Naomba kuelewa: Tofauti ya Wakili na Hakimu

Hakimu mtoa hukumu,wakili mtetezi wa mtuhumiwa,wote wamesoma sheria ila ili kuwa wakili ni lazima uende mbele zaid kuishia pale pale pa degree au diploma!,
 
Kuwa wakili lazima usome school of law na kuwa judge school of law sio lazima
 
Kwanza kabisa kwa mahitaji ya sasa ili uwe hakimu ama wakili. ni lazima usome fani ya sheria kwa ngazi ya degree hakimu na wakili wote ni wanasheria mgawanyo wa majukumu unaanzia hapa mtu anayetaka kuwa wakili mara baada ya kuwa amepata degree ya sheria anakwenda law school kwa mafunzo ya mwaka akifaulu anapaswa kuwa mwanachama wa chama cha mawakili TLS na kulipa ada stahiki .....baada ya hapo anakuwa wakili ...rasmi kwa kufanya kazi za uwakili....kwa upande wa hakimu huyu ni mwanasheria mwenye degree zikitangazwa kazi za uhakimu anaomba akiajiliwa anakuwa hakimu.....Tofauti ni kwamba hakimu kazi yake ni kusikiliza kesi na kutoa maamuzi...wakati wakili kazi yake ni kuwawakilisha ama kuwatetea watu wenye kesi zao mahakamani ...
 
Hakimu na Wakili cha kwanza kabisa wote ni wanasheria, utofauti unakuja hapa;

Hakimu ni mtoa maamuzi.. Hakimu ( Magistrate) akipanda ngazi huwa Jaji (judge).

Wakati Wakili (Advocate) ambaye kama nilivyokuambia ni mwanasheria ila anaweza kuchagua kuwa wa kujitegea ama anaweza kuwa wakili wa serekali (State Attorney)

Mkuu wa mawakili wa serekali ndio huyo Mwanasheria Mkuu(Attorney General)

Na mkuu wa Mahakimu/ Majaji anaitwa Chief Justice (Jaji Mkuu)

Hapo, utakuwa umepata mwanga kidogo.
 
Back
Top Bottom