nAnI kAsEmA ''wAnAuMe'' hAtUnA kU.....???

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
NANI KASEMA WANAUME HATUNA KUMBUKUMBU????

Soma hii......

Mwanamke kashituka kutoka usingizini usiku wa manane na kugungua mumewe hayupo kitandani.

Mwanamke akachanganyikiwa na kuamua kushuka hadi chini. Akamkuta mumewe ameketi juu ya jikoni, kikombe cha kahawa kikiwa mbele yake huku akionekana kusononeka sana. Mwanamke akamtazama mumewe aliyekuwa akijaribu kujifuta machozi.

"Mume wangu una tatizo gani?" Akamwuliza huku akimsogelea. "Kwa nini upo huku usiku wote huu?"

Mumewe akauinua uso wake. Akamtazama. Kisha akamwuliza, "Unakumbuka miaka 20 iliyopita tulipokuwa tumeanza kuwa wapenzi tukiwa na umri wa miaka 17 tu?"

"Nkumbuka sana mume wangu. Jamani you are so sweet umenikumbusha mbali." Mwanamke akajibu huku akiubusu mkono wa mumewe.

"Unakumbuka jinsi baba yako alivyotufuma kwenye siti ya nyuma ndani ya gari langu?" Mwanaume akauliza kwa sauti ya tuo.

"Nakumbuka sana mume wangu!" Mwanamke akajibu huku akiketi sambamba na mumewe.

Mwanaume akaendelea kuongea. "Unakumbuka baba yako alivyonioneshea bastola yake kichwani mwangu na kuniambia aidha nikuoe, ama anipeleke jela miaka 20?"

Kwa sauti ya upole mwanamke akajibu, "Nakumbuka sana mume wangu. Tumepitia mengi mpenzi."

Mwanaume akanywa funda moja la kahawa. Kisha akaongea. "Leo ningekuwa natoka zangu jela.....na kuwa huru mtaani!"
 
teh teh teh. BAMpani una swagga. kwanini ukumalizia hilo neno?
 
Last edited by a moderator:
Halafu unataka kuleta utata kwenye heading yako kwa kuandika ku... badala ya kumalizia kumbu kumbu!!!

Kwa hiyo ni bastola iliyompa mke?
 
teh teh teh. BAMpani una swagga. kwanini ukumalizia hilo neno?

si ili wewe upate mvuto nini kilichoandikwa, sasa umesoma na ujumbe umeupata. KARIBU SANA EROTIKA!!!
 
Last edited by a moderator:
Iweke ya Kiingereza ndio inaleta maana zaidi, kuitafsiri umeitoa ladha yake.

Ina maanisha bora ya jela angekuwa anatoka lakini hizo pingu za maisha ndio anazo.
 
Kwahiyo jamaa angeaamua kumuacha maana mzee au baba mkwe alikuwa nia ya kumuoza binti kwa huyo jamaa kwa miaka 20.au nimewahi story ijaisha?
 
NANI KASEMA WANAUME HATUNA KUMBUKUMBU????

Soma hii......

Mwanamke kashituka kutoka usingizini usiku wa manane na kugungua mumewe hayupo kitandani.

Mwanamke akachanganyikiwa na kuamua kushuka hadi chini. Akamkuta mumewe ameketi juu ya jikoni, kikombe cha kahawa kikiwa mbele yake huku akionekana kusononeka sana. Mwanamke akamtazama mumewe aliyekuwa akijaribu kujifuta machozi.

"Mume wangu una tatizo gani?" Akamwuliza huku akimsogelea. "Kwa nini upo huku usiku wote huu?"

Mumewe akauinua uso wake. Akamtazama. Kisha akamwuliza, "Unakumbuka miaka 20 iliyopita tulipokuwa tumeanza kuwa wapenzi tukiwa na umri wa miaka 17 tu?"

"Nkumbuka sana mume wangu. Jamani you are so sweet umenikumbusha mbali." Mwanamke akajibu huku akiubusu mkono wa mumewe.

"Unakumbuka jinsi baba yako alivyotufuma kwenye siti ya nyuma ndani ya gari langu?" Mwanaume akauliza kwa sauti ya tuo.

"Nakumbuka sana mume wangu!" Mwanamke akajibu huku akiketi sambamba na mumewe.

Mwanaume akaendelea kuongea. "Unakumbuka baba yako alivyonioneshea bastola yake kichwani mwangu na kuniambia aidha nikuoe, ama anipeleke jela miaka 20?"

Kwa sauti ya upole mwanamke akajibu, "Nakumbuka sana mume wangu. Tumepitia mengi mpenzi."

Mwanaume akanywa funda moja la kahawa. Kisha akaongea. "Leo ningekuwa natoka zangu jela.....na kuwa huru mtaani!"

Mkuu hii ni stori nzuri lakini ni ya kusadikika na inakosa mantiki.
Hizo sehemu zenye maandishi mekundu ndio zinazonipa picha kuwa hii kitu ina mushkeli.
Ukisoma vizuri utagundua kuwa hawa watu walioana miaka 20 iliyopita, ambapo walikuwa na miaka 17 tu.
Halafu umejaribu pia kuonesha ukali(umakini) wa baba wa mwanamke hata akafikia kumtolea mkwewe bastola.
Sasa ni baba gani aliye makini kiasi hicho akaruhusu binti yake aoelewe katika umri mdogo hivyo?

Otherwise ni story nzuri kama ungerekebisha hizo kasoro.
 
Back
Top Bottom