Nani wapo nyuma ya leseni vamizi za madini Jimbo la Mbogwe baada ya Hayati Magufuli kufariki? Je, Biteko umenunulika au ni shinikizo juu yako?

Hivi huyo baba mmiliki wa visheli uchwara vya mafuta ndio alisema bungeni ubunge hauna hela
 
Duh, yaani mhhh
Pamoja na Juhudi kubwa zilizofikiwa na Serikali ktk Sekta ya Madini mimi naomba nikiri kuwa Bado kuna changamoto kubwa mno,
Bahati nzuri nimezaliwa katika familia ya Wachimbaji wa madini ya Dhahabu
Nimekulia ktk familia hiyo
Mungu sio Athmani Mwaka 2019 Shamba la Baba yangu Mzazi liligundulika kuwa na Madini ya Dhahabu, ikabidi niende kusimamia,ukweli niliyaona mengi mno.
Wachimbaji wadogo bado wananyanyasika mno
Wenye mashamba ambayo Dhahabu iligundulika bado wananyanyasika mno.
Ktk Sehemu ambazo naweza kukiri kuwa hata Mh. Hayati Magufuli hakuziweza ni Sekta ya Madini japo nakiri kuwa angalau kwa 60% ameleta mapinduzi makubwa ikiwemo kufunguliwa kwa masoko ya Madini.

Naomba kusema yafuatayo:
1.Mfumo wa upatikanaji Leseni bado unatatizo kubwa sana, kuna hatari kubwa huko tuendako kama hatua kubwa hazitachukulia.
2.Wachimbaji wa awali wanaogundua madini hawatambuliwi popote/mfumo wa kuwatambua sio rafiki
Mfano mzee wngu alianza kutafiti dhahabu toka mwaka 2011 akishirikiana na mzee mwenzake, mmoja akipiga nyundo mwingine akipiga boya (Waliowahi kufika machimboni watakuwa wamenielewa zaidi) ilipofika mwaka 2019 Duara yao ikaupata mwamba wa Dhahabu (hapa unielewe sio kwamba miaka yote walikuwa wanachimba Duara moja hapana isipokuwa walikuwa wakichimba na kufikia mita fulani wanaliacha shimo na kuanza jingine)

**Basi kipindi Duara inafika kwnye Mwamba mzee alikuwa anaumwa kifua akikohoa anatema damu, hii ilisababishwa na kazi za Kupiga nyundo/kupiga boya
Akawa ametibiwa na kupona
Yule mwenzake alikuja kugundulika kuwa na Ugonjwa wa kifua kikuu, amemaliza kutumia dawa siku chache zilizopita
Baada ya Duara yao kushika Mwamba watu walikuja maelfu kuanzisha Maduara na kuwekeza,
Jumla ya ajira za watu wasiopungua 1,000 zilipatikana
Serikali ilikusanya mrabaha kupitia mauzo ya mawe
Lakini pia ilikusanya mrabaha kupitia mauzo ya dhahabu kwnye majiko ya Dhahabu
Serikali ilikusanya mapato kupitia halimashauri pamoja na ofisi za madini kutoka kwa watu walioanzisha Plant mpya jirani na eneo la mgodi
Watu walipata ajira kupitia hizo plant kuanzia walinzi, wapishi,wakemia,vibarua wakuopoa na kupakia,maoporeta wa plant,wasimamizi wa plant,wenye magari yakusomba vifusi,madureva,
Wauza kemikali walipata soko na serikali kukusanya mapato yake,
Upande wa Elution napo ni hivyo hivyo
Bodaboda, mama lishe n. K
Mnyonyoro wa ajira na faida kwa serikali ni mkubwa sana.
Kuna haja yakuwaangalia kwa jicho pana wazee hawa waliovuja jasho kufanya utafiti ambao umeleta matokeo makubwa yanaweza kuendelea kwa miaka kati ya 5-10 au zaidi
Mwanzo mwa mwaka huu Serikali ilitoa Reseni ktk eneo husika
Cha ajabu Leseni ilikuja kutolewa kwa watu ambao ktk mgodi mzima hawana hata shimo moja, wazee hawa hawakupata Leseni na hata wachimbaji waliowekeza hakuna hata mmoja aliyepata Leseni
Kikundi kimoja kinapata vitalu zaidi ya vitano huku waanzilishi wakiambulia sifuli.
Baada yakufanya utafiti niligundua kuwa kuna vikundi vilipandikizwa pia vikapata Leseni vitalu kadhaa kisha vikalipwa pesa nakuwakabidhi wahusika.
Tumeshalalamika sehemu mbalimbali toka mwaka 2019 bila mafanikio
Tulishafika kwa waziri, kwa mwenyekiti wa tume ya madini (sasa ni naibu Waziri)
Na hata kwa mwenyekiti mpya tulishafika mkoani Dodoma,
Katibu mkuu wa wizara ya madini wakipindi kile alishawahi kufika pia
Wakati tukiwa tunajiandaa kwenda kumuona mzee Ndo hivyo tena Mwenyezi Mungu akamchukua.
 
Kwani napinga Nini Hadi unibatize kuwa mpinzani? Au kuandika ukweli kuwa hao watu wako wapo kwenye kijiwe chao va upigaji wa Kodi za wananchi imekuuma Sana? Wacha watengeneze scenario za movie Yao na mwisho wa mwezi wanalamba posho na mshahara mnene! Endelea kulipa tozo ili wale na kuvimbiwa! Na bado mtabweka mno humo ndani ya kijiwe chenu japo mpo wenyewe Bado mnatusuana manakozi! Mtauana wallah!
CCM itaendelea kuongoza nchi hii hadi uwe kikongwe. Hatuna chama mbadala wa kuwakabidhi nchi. Hatuwezi kabidhi nchi kwa watu wasoijitambua na ambao malengo yao hayaeleweki
 
Sekta ya madini inahitaji mabadiliko ya viongozi , tumekuwa na viongozi wabinafsi na ambao sio waadilifu.
Naibu waziri wa madini angalau ana uadilifu na weledi.
 
Upinzani gani wa hao wa kubadiki gia angani ? Hahahaa mtasubiri mpaka vikongwe Ikulu mnaiskia na kuipiga picha.
Sasa na wewe unaona mtaongoza mpka mwisho wa dunia?

Kama unajua kwamba mwisho wako upo na utakufa na ccm itaondoka tu. Usijidanganye Kwa sababu akili zenu mnazitegemea vyombo vya dola...
 
Kansa ndio ni nini ? Wewe unataka kujilinganisha na Mbunge Msukuma ? Kweli njaa mbaya sana.
Hiyo kansa Ina wabunge wasanii sana, Anza na msukuma sasa huyu ni jirani yake na wapo mkoa mmoja maana Mbogwe ni moja ya wilaya mpya mkoa wa geita
 
Pamoja na Juhudi kubwa zilizofikiwa na Serikali ktk Sekta ya Madini mimi naomba nikiri kuwa Bado kuna changamoto kubwa mno...
Mkuu Erick Kalemela pole sana kwa yaliyowasibu wazee wako.

Nakupa kongole kwa kuandika na kuyaweka wazi haya mambo.

Ulichoandika ndio ukweli na uhalisia unafanyika kwenye sekta ya madini.

Kuna wakati fulani huko nyuma,niliwahi kuzungumza na kamishina mstaafu wa madini wa miaka ya 1980,alisema tatizo kubwa ni tamaa ya "vigogo".

Viongozi wakubwa huwa wanakuwa na watu wao ambao wanapewa leseni kila migodi mipya inapogunduliwa.
 
....ukisema kilichopo au ukaogopa kusema hakubadilishi ukweli kuwa uongo...ukweli utabaki kuwa ukweli na wakweli watabaki kuwa wakweli.
 
Back
Top Bottom