Naomba kazi niweze kujikimu mimi na familia yangu

Mbona hujasema fani yako ni ipi?
 
Mkuu haueleweki wala hausomeki. Hujatoa hata Wasifu wako halafu unaomba kazi, kazi gani inaombwa au inatafutwa hivyo? Kuna shida upande wako. Kwanza mahusiano na jamii inayokuzunguka yalikuwaje? au yako vipi? Halafu kuna msemo unaosema Anaekupiga teke amekusogeza mbele. kama hauna chochote cha kufanya ili kupata kipato unakuwa unakosea sana kulalamila. Una simu kubwa pita hata sehemu wanakotengeneza au kuuza bidhaa/ biashara mbalimbali omba kuzipiga picha halafu uwatangazie biashara yao kupitia Whatsapp status ili upate kamisheni na uweze ku survive huku ukiendelea kutafuta kazi ya uhakika. Vilevie pita kwenye jukwaa la Biashara humu JF angalia threads mbalimbali kuna kazi ambazo unaweza ukazifanya bila kuajiliwa au bila mtaji.
 
Umeongea ukweli mtupu, makazini watu wana roho mbaya sana. Imagine hayo machozi ya hiyo familia halafu kuna watu wanafurahi kwa walichomfanyia, vijana tuna changamoto zetu lakini maboss wawe na utu na kuangalia nyuma ya hao vijana kuna familia zinawategemea, hasa maboss vijana wana hizo changamoto, vitu vya kijinga tu kisha anataka akukomoe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…