Naomba feedback kwa mliotumia haya mafuta ya parachute

nellwan

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
378
680
Habari.
Kwa wale mliotumia haya mafuta naomba mrejesho maana nataka kiyatumia.
 
Sijawahi kuyatumia lakini naona wengi wanayasifia. Subiri waje waliyoyatumia.
 
Mkuu asante kwa mrejesho. Naomba maelekezo namna ya kutengeza.
Ukitaka upate mafuta mengi inabidi utumie nazi nyingi... Inasemekana nazi mbovu ndo zinatoa mafuta mengi.
Kwa majaribio anza na nazi tatu au nne.
> Pasua na ukune nazi zako, chuja tui zito (lisiwe jepesi sana) weka kwenye chombo kinachoonesha (transparent)
> Acha kwenye hicho chombo ili maji na tui halisi vijitenge. Maji yatatuama chini na tui jeupe litakua juu. Kwa uangalifu toa lile tui na maji yamwage. (Hii si lazima sana ila inaokoa mda na mkaa/gesi, unaweza bandika tui zima tu kwenye jiko)
> Weka tui kwenye sufuria na uweke jikoni lichemke. Lichemke mpaka kukauka ndo mafuta yatajitokeza,
Mafuta yakitokea, yahamishe kwenye chombo kingine na rudisha sufuria jikoni.
> Endelea mpaka hamna mafuta yanayotengenezwa tena.
> Mafuta yako yakipoa Weka kwenye chupa au chombo kisafi na yafunge.

Wengine kuna vitu wanaongeza ili kukata harufu ya nazi. Sifahamu hapo sababu sijawai jaribu. Naioenda ile harufu ya nazi.

Kuna njia nyingi za kutengeneza haya mafuta ila ile njia ya kutochemsha inasemekana si nzuri, mafuta yanawai kuharibika.
 
Asante kwa maelekezo. Nitaleta mrejesho.
 
Mimi kichwa changu kibovu sana, yaani niliposoma mafuta ya parachute nikagoma kufungua uzi huu nikidhani kuwa mwaongelea vilainishi, sasa bahati mbaya wakati na bofya uzi mwingine nikajikuta niko huku, kumbe mwaongelea mafuta ya nazi. Basi sawa.
 
Mimi napaka mwili mzima kasoro kwenye nywele tu nice and lovely and yapo mororo tu Mwanzo mwisho Kopo la Tatu namalizia
 
Kama uso wako ni zoazoa unaweza kuyapaka tu tofauti na hapo mapele yatakujalia
Mamy wewe umetumia yapi Kati ya haya
00a2c250ccc6950492c204f3e6a0b730.jpg
 
Mimi hayakunipenda haya mafuta.nlipaka mwilini nkawa napauka kupita MaeleZo .
Ila wengine yamewakubali ..yakifanya kazi kwako yatumie tuu..watu tupo tofauti .
 
Back
Top Bottom