Nani na nani wanafaa/hawafai kuoana?

Nani na nani wanafaa/hawafai kuoana?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,175
Reaction score
48,459
Ndoa ni jambo lilioko kwenye jamii Kwa miaka mingi sana. Wataaalam wa mambo ya jamii husema kuwa ndoa ndiyo taasisi Kongwe zaidi duniani.

Lakini kati ya jamii na jamii Kuna utofauti wa kimtizamo wa kati ya nani na nani wanafaa/hawafai kuoana.

Makabila mengine binamu na binamu huoana, lakini kwa wengine hawaoni.

Kuna makabila watoto wa baba mkubwa na mdogo huoana lakini kwa wengine haiwezekani.

Kwa kufuata kanuni Fulani Fulani ambazo ni za kale Sana, mifumo ya kuoana imetengenezwa kuzuia au kuruhusu watu kuoana na kutooana.

Jee unadhani Kwa mtazamo wako nani unaona wanafaa/kuoana au hafai kuoana na sababu zako ni zipi?

Dada/ kaka wa Kambo wanafaa kuoana?

Mtoto na mzazi wa Kambo wanafaa kuoana?

Kuoana na mtoto wa dada yako inawezekana?

Kuoa shangazi/ mama mdogo ni sawa?

Kuoa bibi au kuolewa na Babu inawezekana?
 
Subiri, wanakuja kujibu hili,
NB: kataa Ndoa hili haliwahusu, na hakuna points za mezani.
😂😂😂😂
 
Suala la nani na nani wanatakiwa kuoana ni very relative na bahati nzuri hata wewe umelizungumzia.

Kila Jamii ina taratibu zake. Sasa kusema hii ni sahihi zaidi kuliko ile ni kujiliwaza kwa nafsi tu, lakini hakuondoi uhalisia na sababu Jamii husika walizojiwekea kwenye jambo hilo.
 
Ndoa ni jambo lilioko kwenye jamii Kwa miaka mingi sana. Wataaalam wa mambo ya jamii husema kuwa ndoa ndiyo taasisi Kongwe zaidi duniani.

Lakini kati ya jamii na jamii Kuna utofauti wa kimtizamo wa kati ya nani na nani wanafaa/hawafai kuoana.

Makabila mengine binamu na binamu huoana, lakini kwa wengine hawaoni.

Kuna makabila watoto wa baba mkubwa na mdogo huoana lakini kwa wengine haiwezekani.

Kwa kufuata kanuni Fulani Fulani ambazo ni za kale Sana, mifumo ya kuoana imetengenezwa kuzuia au kuruhusu watu kuoana na kutooana.

Jee unadhani Kwa mtazamo wako nani unaona wanafaa/kuoana au hafai kuoana na sababu zako ni zipi?

Dada/ kaka wa Kambo wanafaa kuoana?

Mtoto na mzazi wa Kambo wanafaa kuoana?

Kuoana na mtoto wa dada yako inawezekana?

Kuoa shangazi/ mama mdogo ni sawa?

Kuoa bibi au kuolewa na Babu inawezekana?
Wewe mwenyewe unataka kuoana na nani kati ya hao wote uliowataja? Siyo vizuri kusumbua akili za wengine, na wakati shida ni ya kwako. Tuelekeze kwanza ili tukupe ushauri.
 
Back
Top Bottom