Naomba idadi ya matofali kujenga nyumba hii

mchepuko

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,192
Reaction score
1,418
View attachment 302892

Hello wakuu...

Nina ramani ya nyumba upana mita 7.5 na urefu mita 16.5... sawa na square meter 123.75

Haina mikunjo mingi sana ila ina sebule ya 4.5 by 5m dining, corridor, jiko, stoo, masters... vyumba viwili vya kulala na public toilet moja na front veranda.

Kiwanja kitakua na slope kiasi, sio sana...

Naomba makadirio ya matofali, cement, mchanga n.k. Design ya paa bado ila kama utaweza kunipatia nitashukuru...

Asanteni wakuu
 
Hongera kwa kuanza ujenzi. Kuna mada nyingi za ujenzi humu jaribu kuzitafuta. Ila wataalamu watakuja kudadavua & sisi pia tuta benefit.
 
Kwa details hizo tu unategemea upata hesabu ya tofali na kuchorewa paa?
Huyo aliyekuchorea ramani kama ni mtaalam halali ana uwezo wa kukupa estimation za vitu vyote hivyo unavyovitaka, ni dakika mbili tu wala haichukuwi muda.
 
Piga picha ramani uitume utapata msaada
 
Mkuu
-kama unampango wakutumia mil 30,40 na kuendelea kujenga nyumba na ili iwe nyumbani, sehem utaishinna familia na kujivunia baba wa nyumba, nakushauri utafute mtaalamu "architect" akuchoree kitu kinachoeleweka kitakacho include kichoro yote husika pamoja na picha za itakavyo onekana.
utamlipa kiasi flani ila utapata nyumba yenye value for money.
kwa maelezo yako hapo juu hujapata mtu sahihi aliekuandalia hiyo ramani.
ukaridiriaji wa matofali ya kujenga nyumba mara nyingi hua tofali 3000-6000 ikitegemea na design. ila pia itategemea utatumia zipi, za nchi 4,5,6 au hollow blocks, au interlocking bricks (hesabu yake ni tofauti) nk.
-ukishapata ramani ya kueleweka, onana na fundi muoneshe eneo na mchoro atakupa hesabu ya awali ya vinavyohitajika. sio tofali tu na cement, kuna mbao, kamba, mchanga, kokoto na vitu vingine vingi.
-naomba uchukulie ujenzi kwa umakini zaidi ili uwe na makazi bora na kiujumla wote tuwe na mazingira bora.
 
hello wakuu...

nina ramani ya nyumba upana mita 7.5 na urefu mita 16.5....sawa na squaremeter 123.75

haina mikunjo mingi sana ila ina sebule ya 4.5by 5m dining,coridoer,,jiko..stoo..masters...vyumba viwili vya kulala na public toilet moja na front veranda ...kiwanja kitakua na slope kiasi..sio sana....naomba makadirio ya matofali...cement..mchanga n.k..design ya paa bado ila kama utweza kunipatia nitashukuru....

asanteni wakuu

Ehe unajenga kwenye ardhi ya aina gani? Ina slope au n flat?
 
upo sahihi kabisa mkuu..ramani ambayo ni first draft ninayo na ananisubiri nimpe go-ahead ili amalizie final plan na roof plan zote...ila hofu yangu ilikua nisije nikampa go ahead ya plan ambayo itakua haitekelezeki au inatekelezeka kwa gharama ambayo sijajiandaa....wengi huwa tunafail apo tunaishia kujenga makumbusho.....

sijapenda kuatach ile first draft hapa kuhofia kuharibu kazi yake au kugawa plan bure....naomba nieleweke hivyo
 
Piga hesabu ya tofali 400 kwa..(4m x 4m)

Idadi = 400 x 124/16 = 3075 Blocks.
 
uwiano upoje!? upana mita 7 urefu mita 16!? hiyo humo ndani yamejaa makorido, kuta ili kukutia hasara za tofali na finishing. ungeweka hapa huo mchoro ili watalamu tudadavue vizuri. na pengine kukupa design ambayo ni economy na uchumi wa sasa ulivyo mgumu ktk ujenzi
 
Ungeweka floor kama hivi, watalamu wakusaidie, jukwaa hili ni kuelimishana na kusaidiana. Swali lako linategemea vipimo vya mchoro kupata takwimu halisi ya unachokihitaji.
 
View attachment RAMANI22.pdf
hello wakuu...

nina ramani ya nyumba upana mita 7.5 na urefu mita 16.5....sawa na squaremeter 123.75

haina mikunjo mingi sana ila ina sebule ya 4.5by 5m dining,coridoer,,jiko..stoo..masters...vyumba viwili vya kulala na public toilet moja na front veranda ...kiwanja kitakua na slope kiasi..sio sana....naomba makadirio ya matofali...cement..mchanga n.k..design ya paa bado ila kama utweza kunipatia nitashukuru....

asanteni wakuu
 
ungeweka floor kama hivi, watalamu wakusaidie, jukwaa hili ni kuelimishana na kusaidiana. Swali lako linategemea vipimo vya mchoro kupata takwimu halisi ya unachokihitaji.

mkuu tayari nimeweka ramani ila nisaidie kuiweka vzuri
 
uwiano upoje!? Upana mita 7 urefu mita 16!? Hiyo humo ndani yamejaa makorido, kuta ili kukutia hasara za tofali na finishing. Ungeweka hapa huo mchoro ili watalamu tudadavue vizuri. Na pengine kukupa design ambayo ni economy na uchumi wa sasa ulivyo mgumu ktk ujenzi

nimeweka mkuu nisaidie
 
Mkuu
-kama unampango wakutumia mil 30,40 na kuendelea kujenga nyumba na ili iwe nyumbani, sehem utaishinna familia na kujivunia baba wa nyumba, nakushauri utafute mtaalamu "architect" akuchoree kitu kinachoeleweka kitakacho include kichoro yote husika pamoja na picha za itakavyo onekana.
utamlipa kiasi flani ila utapata nyumba yenye value for money.
kwa maelezo yako hapo juu hujapata mtu sahihi aliekuandalia hiyo ramani.
ukaridiriaji wa matofali ya kujenga nyumba mara nyingi hua tofali 3000-6000 ikitegemea na design. ila pia itategemea utatumia zipi, za nchi 4,5,6 au hollow blocks, au interlocking bricks (hesabu yake ni tofauti) nk.
-ukishapata ramani ya kueleweka, onana na fundi muoneshe eneo na mchoro atakupa hesabu ya awali ya vinavyohitajika. sio tofali tu na cement, kuna mbao, kamba, mchanga, kokoto na vitu vingine vingi.
-naomba uchukulie ujenzi kwa umakini zaidi ili uwe na makazi bora na kiujumla wote tuwe na mazingira bora.

hivi button ya "like" imekwenda wapi? umenena vema sana..
 
upo sahihi kabisa mkuu..ramani ambayo ni first draft ninayo na ananisubiri nimpe go-ahead ili amalizie final plan na roof plan zote...ila hofu yangu ilikua nisije nikampa go ahead ya plan ambayo itakua haitekelezeki au inatekelezeka kwa gharama ambayo sijajiandaa....wengi huwa tunafail apo tunaishia kujenga makumbusho.....

sijapenda kuatach ile first draft hapa kuhofia kuharibu kazi yake au kugawa plan bure....naomba nieleweke hivyo

Sasa wewe unataka makadirio ya Bure na unaogopa kutoa hiyo mep. Naona umesahau ule msemo wa mkuu wako wa "ukitaka kula lazima uliwe"
 
Kiurahisi tafuta square metres za ukuta wako yani urefu mara upana kisha zidisha mara 9 i.e square meter moja huwa ni matofali 9 yakisimama au 14 yakilala
 
Back
Top Bottom