Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Najaribu kujiuliza kama sio utapiamlo wa uelewa kumbe ni kitu gani hiki? Mbona kinachoendelea kwenye siasa zetu ni uadui ule wa weusi na makaburu enzi zile za Afrika ya kusini?
Kwani ACT wakishinda Zanzibar watanzania watafutwa kwenye kitabu cha uzima? Au CHADEMA wakishinda bara ardhi yetu itapoteza rutuba? Madini yetu yatayeyuka yasionekane? Mlima Kilimanjaro utahamia Kenya. Au mbuga zetu za wanyama zitaibukia Uchina?
Hivi kwa mfano CCM wao wakishindwa hawatakuwa ni mawazo mbadala yapendwayo na watanzania dhidi ya serikali itakayokuwepo madarakani? Hivi kweli tumeshindwa kuelewa lengo la demokrasia ya vyama vingi?
Kwani nani kawadanganya CCM kwamba watatawala nchi hii milele? Au nani kawaongopea wapinzani kwamba wakiingia madarakani hawatatolewa siku wakiboronga?
Kwanza ikitokea Upinzani umeshinda na kutawala, mimi nitahamia CCM watakaokuwa wapinzani.
Kwangu mimi Demokrasia ni upambanishi wa hoja na si mapambano ya watu. Ukiona chama cha siasa kinachukia hoja na kurukia viroja ujue hicho ni kitu kingine.
Hivi ingelikuwa demokrasia ni vita kama wadhaniavyo wengine; sidhani kama mwalimu Nyerere angewaachia wajukuu zake hicho kitu.
Ujue mpaka sasa tayari tumeshapanda mbegu za chuki, ubaguzi, na magomvi. Ndiyo maana ukiwaangalia watu wamekaa mkao wa kusubiria mavuno yake!
Ndugu waTz kama siasa zenyewe ni hizi za kuchukiana mpaka kuuana kuna haja gani ya kuendelea nazo?
Hivi kweli sisi kama taifa tumeshindwa kustaarabika kiasi tufanye siasa za kistaarabu.
Mpaka lini tutaendelea kugombania utawala kama manyani yanavyogombania na wenzao huko maporini?
Hapana, nadhani hii njia tunayopitishwa siyo nzuri kwa mustakabari wa Taifa hili.
Hivi nani alituroga kiasi cha kujali vyama vyetu kuliko taifa letu. Hadi tunaona ni aheri taifa zima lisambaratike kuliko chama chetu kishindwe kwenye uchaguzi.
Ee mama Tanzania, nani atakayekuhurumia, akuponye na maradhi yanayokukabiri?