisi za wizara ya mambo ya nje utapata maelekezo yote ila bei kamili ya passport ni shilingi 50000/=

Acha kumwingiza kichakani mwenzio..ni idara ya uhamiaji wizara ya mambo ya ndani.
 
Acha kumwingiza kichakani mwenzio..ni idara ya uhamiaji wizara ya mambo ya ndani.


teh teh na ndo maana upo wewe unisahihishe mkuu nimechanganya japo kupitia mistake yangu angefanikisaha
 
Kama upo bagamoyo nenda uhamiaji ofisi zao ni jirani na ofisi za dc!
Kama kibaha jengo la mkuu wa mkoa, ghorofa namba 3
 
nashukuru wadau kwa kunielekeza mi nko hapa Dsm hvo ni nina uhakika wa kusema ntafata taratibu sahihi ktk kufatilia PP. asante
 
Back
Top Bottom