ChingaMzalendo
Senior Member
- Nov 9, 2008
- 192
- 3
ina maana unataka kuunda chama ambacho watu hawatoruhusiwa kuwa na dini au makabila fulani?
ina maana unataka kuunda chama ambacho watu hawatoruhusiwa kuwa na dini au makabila fulani?
Mkuuniliweka majina hayo kwa mtego, na wewe hauja unasa ila tu umenisaidia kuforce my point home na point yangu ilikua hiviiiiiiii
Je John Mashaka, Mwanakijiji na Dr Shayo wamefanya nini kwa taifa mpaka wawe na vigezo ambavyo watu wanawapitisha kuwa wanafaa kuwa viongozi? au ni uwezo wao wa kuandika? kama ni uwezo wa kuandika wapo watu wengi tu? nilichokua nataka watu waelewe ni kwamba uongozi ni zaidi ya kujua kuchambua mambo..mfano prof lipumba hamna mtu anaemfikia katika wanaogombeaga u prez da kwa kuchambua mambo, ila i am not sure kama ni kiongozi mzuri...me naamini kiongozi mzuri ni yiule ambae anaweza kuwa na mipango mizuri kwenye afya, elim. azingira, technology, utawala bora na chamuhim zaidi kuwa na team thabiti itakayo waezesha kuingia madarakani na si tu kuingia madarakani bali pia kuongoza watu milioni 40...mfano tena vyama vyetu vya upinzani vinakosa team kamili yaani watu waliokamilika zaidi kukijenga na kujenga uwaminifu kwenye chama ambao wanafaa kuongoza nchi...tubahitaji mlolongo wa vitu vingi na si nakuwa na uwezo tu wakuandika na kuchambua mabo...ni sawa na usemi kuwa mchezaji soka bora atakua kocha bora, ambapo saa nyingine siyo
ahsanteeeee
Nchi sio uwezo wa kuandika viji articles tuuu, Kuna mambo mengi katka uongozi, so sidhani kama wanasifa hao watu wako wote..mpaka tungejua angalau historia yao ya uongozi na maendeleo yao na si kujiandikia vijiarticle wapewe nchi
Wadau
Hii nchi inahitaji mapinduzi ya Kijeshi................atokee mtu aipindua kwa muda wa 2 -3yrs ili watu tuwe na adabu. Baada ya hapo hairudishe kwenye utawala wa raia
Bila hivyo kila kitu ni Hovyo Hovyo hovyo
Unadhani nchi inaendeshwa kupitia blogu!Ndugu Wadau, Nadhani muda unavyokwenda, nchi yetu inazidi kudidimia katika wimbi la ufukara. Nchi imekwisha na hali inazidi kutisha, hasa tukizingatia hali ya kisiasa na ya kiuchumi.
Swala zima hapa ni uongozi mzima wa Tanzania kuanzia chini mpaka juu kuna matatizo kwahiyo hata john mashaka akipewe nchi au Shayo hawataweza lolote kwani Tanzania inatakiwa kama Gari ni kushusha engine yote na kuanza kuweka spare mpya "Overhaul"
Pamoja na katiba yetu ambayo bado inalinda viongozi wapuuzi na wanaofoji vyeti pamoja na mafisadi. Tanzania bila umasikini inawezekana kama mafisadi tutawamaliza
Ndugu Wadau, Nadhani muda unavyokwenda, nchi yetu inazidi kudidimia katika wimbi la ufukara. Nchi imekwisha na hali inazidi kutisha, hasa tukizingatia hali ya kisiasa na ya kiuchumi.
kwangu mimi katika watu wa kuogopwa, nadhani mashaka ni moja ya vijana ambao karibuni wataogopeka na kuheshimika siyo tu tanzania bali duniani kote
Mkuu unajua unachokisema, katiba si kitu cha mchezo na si assignment za chuo kikuu na wala si maandishi ya articles kwenye JF hauwezi andika katiba siku moja....waambie hao akina Mwanakijiji waende kutangaza sera zao kwa wananchi na sio kwenye Blogs mkuu..maana naona mnataka kukimbia ukweli kwa kwa sasa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza nchi mpaka tujue sera. sio unashangilia kila kitu, jua kuchuja...
Dr Shayo huyu ninaye mjua mimi hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.
Ndugu Wadau, Nadhani muda unavyokwenda, nchi yetu inazidi kudidimia katika wimbi la ufukara. Nchi imekwisha na hali inazidi kutisha, hasa tukizingatia hali ya kisiasa na ya kiuchumi.
bado manataka Dr Shayo apewe nchi?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120064-dr-shayo-the-plagiarist.html
- Mkuu with all due respect, angalau hao wanajiweka wazi mbele ya taifa na mawazo yao, kuliko wengine ambao kazi ni kuponda tu huku wakiwa hawana hoja hata za kimombo.
- No matter what the case, misimamo yao iko wazi kwamba wana nia njema na taifa letu, na wanazo hoja nzito za kukosoa serikali dhaifu tuliyonayo sasa, na huwezi sema eti Tanzania we are better off na viongozi kama Kusila na Guninita, just because wanasema hoja zao kwa kiswahili kuliko Mashaka na Shayo kwa sababu hoja zao ni za kiingereza, wakuu sometimes tulionee huruma sana hili taifa.
- Ninaamini kwamba Mwanakijiji, Mashaka na Shayo wakipewa nafasi za uongozi wa juu wa taifa hili, watatusaidia better than kina Kusila, Guninita, na kina Kingunge.
Ahsante.
William.