Nani kasema slaa ameshindwa?


Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Messages
6,920
Likes
7,526
Points
280
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined May 1, 2007
6,920 7,526 280
So far, matokeo yaliyotangazwa ni ngome za CCM, na CUF, bado matokeo kutoka sehemu nyingine nyingi sana hayajatangazwa, na inawezekena JK ameanguka vibaya sana ndo maana wanachelewesha matokeo ya sehemu hizo.
Bila Matokeo ya halali kutoka nchi nzima kutangazwa, hawawezi kuniconvice kwamba Slaa kashindwa.
na hii delay tactic yao wala mimi hainisumbui, wacheleweshe, wasicheleweshe watatangaza tu, na matokeo yaliyochakachuliwa yatajulikana tu.

Kitu kimoja ninachowaonea huruma Watawala wanaoingia madarakani kwa kupindisha demokrasia ni ile kukosa hali ya kujiamini wanapodeal na matatizo ya wananchi, hukosa hali ya kujiamini hata wanapokutana na viongozi wenzao duniani, Na kibaya zaidi ni kule kusutwa na roho sana hata baada ya kuondoka madarakani. upweke, na unyonge wa hali ya juu huwaandama watawala wa aina hii.

Ego inaweza kukusukuma ili kumshinda mpinzani wako , lakini je ni wangapi unaowaumiza katika kutekeleza azma yako?.
 

Forum statistics

Threads 1,236,314
Members 475,050
Posts 29,253,944