thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Ni leo bungeni, Bunge likimaliza vikao vyake, kaibuka mbunge wa Jimbo hilo Mheshiwa Maganga akilitaka bunge kujadili kwa dharura yanayoendelea jimboni kwake kuhusu mauaji ya watu sita akiwemo binamu yake , akidai mauaji hayo yalisababishwa na leseni vamizi baada ya hayati Magufuli kufariki.
Nimpongeze Spika kwa kulipa umuhimu suala hilo.
Mbunge huyo kaongea kwa uchungu sana,na kasema mahakama shinyanga anaamini zimenunulika na hata yeye angekuwa ana shida ya pesa angechukua ,kwani alitangaziwa dau,isipokuwa uhai wa waliokufa na binamu yake haulingani na hiyo hongo , hivyo ameikataa.
Pia kaongeza kwa kusema, kuna watu walienda eneo hilo na kujifanya maafisa usalama toka juu na ndio waliofanya uhalifu huo.
Tujiuliuze ,kama ni kweli asemayo mbunge huyo wa Mbogwe, je Waziri Biteko kawasaliti wanyonge dhidi ya wachache wenye pesa kwa kuhofia kupoteza uwaziri wake?, yaani kapiga U turn?
Mambo haya yalishamiri sana awamu ya nne ,lakini awamu ya tano wachimbaji hawa wadogo wadogo walipata utulivu sana .
Mwisho,
Amani ya nchi hii tutaivunja wenyewe kwa mikono yetu kwa tamaa za kujilimbikizia mali pasi kufuata sheria,. kwani hawa wanaodhurumiwa wanakiwango pia cha uvumilivu ,hebu changanya hawa wachimbaji wadogo+wamachinga+Mama lishe+wahitimu wasio na ajira +waliokata tamaa ya maisha ,nini matokeo yake akitokea wa kuliwasha?