Nani mwenye kosa, mwalimu au mwanafunzi?

Nani mwenye kosa, mwalimu au mwanafunzi?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,169
Reaction score
166,142
Mwanafunzi wa shule ya msingi Kakuyu amefukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu wake wa Kiingereza ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa dagaa kwa Kiingereza anaitwaje?

Mwalimu huyo aliposhindwa kujibu swali hilo alihamaki, akamcharaza mtoto huyo
bakora sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali mwilini
mwake na akahitimisha kwa kumwandikia barua ya kumfukuza shule kwa madai ya
utovu wa nidhamu na kutumiwa kama kibaraka wa maadui wa mwalimu huyo.
 
Ni swal gumu pia, kama kibongo bongo yenyewe kuna mikoa hakunaga hata hao dagaa, kujua wanaitwaje ni mtihani pia
 
Kuna dagaa wa aina nyingi kutokana na eneo na walivyo, lakini kwa ujumla wanaitwa "forage"(chakula cha samaki wengine wakubwa), ila kuna
anchovy, herring
menhaden, sardine
shad, sprat(sawa na wale wa maji chumvi, baridi, weupe, wa gold.... Etc)
 
Ulikuwa uchochezi tu kwa mujibu wa intelijensia ya ualimu
 
Mleta uzi usiwadhalilishe watu waliokuondoa ujinga,utalaanika
 
Back
Top Bottom