Nani mmiliki wa Habari Leo?

Nani mmiliki wa Habari Leo?

Wana jamvi amani iwe kwenu,

Kufuatia gazeti la Hahabri Leo kuamua kuandika habari zinazokibeba CCM nai kuandika habari za kuviponda vyama vya Upinzani, naomba kujua mmiliki wa gazeti hilo, mishahara wanalipwa na fedha za nani?
Ungeuliza kwanza nani mmiliki wa Tanzania Daima kabla ya kudandia gari kwa mbele.
 
Hi nyie wenzetu uelewa wenu hua ukoje!? Magazeti yanayoshabikia ccm yapo mengi, Raiamwema, raia Tanzania, Dira nk. Mleta huja si kwamba hajayaona hayo, ameyaona but hayo ni magazeti ya watu. Hata Uhuru likifanya hivyo hakuna atakae uliza cause ni gazeti la ccm lakini sio Habari leo, Daily news na Sunday news, hata TBC haipaswi kufanya hayo inayoyafanya kwasababu hivi ni vyombo vya umma; unataka kunambia we hulioni hilo!? Mwanahalisi linamilikiwa na Sead Kubenea, mgombea ubunge kwa Chadema pale Ubungo, Tanzania daima linamilikiwa na familia ya Mbowe ambaye ndiye mwenyekiti wa Chadema, ulitegemea iwaje!? Ndio maana UKAWA wanasema kipaumbele chao cha kwanza ni Elimu, uelewa wa kupambanua mambo wa Watanzania wengi uko chini sana.

Jana nimerudi toka kazini napata habari kwamba jirani yangu ananitambia kwamba atanizomea sana UKAWA ikishindwa uchaguzi (hua tunatanian anae sana tu) nikamwambia mimi hata nikiumwa ugonjwa wowote pamoja na familia yangu hua hatutibiwi na hospitali za serikali, mwajiri wangu anachukua jukumu hilo, na wewe je!? Ukweli watu wengi wanadhani kushabikia vyama hivi kwenye hu uchaguzi ni kama kushabikia YANGA na SIMBA, yote hi ni kwasababu ya ELIMU. Unaweza kusona but namna yako ya kupambanua mambo ikawa chini sana. Sorry kwa maneno yangu mengi, nasikia kugadhabika kwasababu mtu mwenye uwezo wa kutumia internet naye hajui kutofautisha magazeti ya serikali na magazeti ya watu binafsi.

Nakushukuru sana kiongozi maneno yako yamejaa ukweli naamini hao wanaojitoa ufahamu wamekuelewa ingawa hawawezi kujubali moja kwa moja
 
Binti ongeza bidii katika kozi yako ya pre form one,huku unapokimbilia si mahali sahihi kwako.Mleta mada kauliza uhalali wa Gazeti la Serikali linaloendeshwa kwa kodi zetu kugeuka na kuwa vuvuzera la chama tawala,na hili nalo umeshindwa kuling'amua ewe kizazi cha BRN zao la Mitihani ya multiplechoice?Umedhihirisha huna unachofahamu,umebaki na akili za "kushedi"OMR tu ktika Mitihani yenu ya kuchagua toka swali 1-50,huna thamani yoyote katika Taifa.Bora ufe tu.

Umemaliza kila kitu
 
Ungeuliza kwanza nani mmiliki wa Tanzania Daima kabla ya kudandia gari kwa mbele.

Ndio maana nakwambiaga kila siku kuwa akili zako ni afadhali ya zile za ndezi, mbona sijauliza gazeti la uhuru na mzalendo?
 
Tanzania daima ni gazet la mtu binafsi hivyo yuko huru kuandika habari kwa interest zake kama ilivyo star tv ila habar leo ni gazet la serikali alitakiwi kufungamana na upande wowote kwan linaendeshwa kwa kod za wananchi wote bila kujar itikad za vyama
 
Mkuu kwa vijana wa lumumba kuukubali ukweli wa jambo hilo ni ngumu
 
Kampuni ya magazeti ya Serikali. Haiendeshwi kwa kodi za wananchi.
Daily News na Habari Leo hujiendesha yenyewe kwa mauzo na Matangazo.
TSN inalipa kodi serikalini kama kampuni ingine yeyote ile.
Nao pia wana uhuru wa ku support upande wowote ule. Na hasa kwa maslahi ya taifa.
 
Nilicomment kwenye gazeti mtandao Lao kumkosoa waziri WA habari,wamenipiga ban pamoja na IP yangu
funny thing walikuwa wamesha print comment hizo
 
Kitaeleweka tu mwaka huu huo ujinga wenu ndio umefikia mwisho wenu maana lowasa ndio huyooo ikulu
 
Nilicomment kwenye gazeti mtandao Lao kumkosoa waziri WA habari,wamenipiga ban pamoja na IP yangu
funny thing walikuwa wamesha print comment hizo

Ukombozi ndio unakaribia mkuu
 
Wana jamvi amani iwe kwenu,

Kufuatia gazeti la Hahabri Leo kuamua kuandika habari zinazokibeba CCM na kuandika habari za kuviponda vyama vya Upinzani, naomba kujua mmiliki wa gazeti hilo, mishahara wanalipwa na fedha za nani?
Ndio linaandika habari za ccm,sasa mtu kalala we utaandika nini,acha ulofa ImageUploadedByJamiiForums1445590447.471608.jpg
 
Kampuni ya magazeti ya Serikali. Haiendeshwi kwa kodi za wananchi.
Daily News na Habari Leo hujiendesha yenyewe kwa mauzo na Matangazo.
TSN inalipa kodi serikalini kama kampuni ingine yeyote ile.
Nao pia wana uhuru wa ku support upande wowote ule. Na hasa kwa maslahi ya taifa.

Upo sawa? Kama TBC imeshindwa kujiendesha bila ya Ruzuku hao TSN wataweza?

Tofauti Mali ya umma na Mali ya mtu binafsi. Hawana uhuru wa kuamua kuwa na upande. Iwe ni kwa mujibu wa sheria au kimaadili.
 
Upo sawa? Kama TBC imeshindwa kujiendesha bila ya Ruzuku hao TSN wataweza?

Tofauti Mali ya umma na Mali ya mtu binafsi. Hawana uhuru wa kuamua kuwa na upande. Iwe ni kwa mujibu wa sheria au kimaadili.

Yaambie hao magamba mkuu
 
Upo sawa? Kama TBC imeshindwa kujiendesha bila ya Ruzuku hao TSN wataweza?

Tofauti Mali ya umma na Mali ya mtu binafsi. Hawana uhuru wa kuamua kuwa na upande. Iwe ni kwa mujibu wa sheria au kimaadili.

Mkuu na huu ni ufisadi kama ulivyo ufisadi mwingine wa kutumia kodi za watanzania kwa kuifanyia kampeini ccm
 
Upo sawa? Kama TBC imeshindwa kujiendesha bila ya Ruzuku hao TSN wataweza?

Tofauti Mali ya umma na Mali ya mtu binafsi. Hawana uhuru wa kuamua kuwa na upande. Iwe ni kwa mujibu wa sheria au kimaadili.
Tofautisha TBC na Daily News. TV ni huduma. Hawafanyi biashara. Hawauzi chochote. Daily News hadi sasa ndilo gazeti la kiingereza lenye highest circulation. Pia lina Matangazo mengi katika Africa Mashariki. Kampuni imeizidi Mwananchi kwa revenue zaidi ya mara tatu.
Msikariri ki ukawa ukawa ujinga ujinga, tumieni akili au nendeni Maelezo mkapate taarifa za magazeti.
Daily News ndio inaendesha hata TBC ila kwa ushamba wenu wa vijijini unadhani TV ndio kila kitu. Ulofa nao
 
Back
Top Bottom