Nani kama mama, huu msemo upo tofauti kwangu

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Nani kama mama ni msemo maarufu sana tangu zama za kale hadi sasa!,hakuna chakubalisha katika msemo huu!,pia mara kadhaa ama kila siku watu wamekuwa wakiwasifia mama zao kuwa ni bora sana na pia wamewapambania sana hadi kufikia hapo walipo!,sina shaka na hilo.

Lakini mbona sisi wengine imekuwa ni tofauti sana! Yaani machungu yaliyosababishwa na mama zetu ni makubwa sana yaani hadi unajiuliza hivi huyu ni mama mlezi kweli ama aliniokota tu barabarani!

Yaani sisi wengine tusipokuwa na pesa hata mama zetu hawapokei salamu zetu ! Hauthaminiki tena kama ni Mtoto wake! Pengine unaweza ukisema labda hali hii inaweza kumkumba Mtoto jeuri kwa wazazi wake la hasha! Sisi wengine hatujawahi hata kunyanyua mdomo kumsonya mama wala kukataa kutumwa chochote wala kubishana chochote lakini matokeo yake ni tofauti sana!

Nimeshawahi kuwa natuma pesa kwa mama mzazi ili nijengewe nyumba kwa muda wa miaka mitano niliyokuwa nje ya Tanzania [emoji1241] nakuja nakuta kiwanja hakina hata msingi, nishatuma pesa ili nilimiwe mashamba na mama mzazi na hakulima hata mita mbili.

Nilishawahi kutuma pesa ya maendeleo fulani lakini hakikufanyika chochote na ukiuliza anakuwa mkali kweli kweli! Kama Mtoto unajishusha na maisha yanaendelea!

Cha kushangaza akisikia umemsaidia ndugu yeyote anakununia na hamtaongea kwa muda mrefu! Hayo ni machache sana nayoweza kuweka wazi lakini zaidi ya asilimia 90 niliyofanyia itabaki ni siri yangu hadi siku ya mwisho!

Yaani huwa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa natamani hata nimkate kibao ila nikiangalia kuna wengine wamesaidiwa sana na mama zao nakuwa mpole!

Ni wengi tunapitia changamoto kwa wazazi wetu njooni hata tufarijiane ili kupunguza stress mbali mbali
 
Mmh mzazi tena mama anamchukia mtoto hii ni ajabu kubwa sana aiseee

Kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia aiseee mama mzazi kabisa

Isaya 49:15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Mungu amsaidie sana kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia aisee keep your eyes kwenye why anakuchukia kuna Roho ya shetani nyuma.
 
Nani kama mama ni msemo maarufu sana tangu zama za kale hadi sasa!,hakuna chakubalisha katika msemo huu!,pia mara kadhaa ama kila siku watu wamekuwa wakiwasifia mama zao kuwa ni bora sana na pia wamewapambania sana hadi kufikia hapo walipo!,sina shaka na hilo.

Lakini mbona sisi wengine imekuwa ni tofauti sana! Yaani machungu yaliyosababishwa na mama zetu ni makubwa sana yaani hadi unajiuliza hivi huyu ni mama mlezi kweli ama aliniokota tu barabarani!

Yaani sisi wengine tusipokuwa na pesa hata mama zetu hawapokei salamu zetu ! Hauthaminiki tena kama ni Mtoto wake! Pengine unaweza ukisema labda hali hii inaweza kumkumba Mtoto jeuri kwa wazazi wake la hasha! Sisi wengine hatujawahi hata kunyanyua mdomo kumsonya mama wala kukataa kutumwa chochote wala kubishana chochote lakini matokeo yake ni tofauti sana!

Nimeshawahi kuwa natuma pesa kwa mama mzazi ili nijengewe nyumba kwa muda wa miaka mitano niliyokuwa nje ya Tanzania [emoji1241] nakuja nakuta kiwanja hakina hata msingi, nishatuma pesa ili nilimiwe mashamba na mama mzazi na hakulima hata mita mbili.

Nilishawahi kutuma pesa ya maendeleo fulani lakini hakikufanyika chochote na ukiuliza anakuwa mkali kweli kweli! Kama Mtoto unajishusha na maisha yanaendelea!

Cha kushangaza akisikia umemsaidia ndugu yeyote anakununia na hamtaongea kwa muda mrefu! Hayo ni machache sana nayoweza kuweka wazi lakini zaidi ya asilimia 90 niliyofanyia itabaki ni siri yangu hadi siku ya mwisho!

Yaani huwa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa natamani hata nimkate kibao ila nikiangalia kuna wengine wamesaidiwa sana na mama zao nakuwa mpole!

Ni wengi tunapitia changamoto kwa wazazi wetu njooni hata tufarijiane ili kupunguza stress mbali mbali
Niliwahi kukutana na post moja huko Twitter ya jamaa akieleza jinsi anavyomchukia mama yake, tena yeye alikwenda mbali na kuomba mamaye afe. Wengi walimbeza, ila cha kushangaza ni jinsi watu wengine walivyokuja kushare experience zao za mambo mabaya wanayofanyiwa na mama zao au waliyofanyiwa pindi wakiwa wadogo chini ya Ile post. Nikajikuta nashtuka kwamba these things are real!

I think shetani anapigana sana against the bond iliyopo baina ya watoto na mama zao. And you having the best mother doesn't make others so. Mungu aingilie kati.
 
Ni kweli kabisa mkuu ila kutokana na maadali yetu ya kitanzania kwamba huwezi kumsema mama vibaya unabaki unaugulia tu moyoni
 
Niliwahi kukutana na post moja huko Twitter ya jamaa akieleza jinsi anavyomchukia mama yake, tena yeye alikwenda mbali na kuomba mamaye afe. Wengi walimbeza, ila cha kushangaza ni jinsi watu wengine walivyokuja kushare experience zao za mambo mabaya wanayofanyiwa na mama zao au waliyofanyiwa pindi wakiwa wadogo chini ya Ile post. Nikajikuta nashtuka kwamba these things are real!

I think shetani anapigana sana against the bond iliyopo baina ya watoto na mama zao. And you having the best mother doesn't make others so. Mungu aingilie kati.

Neno hilo ni kweli kabisa ndio maana leo hii unasikia kuna wanawake wanatupa watoto wachanga chooni
 
Inatokea tu mama hajali msaada wako,wala matatizo yako na huweza anza Fanya mashindano nawe kwa kilakitu.Lakini unakaa kimya coz ni mama
 
Nani kama mama ni msemo maarufu sana tangu zama za kale hadi sasa!,hakuna chakubalisha katika msemo huu!,pia mara kadhaa ama kila siku watu wamekuwa wakiwasifia mama zao kuwa ni bora sana na pia wamewapambania sana hadi kufikia hapo walipo!,sina shaka na hilo.

Lakini mbona sisi wengine imekuwa ni tofauti sana! Yaani machungu yaliyosababishwa na mama zetu ni makubwa sana yaani hadi unajiuliza hivi huyu ni mama mlezi kweli ama aliniokota tu barabarani!

Yaani sisi wengine tusipokuwa na pesa hata mama zetu hawapokei salamu zetu ! Hauthaminiki tena kama ni Mtoto wake! Pengine unaweza ukisema labda hali hii inaweza kumkumba Mtoto jeuri kwa wazazi wake la hasha! Sisi wengine hatujawahi hata kunyanyua mdomo kumsonya mama wala kukataa kutumwa chochote wala kubishana chochote lakini matokeo yake ni tofauti sana!

Nimeshawahi kuwa natuma pesa kwa mama mzazi ili nijengewe nyumba kwa muda wa miaka mitano niliyokuwa nje ya Tanzania [emoji1241] nakuja nakuta kiwanja hakina hata msingi, nishatuma pesa ili nilimiwe mashamba na mama mzazi na hakulima hata mita mbili.

Nilishawahi kutuma pesa ya maendeleo fulani lakini hakikufanyika chochote na ukiuliza anakuwa mkali kweli kweli! Kama Mtoto unajishusha na maisha yanaendelea!

Cha kushangaza akisikia umemsaidia ndugu yeyote anakununia na hamtaongea kwa muda mrefu! Hayo ni machache sana nayoweza kuweka wazi lakini zaidi ya asilimia 90 niliyofanyia itabaki ni siri yangu hadi siku ya mwisho!

Yaani huwa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa natamani hata nimkate kibao ila nikiangalia kuna wengine wamesaidiwa sana na mama zao nakuwa mpole!

Ni wengi tunapitia changamoto kwa wazazi wetu njooni hata tufarijiane ili kupunguza stress mbali mbali
Nilifikiri nipo peke yqngu,kumbe tupo wengi ambao "mama"zetu wanazingua,
Yaani mi nikiona mtu anamsifia mama yake,anagonga self akiwa na mama amemkumbatia,huwa nawaza hiyo experience ipo kweli au wanaigiza!maana Mimi hayo mapenzi ya mama sijawahi ona
 
Feminists ndiyo waliopandikiza huo ushetani kwa Ke wa HAKI SAWA.

Biblia inanena "waheshimu Baba yako na Mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi duniani"

Mungu hana upendeleo wowote, na hata baraka zinatoka kwa wazazi wote Baba na Mama, kama ilivyokuwa kwa Esau na Yakobo alipoagizwa Esau na Baba yake mzazi amletee kondoo aliyenona ambariki.

Poleni sana wabaguzi wa wazazi kwa upande wowote.
 
Kweli kabisa hata utoe msaada Vipi bado inaonekana hufanyi lolote zaidi tu yakuambulia lawama kila kukicha
 
Nilifikiri nipo peke yqngu,kumbe tupo wengi ambao "mama"zetu wanazingua,
Yaani mi nikiona mtu anamsifia mama yake,anagonga self akiwa na mama amemkumbatia,huwa nawaza hiyo experience ipo kweli au wanaigiza!maana Mimi hayo mapenzi ya mama sijawahi ona

Kweli kabisa sema ni ngumu kutoka hadharani na kuyasema haya ila tunapitia machungu mengi sana
 
Feminists ndiyo waliopandikiza huo ushetani kwa Ke wa HAKI SAWA.

Biblia inanena "waheshimu Baba yako na Mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi duniani"

Mungu hana upendeleo wowote, na hata baraka zinatoka kwa wazazi wote Baba na Mama, kama ilivyokuwa kwa Esau na Yakobo alipoagizwa Esau na Baba yake mzazi amletee kondoo aliyenona ambariki.

Poleni sana wabaguzi wa wazazi kwa upande wowote.

Nadhani umeingilia uzi usiokuhusu maana haujaelewa chochote
 
Feminists ndiyo waliopandikiza huo ushetani kwa Ke wa HAKI SAWA.

Biblia inanena "waheshimu Baba yako na Mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi duniani"

Mungu hana upendeleo wowote, na hata baraka zinatoka kwa wazazi wote Baba na Mama, kama ilivyokuwa kwa Esau na Yakobo alipoagizwa Esau na Baba yake mzazi amletee kondoo aliyenona ambariki.

Poleni sana wabaguzi wa wazazi kwa upande wowote.
Soma vizur mada mezani sio unapayuka payuka unatetea uovu kwa kivuli Cha dini poor
 
Watu bwana sasa shetani anahusika vipi na huu uzi

Ni matendo yenu binadamu yasiyokuwa na moral ground msimsingizie shetani
 
Nani kama mama ni msemo maarufu sana tangu zama za kale hadi sasa!,hakuna chakubalisha katika msemo huu!,pia mara kadhaa ama kila siku watu wamekuwa wakiwasifia mama zao kuwa ni bora sana na pia wamewapambania sana hadi kufikia hapo walipo!,sina shaka na hilo.

Lakini mbona sisi wengine imekuwa ni tofauti sana! Yaani machungu yaliyosababishwa na mama zetu ni makubwa sana yaani hadi unajiuliza hivi huyu ni mama mlezi kweli ama aliniokota tu barabarani!

Yaani sisi wengine tusipokuwa na pesa hata mama zetu hawapokei salamu zetu ! Hauthaminiki tena kama ni Mtoto wake! Pengine unaweza ukisema labda hali hii inaweza kumkumba Mtoto jeuri kwa wazazi wake la hasha! Sisi wengine hatujawahi hata kunyanyua mdomo kumsonya mama wala kukataa kutumwa chochote wala kubishana chochote lakini matokeo yake ni tofauti sana!

Nimeshawahi kuwa natuma pesa kwa mama mzazi ili nijengewe nyumba kwa muda wa miaka mitano niliyokuwa nje ya Tanzania [emoji1241] nakuja nakuta kiwanja hakina hata msingi, nishatuma pesa ili nilimiwe mashamba na mama mzazi na hakulima hata mita mbili.

Nilishawahi kutuma pesa ya maendeleo fulani lakini hakikufanyika chochote na ukiuliza anakuwa mkali kweli kweli! Kama Mtoto unajishusha na maisha yanaendelea!

Cha kushangaza akisikia umemsaidia ndugu yeyote anakununia na hamtaongea kwa muda mrefu! Hayo ni machache sana nayoweza kuweka wazi lakini zaidi ya asilimia 90 niliyofanyia itabaki ni siri yangu hadi siku ya mwisho!

Yaani huwa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa natamani hata nimkate kibao ila nikiangalia kuna wengine wamesaidiwa sana na mama zao nakuwa mpole!

Ni wengi tunapitia changamoto kwa wazazi wetu njooni hata tufarijiane ili kupunguza stress mbali mbali
Naomba nikuulize maswali machache na unibu kulingana na swali nitakalo kuuliza....

1. Wewe ni mtoto wangapi kuzaliwa?

2.huko nje wameenda wangapi kabla yako na baada yako..kutoka kwenye familia yenu??

3.uliishi muda gani njee ya nyumba yenu baada ya kuanzaa kujitegemea?
Kabla hujapata safari ya njee...??

4.una mchumba au demu ampae alifahamika kwenu kabla hukuanza safari ya huko njee..!?

5.rafiki wa karibu uliye muacha au ulio waacha wanajua safari yako kua uko wapi ...!?

6.baba au wajomba au ndugu wa karibu wa huyo mama yetuu wanafahumu tatixo hiloo...!?

7. Kuna mtuu yeyote Alie kua na maisha angalau mazuri yaani hali ya uchumi wa kipato Cha wastani katika familia yenu ..??;
 
Back
Top Bottom