Nani Kasema Kikongwe Harembwi?

Nani Kasema Kikongwe Harembwi?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,157
Reaction score
166,119



Nyota wa muziki wa mwambao Bongo, Fatuma Baraka ‘Bi. Kidude’ AKIWA AMEREMBWA SEHEMU ZA MDOMONI NA MACHONI KWA RANGI NYEKUNDU.
 
Mwanamke yeyote yule ni lazima uwe mrembo japo si kwa kujipaka yale mapoda mpaka tukusahau. Mwanamke hata kwa vitabu vya dini anasemwa ni pambo, sasa pambo likikaa hovyo hovyo utalitamani??

Hata ukiwa mzee jiweke vizuri, (tafadhali sizungumzii mkorogo wa kienyeji na ule wa madukani). Hata mzee kama Bi Kidude anastahili kupambwa. Mwanamke hata kama uko nyumbani hebu paka kale ka wanja kidogo, bana ua chana nywele vizuri, vaa vazi la heshima na tanashati, si mikanga kutwa nzima, nyonyo linacheza ndani ya nguo, akibisha hodi mgeni unakimbilia ndani!!!

Hata ukizeeka kale ka pedo kako ka heshima hebu vaa tu. Na wanaume ni vema wake waambie wawe mnavyotaka na ndoa itadumu. Kwa nini ukimbilie wa pedo na lipstik mitaani wakati wa kwako unaweza kumwambia unataka apake lipstik na pedo? Tena ikiwezekana nenda dukani ukamfanyie shopping ya vile vitu ambavyo unataka awe navyo na vinakufurahisha. Tuokoe na kuponya ndoa/mahusiano yetu, ni rahisi tu.
 
Nasikia bi kidude amefungua chuo kikuu cha mambo ya ki ndoa huko kwao zanzibari
 
Back
Top Bottom