Naogopa kulala ndani peke yangu, nahisi kuna mtu simuoni

Tatizo dogo sana. Hapo ulipo piga magoti uliite Jina la Bwana Yesu mlinzi wa walinzi. Usijali hata kama hujawahi kwenda kanisani. Wewe mweleze Mungu na sali unavyojua wewe. Sali kemea kwa jina la Yesu. Muite Mungu Akusafishie nyumba hiyo Atume malaika wake wakulinde. Halafu kwa imani kabisa Ingia kitandani ulale. Hutasikia lolote na utalala usingizi mnono ajabu.

Kwa nini nakushauri hivi? Kuna siku moja usiku kama saa nne kule Usukumani nilikuwa peke yangu. Ili kufika nyumbani kulikuwa na kamto fulani hivi lazima ukavuke halafu pembeni kuna miti mingi ya michongoma na mitunduru. Basi kufika pale nikaona mbele yangu watu kama wanne hivi wana vijinga vya moto wamesimama huko niendako. Nikataka kutimua mbio lakini nilipogeuka nikawaona tena hata huko wapo. Basi nikajua kuwa nimezingirwa na hawa siyo watu wa kawaida mpaka nikadhani pengine haya ndiyo mambo ya akina Mch. Gwajima ya kuchukuliwa msukule. Wakati ule nilikuwa Mwadventista Msabato na katika makambi tulikuwa tunafanya mashindano ya kukariri mafungu ya Biblia. Basi hapo hapo nikakumbuka Zaburi 23 na nikaanza kusali kwa sauti kubwa mpaka nasikia mwangwi: Mungu Ndiye mchungaji wangu na sitapungukiwa na kitu. Nijapopita katika bonde la mauti sitaogopa mabaya...Nikatamka kwa sauti kubwa "Yesu nakuhitaji. Shuka Mfalme wa wafalme unipiganie. Waondoe hawa kama wana nia mbaya nami. Ondokeni kwa jina la Yesu..." Yaani mpaka jasho likanitiririka. Kuja kuinua macho sikuona kitu. Huyooo nikatembea mpaka home. Ajabu kesho yake nilikuwa nimechoka balaa. Na baadaye sana nilikuja kuwafahamu wabaya wale na ambacho walikuwa wamepanga kunifanyia. Na kiongozi wao alikuwa ni shangazi yangu kabisa tumbo moja toka nitoke na baba.

Tangu siku hiyo ndiyo nikajua kuwa jina hili Yesu lina nguvu za ajabu. Na cha kushangaza zaidi kuchelewa kote huko mpaka saa nne usiku nakatisha mtoni ni kwa sababu nilikuwa nafukuzia demu. Demu mwenyewe wala hakutokea. Imagine nilikuwa natoka katika harakati za kutenda dhambi lakini Mungu Alikuwa tayari kuniokoa. Ni wema na upendo gani upitao huu?

Sorry for a long story. Mkuu sali halafu uchape usingizi. Mungu Akulinde na kukubariki. Amen!
Nimependa ushuhuda wako. Yesu ni Simba kabila ya Yuda
 
Waungwana habari,hivi sasa naandika uzi huu ni saa nane na dakika 16usiku.nina usingizi ila naogopa kulala kwani nahisi kuna mtu chumbani kwangu.kibaya zaidi nakaa nyumba nzima peke yangu,nimeenda sebuleni ila napo naogopa sana,nahisi kuna mtu ananichungulia huku anacheka.hii inasababishwa na nini.maana kila nikitaka kusinzia nakwama.nashtuka nahisi kuna mtu.kwa mnajua niambieni nifanyeje ili niwe na amani,na ili nilale

Waambie ndugu zako wakupeleke hospital kabla hujaanza kuokota makopo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom