Siri Nzito: Nani Kamficha Gwajima? Ukweli Wafichuka!
Watu wanauliza, Gwajima yuko wapi?
View: https://www.youtube.com/watch?v=Rfnzebx0oiY
Wengine wanasema kafichwa na watu: na anatumia mbinu za kibinadamu kujificha ikiwemo kutotumia simu, kubadili makazi mara kwa mara, na kumtumia mwanasheria wake, Kibatala, kuzungumza na wale wanaomhitaji.
Wanaosema kafichwa na Mungu wanaamini inawezekana kwa sababu yeye si wa kwanza kufichwa! Waumini wake wanakwenda mbali zaidi kwa kudai Gwajima alifanya maombi ya kujificha mbele yao!
Kwa mujibu wa Biblia, watu kazaa wamewahi kufichwa na Mungu miongoni mwao ni:
Musa alifichwa dhidi ya mauaji ya watoto wa kiume yaliyokuwa yanafanywa na Farao.
Ayubu aliwekewa ulinzi na Mungu dhidi ya kuteswa na shetani mpaka shetani alipoomba ruhusa kwa Mungu na kuruhusiwa.
Yusufu, Mariamu na Yesu, walifichwa Misri na Mungu wakikimbia nia mbaya ya Herode ya kuua watoto wote wachanga.
Daudi aliokolewa kutoka mikono ya Sauli. Mfalme Sauli alimuwinda Daudi miaka mingi akitaka kumuua lakini Mungu alimficha mara zote.
Eliya alipowaua manabii wa Baali, Mungu alimwongoza Eliya kukimbilia jangwani, akampa chakula na maji na hatimaye akamficha katika pango ili kumlinda kutokana na ghadhabu ya Yezebeli.
Nabii Yeremia alikabiliwa na upinzani mkali na vitisho vya kuuawa kutokana na ujumbe wake. Mungu alimlinda mara kadhaa, ikiwemo wakati alipofichwa na Baruku mwandishi wake na pia alipoahidiwa ulinzi na Mungu mwenyewe.
Gwajima kafichwa na nani?
Ni swali gumu linalohitaji muda na uchunguzi. Hata hivyo jibu linalokubalika na wengi ni hili, “Watu wanaomwamini Mungu, wamemficha Gwajima.”