Naomba kueleweshwa kuhusu cheque namba

fluid

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
363
235
Ningependa MTU mwenye kufanya utumishi serikalini au yeyote mwenye elimu anieleweshe cheque number ni kitu gani jinsi inavopatikana, anayeitoa, nk nk.. Akhsante.
 
Embu elezea kwa undani shida yako usaidiwe, maana inaonyesha ushatapelewa mahali wewe
Sijawahi kufanya kazi serikalini wala sina mpango. Kutapeliwa ngumu sana kwangu mkuu. Ninaisikia sikia tu lakini sijawahi kuelewa ni kitu gani.
 
Sijawahi kufanya kazi serikalini wala sina mpango. Kutapeliwa ngumu sana kwangu mkuu. Ninaisikia sikia tu lakini sijawahi kuelewa ni kitu gani.
Sasa kitu ambacho huna issue nacho watakia nini kukijua? Ok cheque number ni namba ya hundi na inapatikana kwenye hundi ( cheque). Aya sasa ushajua what next?
 
Nadhani usahihi ni Check Number na siyo Cheque Number. Hiyo Cheque Number inahusiana na cheque (hundi). Mengine wataendelea wenye uelewa zaidi.
 
Sasa kitu ambacho huna issue nacho watakia nini kukijua? Ok cheque number ni namba ya hundi na inapatikana kwenye hundi ( cheque). Aya sasa ushajua what next?
Ukiendelea na akili kama hizo utafika mbali sana. Learn everything and share. Una kiherehere. Huna kazi ndo maana. Unahisi utapewa ukiwa best Ku comment?
 
Nadhani usahihi ni Check Number na siyo Cheque Number. Hiyo Cheque Number inahusiana na cheque (hundi). Mengine wataendelea wenye uelewa zaidi.
Asante sana. Ata nilipo wanatumia neno check. Ila nikapata wazo Tanzania inatumika zaidi British English
 
Cheque number ni kama namba ya utambulisho wa mtumishi wa serikalini inayotumika katika kumbukumbu zake za mshahara...mara nyingi namba hii hupewa watumishi ambao mishahara yao hupitia (H)AZINA
Oh Asante mkuu.
 
Ukiendelea na akili kama hizo utafika mbali sana. Learn everything and share. Una kiherehere. Huna kazi ndo maana. Unahisi utapewa ukiwa best Ku comment?
Andika taratibu mbona mbio ndugu?
 
nadhani mtumishi yeyote aliyeajiriwa parmanently ana namba hii kwa ufupi ni utambulisho wa mtumishi ktk suala la malipo ya mshahara, ukiwa na check namba ndiyo utambulisho wa wewe kupata mshahara
 
Mtumishi Wa Serikali Anapoanza Kazi Huwa Hupewa Cheque Number Na Hazina.
Dhumuni La Cheque Namba Ni Mahusiano Yako Ya Miamala Yote Ya Kifedha Kati Yako Na Hazina.

Ukilipwa Mshahara Lazima Upitie Kwny Chaque Namba Yako, Ukikopa Pia Lazima Mkopo Ukatwe Kwa Cheque Namba Yako, Kama Kuna Posho Ya Pango, Ujuzi Na Nyinginezo Zote Hupitia Humo.

Hazina Wao Wanatambua Kwanza Cheque Kisha Lifuate Jina Lako.

Cheque Namba Huwa Ni Kama Account Namba Hazifanani Hata Siku1.
Mimi Nawe Tunaweza Kufanana Majina Yote Matatu Lakn Cheque Namba Haziwezi Kufanana.

Mfano Kama Mimi Nawe Tumeajiriwa January Cheque Namba Zetu Zitatofautiana Tarakimu1 Tu.
Mfano.
John, 2016-532670
Zuber. . . . . . . . . . . 71
Aisha. . . . . . . . . . . 72
Habibu. . . . . . . . . .73

Hata Ulifuatilia Mafao Au Michango Yako Yako Ktk Mifuko Ya Jamii Ni Lazima Utaje Cheque Namba Yako.

Hapo Umepata Picha Mkuu.
 
Mkuu Prosper C Manasse asante kwa ufafanuzi mzuri
JF Kuna Shida1, Mtu Hajui Kitu Badala Ya Kukaa Kimya Anaanza Kumdhihaki Yule Alouliza.
Much Know Never Know, Lazima Tifunzane Kwa Nidhamu Na Hekima Maana Mimi Najua Hili Lakn Lile Sijui Wewe Unalijua. Mambo Ya Kusanifiana Hayana Maana Kwa Mtu Mwenye Nia Ya Kujua.
 
Ukiajiriwa, unapoingizwa kwenye mfumo wa mishahara, huwa anayeingiza, Mara nyingi ni Afisa Utumishi yeye viambatanisho vikikamilika huwa jina lako linapewa applicant number, halaf Utumishi waki-approve ndipo unapopewa check number, namba ya ajira ambayo ni unique, hakuna MTU mwingine mwenye nayo
 
Mtumishi Wa Serikali Anapoanza Kazi Huwa Hupewa Cheque Number Na Hazina.
Dhumuni La Cheque Namba Ni Mahusiano Yako Ya Miamala Yote Ya Kifedha Kati Yako Na Hazina.

Ukilipwa Mshahara Lazima Upitie Kwny Chaque Namba Yako, Ukikopa Pia Lazima Mkopo Ukatwe Kwa Cheque Namba Yako, Kama Kuna Posho Ya Pango, Ujuzi Na Nyinginezo Zote Hupitia Humo.

Hazina Wao Wanatambua Kwanza Cheque Kisha Lifuate Jina Lako.

Cheque Namba Huwa Ni Kama Account Namba Hazifanani Hata Siku1.
Mimi Nawe Tunaweza Kufanana Majina Yote Matatu Lakn Cheque Namba Haziwezi Kufanana.

Mfano Kama Mimi Nawe Tumeajiriwa January Cheque Namba Zetu Zitatofautiana Tarakimu1 Tu.
Mfano.
John, 2016-532670
Zuber. . . . . . . . . . . 71
Aisha. . . . . . . . . . . 72
Habibu. . . . . . . . . .73

Hata Ulifuatilia Mafao Au Michango Yako Yako Ktk Mifuko Ya Jamii Ni Lazima Utaje Cheque Namba Yako.

Hapo Umepata Picha Mkuu.
Inakuja mkuu. Ahsante sana kwa kushare knowledge. Selfishness is destruction.
 
Kuna cheque namba na check namba, cheque namba ni namba ya hundi na check namba ni namba anayopewa mtumishi anapoanza kazi kama namba yake ya utambulisho.

Wengine wametoa maelezo ya check namba lakini wamekosea kuandika cheque namba. Hivyo mfanye marekebisho
 
Back
Top Bottom