Nani mwenye haki ya kutafuta mpenzi/mchumba?

Nani mwenye haki ya kutafuta mpenzi/mchumba?

MPIKUSASA

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
112
Reaction score
7
Habari za mida hii wanaJF, hongereni kwa majukumu ya kulijenga taifa letu. Nakuja tena kwenu na hoja niliyokumbana nayo huko nje mara nyingi kila nainapotoka katika mjengo huu JF,sasa nimeona nije niwahusishe na ninyi huku tupeana majibu na wakati mwingine tupate mwarobaini wakuwasaidia vijana wenzetu huko nje, mara baada ya kutoka ndani ya mjengo.

Nimekuwa nikikutana na vijana wenzangu wa kiume/kike wakisema "nimesubiria mchumba sijampata" huyo kijana wa kike na kijana wa kiume anasema"natafuta mchumba sijampata" sasa hebu je ni nani kati ya kijana wa kike na kijana wa kiume ana wajibu wa kumtafuta mwingine na nani hana katika suala zima la mahusiano.
 
++
Mwenye hitaji la dhati halitampa nafasi ya kusubiri,,atajikuta tu yumo ndani ya kutafuta.
Mf.mdogo nenda Love Connect
++
 
Nifananishe na wanyama

Me = wala nyama

ke = wala majani

Hapo naamini umepata mwanga.
 
wote wana haki ya kutafuta mtu ampendae usione mke anamkubali mme kimiujiza nae amepanga kutafuta hivyo wote wanawajibu wakutafuta
 
Kwa utamaduni wetu mwanamke anatafutwa, inakua vigumu kwa mdada kuanzisha uzi wa mahusiano ie kutongoza na ndio maana unakumbana na huo msemo kua nimesubiri mchumba na sijampata au nimepata. Na mtafutaji ni mwanaume ndio maana unaona huo msemo kua nimetafuta mchumba sijampata/nimepata. Lakini kwa kipindi hiki cha doti com wote ke/me wanaweza kutafuta wachumba si unajua kipindi cha uwazi na ukweli lkn kuna weakness ktk hili hasa nje ya mji , sidhani kama utaeleweka dada kuanza mazungumzo ya kumuaprochi mwanaume bado haijaweza kupokelewa kivile. Ndio maana hata issue ya kulipa mahari bado ipo kwa mwanaume ie yeye ndie mwenye wajibu wa kwenda kwao mwanamke kulipa mahari.itafikia wakati tutakua kama wahindi dada ataenda kutoa posa kwa wazazi wa mume si itakua poa.
 
Kwingine kote nakubaliana na wewe ila hapo penye red, nadhani haiwezi kuwa poa, acha tu sisi waoaji tuendelee kutoa hiyo mahari.

Hao wahindi acha tu waendelee na tamaduni zao huko na sisi na zetu.
 
Wote wana haki ya kuwatafuta wenzi wao. Wadada siku hizi kuchakarika kivyaovyao kutafuta mume si jambo la ajabu.

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom