Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,547
- 2,194
Dr remmy Ongara, Kanumba na Tx William Moshi? kwa upande wangu Dr remmy na Tx Moshi wamefanya makubwa kuliko Kanumba na wangefanyiwa kama Kanumba, maana sijaona cha ajabu alichofanya kuwazidi hawa jamaa! Serikali ina upendeleo! sijafuraishwa na ubaguzi wa Serikali. Remmy na Tx wametunga nyimbo nyingi za kufundisha na kuelimisha jamii ambazo zinasikilizwa na kila rika mpaka sasa, Je Kanumba kafanya nini mpaka Serikali kugharamia msiba wake na tena rais kuhairisha safari yake kisa Kanumba! kweli kuna mantiki? Tv zinashindwa kuonyesha matukio muhimu ya kitaifa na ya kujenga nchi, chakushangaza hata TBC wanakatisha bunge wanatuletea mazishi ya KANUMBA! kweli tanzania ni zaidi uijuavyo! Sipendi ifike atua niichukie Serikali. Ebu badilikeni jamani na fanyeni vitu vya Msingi, Watoto wanakaa chini, hospital hazina madawa, wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo, umeme tabu hata kulipa IPTL ni shida then mnatumia Kodi za wananchi kuendeshea msiba wa KANUMBA! Au Serikali imelogwa? Bila marehem MZEE KIPARA nani angemjua KANUMBA. Mbona mzee kipara tena mwanzilishi wa maigizo hakufanyiwa hivyo?