Nani mwenye kaliba ya "Kimagufuli" tumpe nchi 2025?


Majaaliwa ya Mungu nadhani atatuvusha vyema zaid ya mzee baba aliyetangulia mbele za haki
 
1. Polepole- Siasa za kistaarabu zisizo za kudhuru watu hasa upinzani anaweza ila ana uwezo mkubwa wa kupambana na Mafisadi na wote wazembe.

2. Bashiru- huyu Mafisadi watapigwa risasi hadharani na ana actions za hapo kwa hapo kama Magufuli.

3. Majaliwa- huyu kutokana na nafasi yake aliyoitumikia ameshaji define hana maamuzi magumu mfano mzuri mambo yanayotokea anaogopa hata ku comment tu. Kwahiyo Nina mashaka naye.

4. Makonda: itoshe kusema ana msimamo mkali sana wa Kimajumui.

5. Tundu Lissu ni kama Magufuli tu ila Lissu atatumia Sheria kuwaangamiza Mafisadi.

6. Mwabukusi- Huyu halitasalia jiwe juu ya jiwe. Yaani atapukutisha kizazi Cha walamba asali wote.
7. Ummy Mwalimu: Anaweza vizur management ila kwenye maamuzi magumu atakuwa kama Mama tu.

8. Juma Aweso: huyu atafaa sana kwasababu akiwa na mamlaka kamili ana maamuzi magumu na actions za papo kwa papo.

9. Mimi Mwenyewe, kwanza mimi nitareform mfumo mzima wa Serikali na nitafukua makaburi kwa yeyote aliyewahi kuhusika na ufisadi nitarara nae Mbere!

Hizo namba sio kwa Ubora au umuhimu ni Serial number tu.
 
Mwabukusi ,Tundulisu,kabudi
 
Namjua ila simtaji.

Ila tu Ataingia na Madhabahu ya Mungu aliye juu itasimama na kuibomoa madhabahu ya baali.

Tusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…