Naomba kufahamishwa kuhusu Mbeya.

Naomba kufahamishwa kuhusu Mbeya.

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,484
Habari yenu wakuu?

Mi naomba tu kwa wale wenyeji wa Mbeya, au hata ambao wamewahi kufika tu watoe uzoefu wao hapa jamvini kwa faida yangu na wengine wote ambao wako interested kupafahamu Mbeya.

Sijali sana eneo, sijui Kyela au wapi wapi, nataka kujua sehemu zote tu.

1. Gharama za maisha zikoje ukilinganisha na sehemu nyingine? (Chakula,Nyumba za kupanga mf. chumba kimoja cha self au chumba na sebule kinaweza kupatikana kwa bei gani? )
2. Hali ya hewa?
3. Biashara gani ambayo haijasambaa sana (mf. Maduka ya nguo za watoto/watu wazima, restaurants, saluni,internet café n.k)
4. Shule nzuri za chekechea kuanzia 2yrs (gharama na upatikanaji).
5. . .na vitu vingine vingine tu ambavyo unadhani mgeni akijua vitamsaidia. Haswa anaefikiria kuhamia Mbeya na kuanza maisha.
 
We njoo bana, unauliza kwa mbali kwanini? Maisha mazuri sana kwa ujumla njoo tu
 
mbeya ni mji wa kawaida sana bado haujawa wa gharama kama arusha ingawa una pato kubwa kwa taifa kuliko arusha.....kama umeweza kukaa majiji makubwa kama dar na Arusha mbeya ni mji laini sana kuishi
 
Kwanza: Wenyeji ni Wasafwa.Japo walio wengi hawaishi mjini bali pembezoni ya mji. Wakazi wengi ni Wanyakyusa na Wakinga, japo pia yapo makabila mengin:Wanyiha,Wanyamwanga,Wandali,na mengineyo mengi.

Maswali yako:

1. Gharama za maisha zikoje ukilinganisha na sehemu nyingine? (Chakula,Nyumba za kupanga mf. chumba kimoja cha self au chumba na sebule kinaweza kupatikana kwa bei gani? )Japo ni moja ya majiji ya Tanzania,lakini gharama yake ya maisha ni nafuu sana:chakula, usafiri hauna foleni.Kwa maisha ya kawaida Tshs 5000-10000 inatosha kwa siku. Nyumba ya kupanga inategemea na eneo.Block T,Sae,Forest Mpya,Uzunguni (Kati ya 200000-1000000) kwa mwezi. Maeneo ya kawaida: 50,000-150000 kwa mwezi
2. Hali ya hewa?Ni baridi Mei-Agosti usiku inaweza kufikia nyuzi joto 0 kwa baadhi ya siku wakati wa usiku mchana nyuzi 15 jotoridi. Ila kwa kawaida joto huwa kati ya nyuzi 28-15 siku za kawaida. Ni mji wenye vumbi sana hasa wakati wa kiangazi (Septemba)huwa kuna tufani ya vumbi...
3. Biashara gani ambayo haijasambaa sana (mf. Maduka ya nguo za watoto/watu wazima, restaurants, saluni,internet café n.k) Binafsi: naweza kushauri mgahawa (restaurant) wa kisasa.Mji ule una mapungufu hayo,pengine kwakukosa wageni wengi kama watalii? Duka la nguo unaweza,ila jiandae kupambana na Wakinga a.k.a Wachaga wa Mbeya.
4. Shule nzuri za chekechea kuanzia 2yrs (gharama na upatikanaji). Jaribu UWATA, St.Mary's kwa kutaja chache kati ya nyingi.

Mchango wangu kwa ufupi.
 
karibu mbeya city me nipo huku one time nakula kitu cha malawi.
 
gharama za maisha ni za kawaida.........ie chakula bei zake ni za chin na za unafuu

hali ya hewa ni sehem yenye baridi
 
3. Biashara gani ambayo haijasambaa sana (mf. Maduka ya nguo za watoto/watu wazima, restaurants, saluni,internet café n.k) Binafsi: naweza kushauri mgahawa (restaurant) wa kisasa.Mji ule una mapungufu hayo,pengine kwakukosa wageni wengi kama watalii? Duka la nguo unaweza,ila jiandae kupambana na Wakinga a.k.a Wachaga wa Mbeya.
4. Shule nzuri za chekechea kuanzia 2yrs (gharama na upatikanaji). Jaribu UWATA, St.Mary's kwa kutaja chache kati ya nyingi.

Mchango wangu kwa ufupi.

hivi yule baba mwenye maduka ya nduo pale maeneo ya mwanjelwa bei zake ni cheap sana

anaitwa nani nimemsahau ila ni maarufu sana.nilisikia ukienda lile duka unakuwa uchi
 
ommymbwambo nimekubali,kweli unaifahamu Mbeya vizuri pia ukitaka vitu vya bei rahisi zaidi nenda Ilemi bajaji nauli ya daladala mboga za majani za sh 100 kwetu Mtwara sh 2500
 
hivi yule baba mwenye maduka ya nduo pale maeneo ya mwanjelwa bei zake ni cheap sana

anaitwa nani nimemsahau ila ni maarufu sana.nilisikia ukienda lile duka unakuwa uchi

Kitambo kidogo nmeukimbia mji wao.Ila hiyo maneno nnaikumbuka, ilikuwa habari ya "mujini sana".Nikikumbuka ntalirusha.Sawasawa?
 
Maisha ya mbeya ni rahisi sana,ila chukua tahadhari maana huko kuna matukio ya kila aina kuliko mikoa yote hapa Tanzania
 
Nilipoondoka mwaka juzi mwishoni Nondo ndio lilikua tatizo kuu pale Mbeya mjini sijui kwa sasa hali ikoje.

Maisha ya Mbeya ni rahisi sana ukilinganisha na majiji mengine.

Nenda kiroho safi mkuu.
 
ommymbwambo nimekubali,kweli unaifahamu Mbeya vizuri pia ukitaka vitu vya bei rahisi zaidi nenda Ilemi bajaji nauli ya daladala mboga za majani za sh 100 kwetu Mtwara sh 2500

Soko Matola ndiyo soko la Bei Chee kupindukia.

Viazi Mviringo debe moja ni 5000 unajaziwa plastic ya lita 20 na flat lita10.Maisha ya Mby ni cheap sana.
 
Mbea kila kitu ni rahisi,chakula,malazi,kama ni mkiristo makanisa karibu kila nyumba,kama unapenda totozi kule ni sawa na bure,huhitaji kumwaga vesi kali,kwa kweli mabinti wa mbeya wanatekeleza ile kanuni ya wamepewa bure nao wanatoa bure!
 
mie nilieko Arusha basi mbeya rahaa yani mboga shlng100 hahahaha wenyeji mpo mie nakuja
 
Back
Top Bottom