Nani ni mkweli CCM au CHADEMA

nyambari

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
355
171
Tangu kampeni zianze Igunga kwa ajili ya uchaguzi mdogo kumekuwa na kushutumiana kwa hapa na pale hasa vyama viwili vya CCM na CHADEMA kuhusu vurugu zinazotekea kila kukicha kila mtu akimtuhumu mwenzako kwamba ndo chanzo cha vurugu hizo.

Je ni nani mkweli kati ya hawa ?

(a) CCM
(b) CHADEMA
 
Mbaliche

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
294
61
mkuu wananchi wa igunga ndio watakao jua mkweli na mwongo ninani' ifikapo trh 2oct 2011.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
523
Ukitaka kujua nani mkweli au muongo, angalia matendo ya Polisi katika kushughulikia hizo vurugu. DC aliponyakwa na CDM kwenye anga zao, Polisi walichukua hatua gani? Viongozi wa CDM walidakwa na wameshitakiwa. Rage alipotinga Mkutanoni na bastola,Polisi wamechukua hatua gani?Kiongozi wa CUF alipopigwa na kina Shigela,Polisi wamefanya nini?Balozi wa CCM alipodakwa na shahada na orodha ya wapiga kura,Polisi walifanya nini?
Kama pisto ya Rage ingekuwa ya Lema au Heche wa CDM,reaction ya Polisi ingetoa jibu!
 
STIDE

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
997
350
Ibrah, thanx!! Nadhani majibu yako hayamgharimu yeyote kwenda shule!! "Eee mwenyezi mungu ibariki Tanzania, ilinde CDM".
 
Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
256
Mkuu umekosea kwa bahati mbaya au ulidhani WanaJF wote tupo Igunga na tunashuhudia live yanayotokea? Nadhani hili swali lilipaswa lijibiwe na wale walioko huko Igunga na si sisi wala polisi ambao nao ni mawakala tu wa Magamba
 
nyambari

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
355
171
Babu wa kijiji mimi kuandika thread hii haina maana kwamba nisitoe maoni yangu au ulitaka nipigie CCM huo no matzamo wangu
 
Salas

JF-Expert Member
Feb 15, 2009
382
81
Tarehe 3 mwezi October 2011 watanzania kuvaa nguo nyeus kulaani utendaji wa serikali kama kama unaguswa na mambo yafuatayo basi na wewe vaa na umwambie na mwenzako kama yana muhusu naye avae.
1.ukosefu wa ajira
2.kupanda kwa gharama za maisha
3.huduma mbaya za afya, elimu na maji.
4.ukosefu wa umeme
5. Ufisadi
6.mikataba mibovu
7. Ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu
8.malipo duni ya wafanyakazi wa serikali
9.ufujaji wa mali ya umma kwa watendaji wa serikali kwa safari zisizo na tija.
10. Kuwakumbatia wawekezaji katika kuiba ardhi na rasilimali ya wanyonge

Huu ni ujumbe unao zunguka kwenye Mitandao ya kijamii twitter, facebook na myspace pia sms kwa njia ya simu zimeanza kusambaaa nchi nzima.
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
Hakuna haja ya kuongeza!!!

Ukitaka kujua nani mkweli au muongo, angalia matendo ya Polisi katika kushughulikia hizo vurugu. DC aliponyakwa na CDM kwenye anga zao, Polisi walichukua hatua gani? Viongozi wa CDM walidakwa na wameshitakiwa. Rage alipotinga Mkutanoni na bastola,Polisi wamechukua hatua gani?Kiongozi wa CUF alipopigwa na kina Shigela,Polisi wamefanya nini?Balozi wa CCM alipodakwa na shahada na orodha ya wapiga kura,Polisi walifanya nini?
Kama pisto ya Rage ingekuwa ya Lema au Heche wa CDM,reaction ya Polisi ingetoa jibu!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom