"Nani yupo juu ya sheria ???

Unbounced

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
345
430
"Habari za wikendi wakuu,
Natumai mko njema, baadhi mnaosumbuliwa na afya niwape pole na kuwatakia kheri mpone haraka.

Moja Kwa moja niende kweye kile kinachonifanya niandike uzi huu Kwa uchungu kuzidi ule wa mjamzito aliekatika maumivu ya leba,

Miezi takribani isiyopungua saba kuna wafanyakazi wa idara mbalimbali kutokashirika la elimu kibaha walisimamishwa kazi (Kwa kupewa barua za kusitishiwa mishahara huku wakitakiwa kukabidhi ofisi na kutoonekana tena kazini).

Hii ilitokana na kauli ya mkuu wa nchi kwamba wale walio na elimu chini ya kidato cha nne hawatakiwi tena kazini hususani Kwa wale walioajiriwa zaidi ya mwaka 2014.

Shirika la elimu kibaha liliandika barua kuomba wizara husika kupata kibali cha kuajiri baadhi ya watu wenye kuangalia mifugo na usalama wengi wao wakiwa wamehitimu mafunzo ya ulinzi ya mgambo
Kwa maandishi shirika lilikubaliwa kuajiri hao darasa la saba Kwa mujibu wa sheria na kuzingati taratibu zote za kisheria na wameshafanya kazi Kwa miaka kadhaa.

Baada ya tamko la mkuu wamewageuka hawa watu sasà miezi inaenda bila kupewa haki yao wala tamko lolote. Kawaida kama umeajiriwa kisheria Basi unazo haki za kulipwa haki zako kinyume na hawa ndugu zetu walichofanyiwa.

Je, tamko la mkuu ni zaidi kuliko sheria ya kazi na haki za wafanyakazi????
Je, nini kinasababisha hawa watu walioajiriwa kisheria leo hii kunyanyasika na kutopewa haki zao licha ya kulitumikia taifa Kwa miaka kadhaa???

Kama Kwa mujibu wa sheria hawakutakiwa kuajiriwa kwanini kilitoka kibali toka wizarani kuajiriwa watu hawa ??

Kama Kwa mujibu wa sheria waliajiriwa kwanini Kwa mujibu wa sheria wasipewe haki zao???
Watalaamu wa sheria uwanja ni wenu kusema neno .
 
Komeo la magogoni na yule Tasa WA masifuri form four wapo juu ya sheria
 
Back
Top Bottom