Naomba kufahamishwa gharama ya Floor slab

Habarini za saa hizi wana JF,

Nina mawazo ya kujenga shambani kwangu lakini ni kighorofa cha floor moja tu ambapo juu nitaweka Master bedroom, ofisi na balcon tu kwa ajili yangu na mke wangu ila watoto na wageni watalala upande wa chini.

Sasa nilikuwa naomba kujua gharama za kupandisha slab na zile nguzo zake pamoja na beam yaani (skeleton structure) yote inaweza kufika kiasi gani?

Shukrani...
Kwani aliye ku dezainia hilo ghorofa lako hayupo? Kama ameku dizainia anashindwa vipi kukupa makadirio ya bei?
 
Kwani aliye ku dezainia hilo ghorofa lako hayupo? Kama ameku dizainia anashindwa vipi kukupa makadirio ya bei?

Ni Tatizo hilo
Hujui mtu anayedesign na kupiga hesabu ni watu wawili tofauti na wanakwenda shule kwa ajili hiyo ??

Swali lililenga vilivyofanyika tayari practically sio theoretically
 
Kwa standards za kawaida, suspended slab inakuwa na thickness ya 0.125m.
8x8x.125 = 8 cubic meters of concrete.

Ambayo ni kama mifuko 70 ya cement.
7 cubic meters za kokoto.
4 cubic meters za mchanga.
Hii ni kama concrete ni M20 na ujatoa space ya ngazi (ngazi zipo kwa nje).

Steel kwenye suspended slab inatakiwa 80kg/cubic meter.
Kwenye 8 cubic meters utahitaji 640kg of steel (price index ya steel ni appr. 1000$/tonne).

Slab peke yake itakugharimu kama milioni 5 au 6.

Usisahau mabomba ya wiring.
Inatia moyo kusikia hivi....ila wazee wa msingi umegharimu milioni 80 Mungu anawaona
 
Chief mi naomba kujua estimates za tofali kwa ukuta kwenye kiwanja cha 15x18... natanguliza shukrani
kunena ili kujua idadi ya tofali kwenye kiwanja hicho, hebu fanya hivi- pima urefu wa tofali moja, ukishajua urefu wa hilo tofali (inaweza kuwa katika vipimo vya cm au inchi); tafuta urefu wa hizo kuta zako katika cm au inchi. Kisha gawanya, yaani urefu wa tofali gawanya kwa urefu wa ukuta - huo wa 15m na huo wa 18m. utajua ni tofali ngapi then zidisha mara course au mistari za huo ukuta! Utajua idadi ya tofali na kisha gharama zake! Changamasha BONGO!
 
Ni Tatizo hilo
Hujui mtu anayedesign na kupiga hesabu ni watu wawili tofauti na wanakwenda shule kwa ajili hiyo ??

Swali lililenga vilivyofanyika tayari practically sio theoretically

Architect ndiye kiongozi linapokuja swala la ujenzi hivyo yeye ndiye alitakiwa akuongoze kwenye haya yote uliyo andika hapa!

Architect ndiye angekuongoza na kukushauri QS gani atakufaa vivyo hivyo angekuongoza structural engineer gani atakufaa!

Sijui umeelewa?
 
Kanyumba katamu haka.
Nyumba yeyote ni TAMU upate tu

Fundi wa kupiga bati vizuri,

Upate Mtaalamu au wewe mwenyewe ujue kuchagua Rangi ya Nyumba yako inayotulia machoni..

Kwenye finishing Atleast jitahidi umalizie na Classic Material (Taa + Urembo)

Hata kama ni Single room Ikipigwa picha ikitupiwa hapa Lazima kimiminika kikutoke..
 
Habarini za saa hizi wana JF,

Nina mawazo ya kujenga shambani kwangu lakini ni kighorofa cha floor moja tu ambapo juu nitaweka Master bedroom, ofisi na balcon tu kwa ajili yangu na mke wangu ila watoto na wageni watalala upande wa chini.

Sasa nilikuwa naomba kujua gharama za kupandisha slab na zile nguzo zake pamoja na beam yaani (skeleton structure) yote inaweza kufika kiasi gani?

Shukrani...
Tafuta 80m mpaka ikamilike
 
Nyumba yeyote ni TAMU upate tu

Fundi wa kupiga bati vizuri,

Upate Mtaalamu au wewe mwenyewe ujue kuchagua Rangi ya Nyumba yako inayotulia machoni..

Kwenye finishing Atleast jitahidi umalizie na Classic Material (Taa + Urembo)

Hata kama ni Single room Ikipigwa picha ikitupiwa hapa Lazima kimiminika kikutoke..
Sasa nipe comnection ya fundi michael
 
Back
Top Bottom