Unatafuta best friend wa nini? bila best friend umepungukiwa nini? au unataka wa kuvaa naye sare?
Ushauri wa bure: - ishi vizuri na watu wote, changamka nao, saidiana nao, lia nao USITAFUTE BEST FRIEND. Utajuta mchana kweupeeeeeeee kwa Mungu hakuna nyota!
du! sikujua kumbe hata mimi ni "wa kawaida" tu, lol!to me nilishajisemeaga kwamba sitaki kuumizwa na friends hiivyo nikajifunza kuwa na marafiki wa kawaida tu ambao tunasaidiana katika raha na tabu basi ila yule shoga hadi tuvaliane sare, tuazimane magari nk sina.
Asante kwa ushauri ila nakosa mtu wa kumwambia hw i feel kama rafiki.... kuna vitu cant tell mama.
ofcourse wewe waijua nafasi yako kwangu ni zaid ya rafiki sio??du! sikujua kumbe hata mimi ni "wa kawaida" tu, lol!
vibaya hivyo rafiki
I was just checking, to make sure, lol!ofcourse wewe waijua nafasi yako kwangu ni zaid ya rafiki sio??
wewe na shoga yangu cacico et al ni watu ambao ni zaid ya marafiki, shoga, nk.
nyie ni wakaribu yangu.
Hamna haja ya kujilaumu kwa kutokuwa na "best friend", la muhimu ni kuishi vizuri na kuwa na mawasiliano mazuri na watu wote wanaokuzunguka. Watu wengi hujilazimisha kuwa na best friends ili tu kuweza 'kufit in society', kuonekana wanakwenda na wakati, na kubwa zaidi ni kutojiamini. Kuna vijana wengi wanafanya vitu wasivyovipenda for the sake of maintaining friendship, hii husababisha watu waingie kwenye matumizi ya vilevi, uzinzi, kutoheshimu wazazi, utovu wa maadili, kutopata maendeleo/mafanikio kwenye ajira/masomo/biashara n.k. Kwa mfano mwanafunzi wa chuo anaweza kushawishika aende kujirusha usiku na marafiki zake badala ya kukaa na kujisomea kwani akikataa atauharibu urafiki uliopo.