Nani zaidi: Musabe Schools au Wizara ya Elimu?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,139
2,000
Shule zinaenda kufunguliwa tarehe 29 Juni, 2020 kama ilivyotangazwa na Mh Raisi JPM, wizara ya elimu ilitoa maelekezo ya ulipaji wa ada hasa shule za binafsi ( Private Schools) kuwa ada isipandishwe wala kipindi ambacho watoto hawakuwa shule wazazi wasilipishwe. Shule ya MUSABE iliyoko mkoani Mwanza katika wilaya ya Nyamagana imepandisha ada zaidi hata ya ile kulipia ada ya kipindi watoto walikuwa nyumbani!

Ada ya shule hiyo kwa mwaka ni 2,200,000( Day Schoolars) kwa mwaka na malipo yake ni mara nne kwa mwaka kwa maana ya 550,000 mara nne na kuna mahitaji mengine machache kama maziwa,stationeries nk hulipwa Jan na July kwa ongezelo kama la 193,000 na hivyo kupelekea kulipa 743,000 kwa miezi ya Jan na July.

Wakati shule zinafungwa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa covid19 watoto walipewa barua za kufunga ikiwamo na ada inayotakiwa kulipwa ya 550,000 kama kawaida. Sasa maajabu wazazi wametumiwa meseji wanatakiwa kulipa 850,000 kwa mwezi Jun na 843,000 Sept!

Hivyo ukijumlisha inakuwa 1,693,000 hii ni ada ya kipindi kilichobaki wakati huo ikumbukwe mzazi keshalipa 550,000 ukijumlisha hapo unapata 2 ,243,000! Hapo kuna quarter iliyotakiwa kulipiwa 550,000 watoto walikuwa nyumbani,tifanye wangekuwa shuleni nayo tuijumlishe maanake ada imekuwa 2,793,000!

Hapo ni bila ya wazazi kupewa notisi ya kupanda kwa ada! Mhasibu akipigiwa simu anatoa namba ya mkuu wa shule ndo aulizwe na mkuu huyu anajibu kwa mkato haswaa kuwa serikali imeongeza muda wa masomo kwa hiyo hakuma jinsi mzazi atakwepa kulipia ongezeko!

Na kila siku wizara inatangaza kuwa ada isiongezeke hata shilingi! Sasa hawa MUSABE wao wanafuata muingozo gani kama shule zingine hadi zimewatumia wazazi waraka toka wizara husika unaosema ada zisipandishwe,hiki kiburi cha MUSABE kupandisha ada kinatoka wapi? Nani yuko nyuma ya shule hii? Wazazi wanahaha kupiga simu na kulikuwa na magroup ya watsup ya wazazi yaliyofunguliwa na shule yote yamewekewa restriction only admin allowed to post!

Yote hii ni kuwabana wazazi wasiwe na umoja wa kuhoji kwa pamoja.

Hebu waziri husika wasiliana na MUSABE walkuambie kwa nini wanapingana na maelekezo yako au basi utoke tena ufute kauli yako ya ada kutopandishwa kwa musa huu.

Nawasilisha.
 

mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,432
2,000
Kama kwenye form yao walisema
2,200,000 kwa mwaka basi unapaswa kulipa hiyo yote. Corona sio kisingizio.
 

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,139
2,000
Kama kwenye form yao walisema
2,200,000 kwa mwaka basi unapaswa kulipa hiyo yote. Corona sio kisingizio.
Huelewi na hutakaa uelewe,unataka kujiambia Wizara ni wajinga na unafikiri hawakuliona la Covid19? Walipotoa mwongozo wa ulipaji ada hawakujua kama form ziliandikwa kwa mwaka?
Nonsense
 

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,016
2,000
Mkuu poleni sana kwa kweli inasikitisha.
Wanapandidha Ada bila mawasiliano na wazazi hapo siyo bure Kuna mkono wa mkubwa ndani ya shule.
 

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,016
2,000
Kalipe ada wewe siku walizosoma zinafidiwa acha kelele kama huna pesa wapeleke kayumba
Mkuu kwani wazazi wamegoma kulipa Ada?
Wanagoma ongezeko hilo la katikati ya mhula kumbuka mhula wa kwanza bado
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,994
2,000
Hiyo international school msabe si ndo naskia miradi ya wakubwa wetu wa nchi

Poleni sana wenye watoto uko, kazi mnayo
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,603
2,000
Hyo ada mnayotoa mnaipigia hesabu kwenye kufundishwa tuu,...? Kuna variable cost nying Tu shule iliendelea ku-incur wakat watoto wapo huko home , shule ili ndelea kuwalipa walimu kpind watoto hawapo , kumaintain Hali ya usafi , security na hata kodi waliendelea kulipa kama kawa, na vingine ving , hyo gharama ilikuwa inatoka wap.... Watz mnapenda kulia Lia Sana , kama ni punguzo Kwa shule kama hyo ni nothing , ...... Ukiona unaumia sana bas organize wazazi kadhaa mu-request kikao na bodi ya shule myajenge ....
 

Pennstatepro

Senior Member
Nov 22, 2019
184
250
Huelewi na hutakaa uelewe,unataka kujiambia Wizara ni wajinga na unafikiri hawakuliona la Covid19? Walipotoa mwongozo wa ulipaji ada hawakujua kama form ziliandikwa kwa mwaka?
Nonsense
Mkuu,wewe ndo huelewi mambo, ADA haibadiliki mkuu, kama ulipaswa kulipa 2M kwa mwaka ni hyo utalipa! No increasement or decreasement
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom