teh teh teh Felix bana! Ila mkuu una mawe sana hebu tupe ajira basi.
Mwenzangu mimi nilikuwa nautamani sana unene ila kwa artical yako siutaki tena kabisaaaaa!!! kilicho nifanya niutake unene ni hivi. siku moja nilinunua nyumba pale kinondoni ni kama nilinunua kiwanja tu kwasbb ilikuwa ni mbovu. nyumba hiyo ilikuwa inakaribia barabara ya lami ila kwa mbele yangu ilikuwa na nyumba moja tu ndo ufikie lami. madalali waliniambia hata hiyo nyumba wenye nayo wanaiuza. hivyo nilifanya biashara ya kununua ile nyumba ya kwanza na nilikuwa na malengo ya kujenga ofisi ya ghorofa moja tu kwa mjengo wa kawaida. kwa bahati mbaya majirani walio kuwa mbele yangu wakitazama barabara ya lami waligombana baada ya baba yao kufariki hivyo wakashindwa kuelewana na hivyo waka kataa kuni uzia nyumba yao wakawa na kesi mahakamani kwasbb marehem alikuwa na wake wawili watoto 15!
Baada ya kuwa wamekataa kila mtu kivyake, nilikata tamaa ya kujenga ofisi yangu uku mbele yake kuna nyumba nyingine. hivyo nilimwambia dalali wangu anitafutie mteja nikauze tena then nikanunue nyumba nyingine. Nashukuru dalali alimtafuta mteja, na kumbuka mteja mwenyewe alikuwa ni waziri flan (.................) nilimwambia dalali leta mteja aone akiridhika na yuko tayari kufanya biashara niite. baada ya muda niliutwa na kuambiwa mheshimiwa flan anataka kununa nyumba yangu na hivyo niende ananisubiri. Baada ya kufika nilikuta gari aina ya Londcruza VX limepak pale na mimi pia nilikuwa na gari yangu. sasa basi niliposhuka kwenye gari yangu yule waziri nikamsalimia akaanza kuniangalia toka juu mpaka chini! akaniambia wewe mtoto tunamsubiria baba yako mwenye nyumba hii tufanye biashara yuko wapi?
Nikamjibu ni mimi ndiye mwenye nyumba hii! yule waziri akasema ni nyumba ya urithi? ni kasema hapana, akanijibu mmmmmm mbona kamwili kako kadogo dogo mimi nilifikiri baba yako anakuja!! ukweli tokea siku hiyo nilichukia kuwa mwembamba nikaanza kula lakini jamani wapi sinenepi!!! nilikula sana misosi unene nikawa sipati mpaka leo. tulifanya biashara ila yule mzee alionesha kunidharau kwasbb ya kuwa mwembamba. mkuu kwa artical yako si taki tena unene nitabaki tu hivyo mwaya!!!!!!!!!!. hivi ni kweli mili ingine hata ule vipi haizi kunenepa?
Afu nimegundua ni wanaume ndio wanachukulia wembamba wao kama tatizo...kwa sababu jamii inaheshimu wanaume warefu na waliojaa jaa..kuna kaka yangu hivyo hivyo alipalilia kitambi sasa hivi ameshapigwa red flag na doctor...kisukari inamnyemelea na hajafika hata 45...hatare kuliko tunavyodhania...
Alishaanza kuingia gym kabla ya doctor ku detect tatizo; lakini kilo zilikuwa hazishuki...sasa ameanza kutokula vyakula kibao...shida kweli kweli...nadhani vitisho vya doctor vitamfanya awe more serious...
Afu nimegundua ni wanaume ndio wanachukulia wembamba wao kama tatizo...kwa sababu jamii inaheshimu wanaume warefu na waliojaa jaa..kuna kaka yangu hivyo hivyo alipalilia kitambi sasa hivi ameshapigwa red flag na doctor...kisukari inamnyemelea na hajafika hata 45...hatare kuliko tunavyodhania...
Alishaanza kuingia gym kabla ya doctor ku detect tatizo; lakini kilo zilikuwa hazishuki...sasa ameanza kutokula vyakula kibao...shida kweli kweli...nadhani vitisho vya doctor vitamfanya awe more serious...
kama unataka kuzaa mtoto kama mjusi neenda kaoe mwembemba sasa.
siwapendi wembamba.
Kumbe kamwili kangu dili eeh... Mie mwenyewe nilikuwa najichukia na kamwili kangu....
Siku moja nilikwenda hosp, Dr.akaniuliza unasoma wapi?
Siku nyingine nikawa napita Karume wacha wale wauza mitumba waniite "Wakusoma njoo kuna begi zuri hapa la shule" "Wakusoma njoo kuna viatu vya shule vya ukweli"...Lol mie mama mtu mzima nasoma khaaa..... Ila saiv najikubali jamani awali nilikuwa najiona kembambaaa mpaka natisha!!
hhaaaaa naomba nicheke mana ni kama umenisema mimi........mwe.....
Hahahaa.... Wakusoma kumbe tupo wengi eeeh!!! sasa ndio ukute na nywele unakata, ndio unakuwa Wakusoma square...
hahaaaa na nywele nilikata sasa ikabidi nianze kusuka tena mana ilikuwa ni shida......na nina mtoto nikawaambia huyu mwanangu ndo kabisa.......wanasema mtoto kazaa mtoto......
weka ya ki afrika......utakuta tumbo uko.....
Hahahaaa.... Yaan hatutofautiani, ila mie kusuka bado. Nikimwambia mtu umri wangu anakataa... Et anasema ntakuwa kwenye 22/23yrs huwa nacheka mno.
Ila ni jambo la kushukuru make tuna kaudongo fresh..
Geuza simu yako kwa nyuma utaliona tumbo, flat..... :becky: