Nanukuu: Mgao wa umeme ni historia

Nanukuu: Mgao wa umeme ni historia

saronga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2008
Posts
909
Reaction score
218
Nchi kuingia gizani
• TANESCO yadaiwa kuendeshwa kisiasa

na Mwandishi wetu

NCHI iko hatarini kuingia gizani wakati wowote kutokana na hali ya uzalishaji umeme kuwa tete katika Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO), Tanzania Daima imedokezwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani, hali ya shirika kifedha ni mbaya licha ya serikali kukwepa kukiri uwepo wa mgawo ikihofia kubanwa kwa ahadi yake kuwa mgawo utakuwa historia.

Julai 28 mwaka jana, wakati wa kuhitimisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa wizara hiyo, Prof. Sospeter Muhongo, na Naibu wake, George Simbachawene, walilihakikishia Bunge kuwa mgawo wa umeme ungelikuwa historia.

Lakini kwa takriban wiki nzima sasa, umeme umekuwa ukikatika hovyo kwa muda mrefu katika maeneo mengi nchini huku TANESCO ikitoa sababu za kawaida kuwa hali hiyo inatokana na matengenezo madogo kwenye nguzo.

TANESCO linadaiwa kuendeshwa kwa hasara kila siku na hivyo kuwa na deni kubwa ambapo sasa mashirika yanayoliuzia umeme yanatishia kusitisha kuendelea kutoa huduma hiyo.

Mathalan Songas imeshatishia kusitisha huduma hiyo baada ya deni lake kufikia zaidi ya sh bilioni 80 zinazopaswa kulipwa na TANESCO.

Tanzania Daima imedokezwa kuwa kwa sasa TANESCO inaendeshwa zaidi kisiasa badala ya ufanisi wa kuliwezesha kujikwamua na kujiendesha ili kuiondolea serikali lawama kwa wananchi.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa TANESCO katika kujinasua isifilisike iliiangukia Mamlaka ya Nishati na Maji (Ewura) kuomba iruhusiwe kupandisha bei ya umeme ili liweze kujiendesha na kunusuru nchi isiingie gizani.

Hata hivyo, kwa maslahi ya wakubwa kisiasa inaelezwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini iligundua kuwa suala hilo lisingeiacha serikali salama kutokana na ahadi yake bungeni kuwa mgawo wa umeme ungelikuwa historia.

Hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, aliandika barua kuiomba Ewura isikubali ombi la kupandisha bei ya umeme na kuiasa TANESCO kuondoa barua hiyo, na kikao cha bodi ya Ewura cha Januari 24 mwaka huu kilikubali kuiondoa.

Baada ya Ewura kukubali ombi la wizara kutokukubali ombi la TANESCO, Maswi ananukuliwa katika waraka mmoja akimshukuru Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu.

Waraka huo ulisomeka: "Naomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa uungwana wako na kuamua kazi kwa kulinda heshima ya serikali yetu. Heshima haina duka. Nakushukuru sana na naomba tuendelee kuisaidia serikali yetu pamoja na matatizo yaliyo mbele yetu. Kwa aina hii ya kushirikiana tutafika tu wala haina gogoro."

Chanzo chetu kinasema kuwa baada ya kutopandisha bei ya umeme, serikali kupitia Maswi iliwasiliana na Benki ya Dunia ili iweze kupatiwa mkopo kusaidia shughuli za uendeshaji wa TANESCO kwa ruzuku.

Inaelezwa kuwa benki hiyo ilipokea barua lakini ilikataa kutoa mkopo huo kwa masharti kwanza ya kujua mapato na matumizi ya TANESCO kwa mwezi, kiwango cha umeme unaogawiwa, makusanyo halisi na mtiririko wa fedha.

Kupitia mawasiliano kati ya Maswi na Jacques Morriset, mchumi mkuu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Mashariki, mkakati huo haukufanikiwa nandiyo maana shirika hilo bado linadaiwa.

Kwa sasa serikali inahaha kutafuta fedha kwa njia zozote mahali popote ili kujinusuru na hali ya ahadi yake kuwa mgawo utakuwa historia.

Muhongo na Simbachawene walilieleza Bunge kwamba waligundua kuwa mgawo uliokuwepo kipindi cha nyuma ulikuwa biashara ya watendaji wa TANESCO, waliokuwa wakitumia mwanya huo ili kujineemesha kupitia ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo.

Wataalamu wa masuala ya nishati wanasema kuwa ili mgawo wa umeme utoweke, sh bilioni 42 zitapaswa kutumika kila mwezi kwa ajili ya kuyalipa makampuni yanayoiuzia TANESCO umeme.

Kwa muda mrefu sasa TANESCO imeelezwa kuwa hoi kifedha licha ya kuwa na makusanyo makubwa lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia mikononi mwa mafisadi na hivyo shirika kubakia tegemezi kwa serikali.

Kwa mujibu wa takwimu za Waziri Muhongo, alizozitoa bungeni wakati akihitimisha hoja ya hotuba ya bajeti kwa mwaka 2012/2013, TANESCO inakusanya mapato kati ya sh bilioni 60 mpaka 70 kwa mwezi.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, licha ya matumizi ya shirika hilo kuwa sh bilioni 11 kwa mwezi, waziri alishindwa kufafanua ni wapi zinakwenda sh takriban bilioni 40 zinazosalia.

Mara kadhaa Muhongo, naibu wake na TANESCO wamenukuliwa wakikanusha kuwa hakuna mgawo wowote wa umeme kwa sababu shirika limejipanga kutafuta vyanzo vingine vya kuzalisha umeme wa uhakika.

Chanzo chetu kimedokeza kuwa katika kila sh 100 ambazo TANESCO inakusanya, sh 86 zinakwenda kulipa madeni ya mikataba iliyosainiwa kifisadi ya Aggreko, Symbion, Songas na IPTL.

Mpaka sasa Symbion inalipwa sh milioni 152 kila siku kama gharama za uendeshaji wakati IPTL inalipwa sh bilioni tatu kila mwezi na Songas sh bilioni 4.5.

"Agrreko wanaiuzia TANESCO umeme kwa senti dola 42 kwa unit moja halafu TANESCO inauza umeme huo kwa senti dola 11 kwa unit moja," kilisema chanzo chetu.

Serikali ilikataa kununua mitambo ya Dowans wakati huo ikiuzwa kwa dola milioni 59 kwa madai kuwa sheria ya manunuzi ya umma inakataza.

Lakini mitambo hiyohiyo ilinunuliwa baadaye na Symbion kwa dola milioni 159 na sasa kampuni hiyo inazalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

SOURCE: TANZANIA DAIMA 1st March 2013

NB: Wanajamvi, kwa mtaji huu kweli tutafika au tutaishia kuwasingizia watu wa Mtwara kuwa ndo wanasababisha ukosekana kwa umeme? Ukombozi wa kweli wa nchi unatakiwa upatikane ili tuondokane na madudu haya. Otherwise siasa katika mambo ambayo yapo kitaalamu zaidi zitatumaliza.
 
Mimi mwanzoni alipoingia ndugu yangu Prof. Dr. Muhongo nilijua mgawo wa umeme umekuwa historia. Alikuja na ahadi nyingi kweli kwamba mgawo hautakuwepo. Sasa kumbe afadhali wakati wa enzi za Ngeleja tulikuwa tukitangaziwa kuwa kutakuwa na mgawo japo tukajiandaa kwa kuweka mafuta kwenye vibatali ila kwa sasa wengine tuna mgawo wiki ya pili sasa lakini mambo yanapigwa kimya kimya!

Tulianza kuona umeme unakatika mara kwa mara na kwa muda mrefu, wenye akili tukajua gawo hilooo lakini tukanyamaza kimya tukisubiri tamko la kisiasa. Hali si hali bali muhali.
 
hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania, no challenges kwa viongozi!! hata wakisema uwongo watu oyeeeee.....baada ya mwezi wakija na uwongo mwingine watu oyeeee......na wale wanaojua kuwa ni owongo wao wanakaa kimya as if there not part of the society - taifa la wananchi kama hawa ni rahisi mno kuliongoza.

niliangalia mdahalo wa Kenya, nikajua those guys wako serious - they know what they want na sidhani ukidanganya mara mbili you have any chance to be respected. sisi ndugu zangu tumo ndani ya gari la mkaa na mbaya ziadi tumefunikwa na turubai jeusi.

Leo kuna mgawo, who cares!!! wenye vijicenti vyao wamewasha vile vi Tyger vyao basi mtaani makelele matupu.sisi ambao hatuna mijasho kibao na maji hakuna. haya ni maisha kweli?
 
We acha tu ndugu yangu, sijui tope hili kichwani litatutoka lini. Viongozi kama hawa tulitakiwa tuwe tumeshakata shingo zao siku mingi sana. Wanatia uchungu sana hawa waongo.Kuna siku inakuja ambayo hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe.
 
Sospeter muhongo ni mwongo kweli yale yale kama ya ngeleja!!!!!!!
 
tukisema tatizo la uongozi wa nchi hii ni mfumo wengine wanabisha sasa angalia; mlipiga kelele mingi juu ya umeme na matamko ya uongo ya mh. ngereja- Mkamuweka pembeni, huyu ni mwanasiasa.

Sasa mkaona badala ya mwanasiasa ngoja tujaribu kumweka mtaaluma kabisa aliyesomea fani hiyo nje ndani; sasa naye mnasema kawaongopea; mi siamini kama prof. ni muongo bali mfumo ndiyo unaotuongopea, hata mimi ningekuwa waziri leo ningewaambia hivyo hivyo "wananchi tulieni mgawa hakuna kama tulivyokwisha kuwaleza mwanzo, mkiona umeme unakatika katika basi ni matengenezo ya kawaida tu"
 
Aonyeshe hizo nguzo zinarekebishwa wapi?
 
Mimi mwanzoni alipoingia ndugu yangu Prof. Dr. Muhongo nilijua mgawo wa umeme umekuwa historia. Alikuja na ahadi nyingi kweli kwamba mgawo hautakuwepo. Sasa kumbe afadhali wakati wa enzi za Ngeleja tulikuwa tukitangaziwa kuwa kutakuwa na mgawo japo tukajiandaa kwa kuweka mafuta kwenye vibatali ila kwa sasa wengine tuna mgawo wiki ya pili sasa lakini mambo yanapigwa kimya kimya!

Tulianza kuona umeme unakatika mara kwa mara na kwa muda mrefu, wenye akili tukajua gawo hilooo lakini tukanyamaza kimya tukisubiri tamko la kisiasa. Hali si hali bali muhali.

Ndugu yangu Kimbunga wenye akili waliyaona haya mapema na wakasema lakini wakaitwa wazandiki, waongo, wazushi na majina yote mabaya unayoweza kufikiria ikiwemo 'wanapiga siasa hao'. Huwezi kutatua tatizo kwa kusema 'na iwe hivyo' ikatokea kuwa hivyo bila kutatua kiini cha tatizo. Ni Mungu tu aliyeumba kwa kutamka (kwa mujibu wa Vitabu Vitakatifu). Bahati mbaya lawama za rahisi sana zinazokubalika bila juhudi kubwa ni kuwasukumia watendaji na wataalamu.

Serkali baada ya kuona single ya mgawo imechuja na haiuziki masikioni mwa watu wakatengeneza single ingine inaitwa uvhakavu wa miundombinu. Hii nayo inachuja haraka haraka na kwa hiyo tayari kuna juhudi za kutengeneza ingine na inawezekana kutoka wakati wa kikao kijacho cha Bunge. Inawezekana ikawa 'remix' ya mgawo!
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu
 
nice 2...... Zitto......????

Mi kichwa kinazunguka ngoja nipumzike kwanza!!!
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu

mmh mwandiko kama wa Zitto....asante kwa ushauri nice 2
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu

Nimesikia Leo asubuhi Tanesco wakishauriwa na watabiri wa Hali ya hewa kutafuta njia ingine ya kuzalisha umeme kwani mvua haitakuwa ya kutosha kujaza mabwawa ya kuzalisha umeme! Hoja zinaanza kujengwa kutoka kila sehemu ikiwemo kwa hawa watabiri ambao Mara nyingi hawapatii katika tabiri zao!
 
Tanzania yangu kana tambara bovu,muhongo yuko zake Uk anakutana na wanaotafuta na kuchimba gasi.Mgae eti hakuna lakini kila siku umeme unakatika zaidi ya masaa nane
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu

Nimeipenda hiyo mkuu!!Lakini hakunaga giza jema yaani ni matatizo tu kwakwenda mbele.Leo Sinza wamekata umeme asubuhi wakarudisha saa moja usiku.
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu

Sasa si uje kwa ID yako tu .....Hebu njoo tujadiliane kwa mapana mkuu?
 
Kwa hali ya mgao wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa, nimekumbuka ushabiki uliotokea siku si nyingi za kumshangilia Mhe. Muhongo aliposema kwamba "mgao sasa basi", na tukamuita Zitto kuwa mkurupukaji, hajui afanyalo na majina yote mabaya alipodhubutu kusema kwamba Prof anatudanganya na ku criticize tenda waliyopewa Puma.
Nawatakia giza jema
Somo: tujifunze kuukubali ukweli hata kama hatuufurahii maskioni mwetu

Mie nimekumbuka pia lile alilosema JK kapoteza uwezo wa kuongoza nchi sasa.
 
Back
Top Bottom