Dk. Slaa mwanamume! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa mwanamume!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Boramaisha, Nov 2, 2010.

 1. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wana-JF wapenda mabadiliko ya kweli yenye manufaa kwa nchi yetu hatuna budi kumpongeza kwa dhati kutoka ndani ya nyoyo zetu Dk. Wilbroad Peter Slaa kwa kazi nzuri na kubwa mno aliyoifanya kwa Chama chake CHADEMA, kwa Tanzania yetu na Watanzania wanyonge kwa ujumla.

  Awali ya yote, Dr. Slaa amejinyanyua na amekinyanyua chama chake juu kabisa. Dr. Slaa amekuwa tishio na mwiba uliowachoma viongozi wa CCM katika kipindi chote cha Kampeni na upigaji kura. Dr. Slaa aliweza kubadili hali ndani ya CCM na chama hicho kutokuwa na uhakika wa ushindi na hata pale viongozi wa juu wa CCM nyuso zao zilionyesha taharuki walipokuwa wakitumbukiza kura zao kwenye masanduku ya kura. Dr. Slaa amefanikiwa kuondoa kujiamini kupita kiasi kwa viongozi hao wa CCM na wanachama wa chama hicho kwamba ushindi kwao hauwezi wakati wote kuwa wa cheeeee kama ilivyokuwa huko nyuma. Dr. Slaa alipoingia ulingoni kila kitu kilibadilika. Asante Dr. Slaa kwa kuwaamsha viongozi wa CCM na wanachama wao kutoka lindi la usingizi la kudhani kwamba wakishavaa magwanda ya kijani na njano kwenye mikutano ya kampeni basi wataendelea kupata na kuchaguliwa kuwa watawala wa nchi hii daima dumu.

  Dr. Slaa amefanya tuelewe kwamba CCM sasa kimefikia ukingoni katika uhalali wa kuiongoza Tanzania yetu. Dr. Slaa ameweza kutuonyesha jinsi CCM kilivyooza na kuharibika kutokana na vitendo vya rushwa iliyokithiri tangu kwenye kura za maoni za chama hicho hadi kipindi chote cha kampeni. Je. CCM wanaweza kututajia ni mgombea gani wa chama hicho ambaye hakutoa chochote kuwashawishi wananchi wamchague? HAKUNA!

  Dr. Slaa ametufungua macho, masikio na akili zetu kuelewa kwamba bila kutumia nguvu za ziada za rushwa na mabango kila kona, CCM si lolote kimepoteza mvuto na uhalali wake wa kuongoza wananchi. Wakati wote CCM imekuwa ikipanga mbinu mbalimbali za kujitafutia ushindi kwa nguvu, ushindi usio halali. Tumejionea wenyewe jinsi ambavyo kura za mijini na vijijini zilivyoweza kuwa na tofauti kubwa. Kwa nini? Kwa sababu CCM wametumia umaskini wa wananchi wa mijini na vijijini kama mtaji wao wa kupatia kura. Wamewahonga wananchi t-shirt, kofia, skafu, pombe, sukari, chumvi, kanga, pikipiki, baiskeli, vijisenti viduchu kiasi cha elfu moja ama mbili n.k. ili waweze kupata kura kutoka kwao. Ni aibu kubwa kwa Chama chochote cha siasa kufanya mambo hayo kwa makusudi ya kuwarubuni wananchi ili chama hicho kichaguliwe.

  Wana-JF wapenda mabadiliko na wanaoitakia mema Tanzania yetu, hatuna budi kumshukuru sana Dk. Slaaa kwa kuweza kutufumbua macho na kuweza kuyaona maovu yote hayo kwa ukweli, uwazi na mwanga zaidi.

  Tumuombe Dk. Slaa asife moyo kabisa kwa kukosa ushindi katika uchaguzi huu. Yeye ni shujaa na tena ni ‘Rais' wa Watanzania wanyonge aliokuwa akijaribu kuwatetea kwa dhati majukwaani akionyesha dhahiri kuwa na uchungu wa dhati kwa Watanzania hao waliopigika. Tumuombe Dk. Slaa asherehekee ushindi wake yeye binafsi na ushindi wa CHADEMA na hata wa vyama vingine vya Upinzani vilivyoweza kupata viti Bungeni na kwenye safu ya Udiwani ambao tunaamini kabisa umetokana na yeye Dk. Slaa na si vinginevyo.

  Tumuombe na tumuunge mkono Dk. Slaa aanze sasa kukijenga na kukiimarisha CHADEMA tayari kwa mapambano mapya ya 2015. Twendeni vijijini tumsaidie. Hatuendi huko tukiwa tumebeba mafurushi ya kanga, t-shirt n.k. lakini tunakwenda huko na dhamira ya dhati ya kuwaelimisha wananchi wenzetu kwamba maisha bora kwao yataweza kuja tu pale watakapoelewa nini maana ya utawala bora na haki yao ya msingi ya kuweza kugundua na kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia kuyatafuta hayo maisha bora kwa kutumia raslimali ambazo ni mali ya kila Mtanzania kwa manufaa ya Watanzania wote na si wachache.

  Zaidi ya hayo, ushindi wa CCM safari hii na amani na utulivu katika upigaji kura na kusubiri matokeo na kuyakubali vimetokana na kile alichokijenga Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kinachoshangaza, CCM wamebaki kujisifia wao juu ya hali hiyo na kutaka kurushia lawama kwa vyama vya upinzani kila zinapotokea rabsha ndogo ndogo wakisahau kwamba wananchi wa Tanzania bila kujali vyama vyao ndio wadau wakubwa na wajengaji wa hali hiyo ya amani na utulivu iliyotamalaki kwa miaka mingi hadi kuonekana ni jambo la kawaida. Cha kushangaza zaidi ni kwamba CCM kwenye kampeni zao wameonekana dhahiri kunyanyapaa hata jina la Mwalimu Nyerere! Mgombea gani wa CCM aliyejaribu kuomba kura kwa kutumia jina la Mwalimu Nyerere zaidi ya Dk. Slaa wa CHADEMA?

  Tumuombe Mungu ampe Dk. Slaa nguvu na uwezo wa kuendelea kupambana kwa manufaa ya Watanzania. Mungu ampe ujasiri wa kufuata nyayo za Baba wa Taifa.

  Dk. Slaa ni Mwanamume! Ameweza kuwanyima usingizi viongozi wa CCM waliodhani kuwa kwao uongozi wa nchi yetu ni haki yao ya kuzaliwa!

  HONGERA SANA DK. SLAA, NA MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA!
   
 2. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Well noted! Asante Dr. Slaa! Watanzania watakutambua wewe kama raisi wao mioyoni mwao hata kama kura zako zimechakachuliwa!
   
 3. k

  kamasi New Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa. Ndugu Dr Slaa, ataendelea kuwa Raisi wetu wa moyoni. He has won not only the battle of credibility but also our hearts and mind.

  God bless Dr Slaa.
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa wanapenda mababiliko na mageuzi ya kisiasa tumuunge mkono Dr Slaa na CHADEMA.
   
 5. A

  Aine JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  We congratulate uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu regardeless what, you are the worrior
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  Moyo wangu unaniambia Dr Slaa atashinda uchaguzi huu.
  Kichwa changu kinaniambia maluweluwe mengine lakini miye nausikiliza moyo wangu tuu.
  Sema moyo, sema moyo wanguu.
   
 7. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini watu Mmeshajipandikizia kua Dr Slaa hatashinda? CCM wamefanya makusudi kutangaza yale majimbo waliyoshinda ila pale aliposhinda Dr Slaa hawajatangaza. Mi naomba watu msifanye hitimisho na kukubali matokeo kabla hayajatangazwa..

  Kueni makini, siasa ni mchezo mchafu and we have to play very smart.!!!!!
   
 8. W

  We can JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu wanaweza kuchakachua kura zako, lakini hawawezi kuchakachua akili yako. Na ikitokea wakachakachua akili yako, KAMWE hawawezi kuchakachua ROHO YAKO, Viva Wilbroad; I have a big trust on you. Imani yangu kwako iliongezeka pale ulipowanandi wabunge wa vyama vingine visivyo CHADEMA, pale ulipoamini kuwa wanajitahidi; mfano ulimnadi mpambanaji Dr. Mwakyembe wa CCM-ILINIGUSA SANA, once again VIVA Dr. Slaa.
   
 9. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli Mkuu, nashangaa watu wameshakubali matokeo kabla hayajatangazwa.
  Matokeo yakitoka tuna haki ya kuyakubali au kuyakataa..
   
 10. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mimi rais wangu ni Dr Slaa, mwingine kimeo tu! Nawaahidi watanzania wenzangu, Dr Slaa na wana-CHADEMA wote, niko tayari kuwa mmoja ya wale watakaoenda kukijenga chama mara baada ya uchaguzi huu. Anytime, any place. Nawakaribisha vijana woote, tujitume katika kuikomboa nchi yetu!
   
 11. N

  Nesindiso Sir JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ujumbe mzuri sana wa shukrani kwa Dr. Slaa (Shujaa wa taifa)
   
 12. p

  p53 JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ujumbe huu ni mzuri lakini ningeupokea vizuri kama matokeo yote ya uchaguzi wa udiwani,ubunge na urais yangekuwa yameshatoka.Mwandishi unaposema Slaa ajipange kwa 2015 wakati uchaguzi wa 2010 haujaisha sikuelewi.
   
 13. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  It breaks my heart to read this msg. Mimi na vijana kumi, tuliacha biashara zetu na kukimbilia kupanda train ili tuje tushiriki ktk uchaguz kwa kumchagua Mh. Dr. Slaa, Sugu na madiwan wa Mbeya.
  Like all my colleagues 've said, lets all stand by our dear president Dr. Slaa, the true patriot & humble servant. Don't lose hope mkuu, we shall stand by yo side all the way to ikulu this yr if not in 2015. Pls be our hero till we win. Someday, we will sit back,reflect & smile.
  Dr. Slaa, u a my star. Pls hang on in there coz pamoja CHANGE WILL COME. Yes We Can!
  I salute u & all Chadema cadres!
   
 14. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Dr. Slaa atashinda matokeo bado hayajatangazwa acheni kukata tamaa mapema, wanajitahidi kuchakachua lakini kura hazitatosha.
   
 15. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hata mimi niko pamoja nanyi Dr.Slaa 4Life!
   
 16. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  Big up sana kwa dr wa ukweli na chadema kwa ujumla tusikate tamaa tutasonga mbele, natoa wito kwa wapenda mageuzi wote tushirikiane kujenga chama cha chadema SI tu kwa mawazo bali hata kwa michango ya fedha ili kiweze kuwa imara Kila nyanja
  Au wapenda mageuzi mnasemaje
   
 17. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  Hata mimi bado naamini kuwa Dr Slaa, CHDEMA na Watanzania Tutashinda!
   
 18. z

  zantel Member

  #18
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Boramaisha umesema iliyokweli ya watanzania wote, hata wasiopenda kusema ukweli hlo wanalikubali, kazi imeonekana, palipokuwa na miti sasa pana makazi na watu wamenawa, hawana matongo tongo, Hakika Padri alikuja kikazi zaidi, Viva Slaa Viva,, ALUTA KONTINUA.
   
 19. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Dr. Slaa ni mpiganaji wa kweli, ni mtu ambaye unaweza kuusoma moyo wake na mawazo yake na kujilizisha kuwa jamaa ni HONEST na mwenye kuitakia mema nchi hii. Watanzania wataendelea kumheshimu na kumwamini Dr Slaa kwa uwezo wake na ujasiri mkuu alionao. Tunaamini kutoka mioyoni mwetu kuwa Dr. Slaa ni kiongozi wetu hata kama hatakuwa pale magogoni!

  KIONGOZI NI YULE ANAYEWEZA KUISHAWISHI MIOYO YA WATU WAKAFANYA KITU KWA HIARI YAO PASIPO KULAZIMISHWA.

  TUNAHITAJI KIONGOZI ATAKAYEWEZA KUTUFANYA TUONE FAHARI KUITUMIKIA NCHI HII KWA MOYO WETU WOTE.


  CCM can rule this country but will not rules TANZANIANs!

  Nilikuwa na suggest CHADEMA tuandae event kubwa ya kumpongeza Dr. Slaa. pamoja na kutafakari mstakabali wa Nchi yetu.... Sijuwi tunaweza kuifanyaje... tunaweza kuchangia mawazo namna ya kuifanya ili kumtia moyo na kumhakikishia kuwa bado tunamuunga mkono yeye pamoja na wabunge wateule na Chama kwa ujumla. Hata kama CCM wataiiga,hawatapata credibility kama ya Chadema.


  MUNGU MBARIKI Dr.slaaa, MUNGU WABARIKI WABUNGE WA CHADEMA,MUNGU WABARIKI WANACHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Dr slaa wa ukweli. Amenifanya nipende kufatilia siasa.
  Bado nina matumaini ya ushindi kwa dr. Sijawazia kushindwa hata mara moja tangu mchakato umeanza.
  God bless Dr Slaa.
   
Loading...