Naogopa kufa nikimfikiria mtoto wangu kubaki mwenyewe

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
16,621
27,567
Jamani nikiona Agness amefariki akiwa mdogo nasikitika kiukweli,vifo vya vijana wadogo vinauma sana ,nikiona mwanae naumia kaachwa hana hata kaka au dada yake ,nikifikiria na mimi mtoto wangu yupo mwenyewe tu ikatokea nikafa atakimbilia kwa nani, Mungu nijaalie hata mwaka huu tu nibebe mimba nyingine ikiwezekana nizae hata mdogo wake au wadogo zake wawili hata wa kulia nao pamoja abaki nao,akipata hata shida awe na ndugu zake , mimi mwenyewe nikiwa na matatizo namlilia kaka yangu napiga simu nalia kweli au kama akiwa karibu nae namlilia mno ananibembeleza na kunifariji ananiambia mimi kaka yako nipo usilie,natamani iwe kwa mwanangu sijakata tamaa naamini ntapata tu ,maana mi nikifikiria akibaki mwenyewe naumia kweli maana najua hapa kwenye kifo hakuna kuchenga ,najua siku moja nami nitakufa japo naipinga sana hii roho lakin Mungu ndio mwenye kujua.

Na mnavyojua mkizaliwa tumbo moja kwa mama nyie ndio ndugu kabisa, sitaki kumuacha mwenyewe najua uzazi wangu wa ni shida sana sijui kama nitabeba mimba nyingine tena labda itatokea bahati nitabeba tena mpaka sasa alitakiwa hata wawe wawili tu ,ila malengo yangu kama siku nikibeba mimba ntazaa haraka wawili,malengo yangu ni kuwa na watoto watatu tu.

Mpaka mama yangu aliniambia siku moja hivi mwanangu utazaa kweli tena mbona hata sioni dalili ,japo nashukuru hata kwa huyu mmoja maana kuna wengine hawana hata huyu mimi nilienae, kwanin wengine kidogo tu wanazaa kama kuku anavyototoa na kwanini wengine ukishazaa ka moja tu ndio basi tena nna ndugu zangu kama watano hawajazaa na umri umeenda sidhan kama watazaa,nna mama yangu mkubwa nae ana mtoto mmoja tu hakuzaaga tena mpaka leo ana wajukuu tu

Najiulizaga ningetoa hii mimba ingekuwaje?ndio maana hata aniite single mother huwa siumii kabisa na sijali naonaga mnavyotunanga lakin wengine hatukutaka kuchoropoa mimba

Nashukuru mpenzi wangu G kuniambia hata nisipozaa ni sawa tu ananipenda nilivyo na hatoniacha kisa kuzaa. mwaka huu nitajaribu tena nione kama itaingia,ikiingia tu nazaa hata watatu haraka haraka
Mwanangu huwa ananiambia "mama nizalie mdogo wangu na mimi "yaan ananichoma ka moyoo akisema vile

Sawa basi hata nikiwa na haka ka moja tu niwepo tu kama mama yake Hamisa Mobeto,alimzaa hamisa peke yake tu lakin kamlea mpaka kapata wajukuu Mungu tuhurumie basi

Vifo vinaumiza sana hasa za vijana wadogo ambao ndio tegemeo la taifa ,Mola mkuzie huyo mtoto alieachwa na Masogange ampe ufariji nayahisi maumivu yake makali sana huyu mtoto ,Mungu angejuaga asingeweka vifo sijui alifikiria nini jamani anatuumiza sana tunapotelewa na watu wetu tunaowapenda .basi bana leo siku yangu mbaya kweli jamani ,kuna hii nyimbo huniliza sana ya Ambwene -Misuli ya imani yaan unafikiria wapendwa wako wote waliofariki
UPUMZIKE KWA AMANI AGNESS MASOGANGE
 
Siogopi kufa!
Naogopa kuzikwa na kubaki pekee angu kaburin. Pia naumia kijana unaondoka hata 2% ya malengo yako hayajatimia...
Ila cha msingi ni UNAKUFAJE? sio unakufa ajili ya kulewa sana,umechomwa moto,Umetembea na mke wa mtu wakakupasua.
 
Yaani upo kama Mimi binamu hua nawaza wanangu Nikifa Leo Hii baba yao atawajali kweli?naumia inafika mda namuomba Mungu ikitokea nimekufa Leo basi nife na wanangu siku moja najua watakavyoteseka siamini ndugu hata mmoja
 
Kwa imani yetu waislam tunaamini kwamba tukio la mwisho ndilo utakalofufuliwa nalo.
Kufa kwenye kifua cha zinaa uone balaa lake.
 
Yaani upo kama Mimi binamu hua nawaza wanangu Nikifa Leo Hii baba yao atawajali kweli?naumia inafika mda namuomba Mungu ikitokea nimekufa Leo basi nife na wanangu siku moja najua watakavyoteseka siamini ndugu hata mmoja
Yaan bora ufe washakua wakubwa kabisa wanaweza kujiongoza,watoto wakiwa wadogo yaan acha tu,ndugu unawajua unawasikiaa mim tunakutanaga msibani na kwenye harusi tu
 
Unapenda ukiondoka uache watoto wako kadhaa wakiwa wanakulilia, penda pia ukiwaacha waseme tumeondokewa na mzazi wetu mmoja na tumebakiwa na mmoja(Baba/mama) huyu hapa. Sio mtoto anamjua Mama/Baba tu ilihali hamjui mzazi mwingine.
 
Unapenda ukiondoka uache watoto wako kadhaa wakiwa wanakulilia, penda pia ukiwaacha waseme tumeondokewa na mzazi wetu mmoja na tumebakiwa na mmoja(Baba/mama) huyu hapa. Sio mtoto anamjua Mama/Baba tu ilihali hamjui mzazi mwingine.
Kulia ni lazima,ila tu wabaki wanafarijiana wao kwa wao sio abaki mmoja tu atakuwa mpweke
wababa wakishaoa wanawake wengine mnajali sasa
 
Jitafakari Ukifa Muda huu umetanguliza nini Kwa Mola wako Kwa maana ya matendo Mema?

Mtoto wako atakuwa tu Mbona Hata Mvua inyeshe Mfululizo wiki mbili huoni kuna Ndege kadondoka nankufa Kwa njaa japo hawatoki kwenye Matundu Yao nyakati za Mvua
 
Jitafakari Ukifa Muda huu umetanguliza nini Kwa Mola wako Kwa maana ya matendo Mema?

Mtoto wako atakuwa tu Mbona Hata Mvua inyeshe Mfululizo wiki mbili huoni kuna Ndege kadondoka nankufa Kwa njaa japo hawatoki kwenye Matundu Yao nyakati za Mvua
We wasema kaka
 
Napenda siku nikifa mwili wangu usizikwe upelekwe hata Mbugani huko wale Tai (napenda nikifa wasitokee watu kwenda kuzuru kaburi langu).
 
Back
Top Bottom