Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na Mvumbika Changa Hula Mbovu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na Mvumbika Changa Hula Mbovu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babykailama, Apr 11, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [FONT=&amp]Mimi ni mshabiki mzuri sana kazi nzuri za sanaa. Nilimkubali Marehemu Kanumba katika jitijada zake katika kuiendeleza Tasnia ya Filamu za kibongo. Kibinadamu, inasikitisha kwa taa ya kijana kama huyu kutoweka ghafla katika umri wa ujana wake. [/FONT]
  [FONT=&amp]Pamoja na hayo, zipo hisia, maneno na matendo yaliyoibuka wakati wa msiba hadi mazishi yake ambayo sikubaliani nayo. Hapa nimeamua kuwashirikisha maana konzo ya maji haifumbatiki kiganjani, itapenya tu! Pamoja na kwamba alikuwa maarufu (Bongo Celeb),[/FONT]
  [FONT=&amp]1. [/FONT][FONT=&amp]Hakukuwa na haja ya Viongozi wengi wa ngazi za juu kuacha shughuli nyingine nyeti za Taifa kwenda msibani, kusaini vitabu na kuhudhuria mazishi. Ni bayana kuwa huyu hakuwa Kiongozi wa Serikali, hata Wawakilishi tu wa hao wakubwa wetu wangeweza kuwawakilisha vyema. Fikiri kuwa Waziri (na Naibu wake) wa habari, Vijana na Michezo wote hawakuonekana kujibu swali husika katika Kikao cha 7 cha Bunge la 10 eti kwa kuwa walikuwa kwenye msiba wa Msanii maarufu! Wapi vipaumbele vyetu kama Taifa.[/FONT]

  [FONT=&amp]2. [/FONT][FONT=&amp]Ilishangaza Waziri kutangaza kutoa mchango wa Tshs.15 M (kwa niaba ya Serikali) na pia (tulisikia) kuwa Serikali iligharimia maziko yake. Ni kigezo gani kimetumika kuamua hivyo na pia kwa uamuzi wa nani aliyeidhinisha matumizi hayo? Ni Bongo Stars wangapi wamefariki bila hata mchango wowote (toka Serikalini) na hata kama tungelinganisha michango yao katika jamii mfano akina Sembuli, Remmy, TX Moshi, Marijani n.k basi hata tungesikia kiwango kama hicho au hata angalau nusu yake. Utashangaa kusikia kuwa mimi babu yangu alifariki na alikuwa Mwenyekiti (mwadilifu) wa CCM (M) na Mjumbe kwenye Jumuiya ya CCM (T) lakini cha ajabu hata hatukuona hata salamu tu za maandishi za rambirambi toka kwa Mwenyekiti wa CCM (T) kwa wafiwa hata Mjane wa babu yetu hajawahi kutembelewa wala kupewa mkono wa pole hata siku moja! Vitendo kama hivi vinatafsirika kuwa ni matumizi zaidi ya hisia (feelings) kuliko taratibu na kanuni zinazotuongoza na huleta manungĂșniko ambayo hayataisha kwa wengine wengi (nimewataja wachache tu). [/FONT]

  [FONT=&amp]3. [/FONT][FONT=&amp]Inasikitisha Watu wengi (akiwamo Mchungaji Muongoza Mazishi, Mkuu wa Nchi na Waziri wa HVM) tunapotoa Wasifu wa Kanumba, eti "Kijana mwenye TABIA nzuri ya mwenendo wa maisha wa kuigwa katika Jamii" nayo ni sifa yake. Je, hii ni kweli? Kwa vile wakati pumzi ya mtu imekoma huwa hatusemi mabaya basi tungeishia hapo tu katika kumsifia Weledi wake katika kazi ya sanaa ya kuigiza na filamu. [/FONT][FONT=&amp]Kusema kuwa vijana wengine waige tabia ya mwenendo wa maisha yake ni kuvumbika changa ambayo itawaletea vijana wanaoiga wale mbovu![/FONT]

  [FONT=&amp]Tuwe wakweli na tuwasaidie Wasanii wengi, Wasomi na pia Wanasiasa maarufu hasa katika kipengele cha mienendo ya maisha yao ili waendelee kuishi maisha marefu wakitoa michango yao mbalimbali ya vipawa walivyojaliwa na Mungu. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Nami Mungu anisamehe na muendelee kuniombea maana katika hili nami si mfano wa kuigwa kabisa! [/FONT]
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  you are right dude, hĂ­i ni ishara tosha kwamba maamuzi yetu ya kila siku esp mwenendo wa serikali huong6zwa na hisia zaidi kuliko kanuni na taratibu tulizojiwekea
   
 3. s

  shikasana Senior Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Daaa!! We mkali,ndomana ata wahengwa wanalonga...."filufilu filaaaa abadan Jalalaaa!!
   
 4. ikuo

  ikuo Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Hii ndo nchi yenye utawala bora. Rais ana ahirisha safari kisa kanumba? watu wote twaonekana hamnazo! tubadilike jamani, hatukatai alikua maarufu nchini lakin tunaangalia matumizi ya pesa za wananchi.
   
 5. f

  fisadimpya Senior Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hii ndo 'danganyika' maswala ya msingi hayapew kipaumbele,ulisikia serikal ya u.s.a ikitoa rambirambi kwa wako jako?
   
 6. e

  evoddy JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hoja zako namba 1&2 kwangu mimi hazina msingi maana kazi ya KANUMBA inafahamika zaidi Kimataifa hasa barani Afrika hivyo kwangu mimi ninazipuuza. Hoja ya tatu imeandikwa kuwa usimuhukumu mtu kabla hujajihukumu maana mwenye mamlaka ya hukumu ni MUNGU TU
   
 7. c

  chi-boy Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii yakusema kitamataifa bado inanipa kitendawili, ni kama waigizaji wa Nigeria. Tunawafahamu wengi lakin kuwafahamu hailiongezei taifa la nigeria chochote same applys kwa kanumba.. Kwa film analyst yeyote wa kimataifa hawezi kumaliza kuangalia bongo mvy hata 1, so 2sindanganyane kuhusu umataifa wake...
  Hapa nchini 2 ni chin ya 20% ndo watakuwa wanamjua coz ndo wanaopata umeme including wachunguliaji..
  Kanumba kafariki bt Taifa halijafa..
   
 8. FULLUMBU

  FULLUMBU Senior Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 180
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  ndo walewale ni maisha yap yafaa kuigwa kutoka kwa kanumba tuwe wakwel! Au nawe kama serikal yako unatumia hisia
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wanigeria walisha anza siku tele na wameyazoea hayo yakuwa na waigizaji wanaojulikana dunia nzima.

  Sisi kwetu the great ndio alikuwa anaanza kututoa ktk tasinia hii ya uigizaji.
  R.I.P the great bora serikali imeliona hili kuwa Kanumba alikuwa the great kwa waTZ wa kawaida sana.

  Naipongeza serikali kwa kulitambua hili nakuungana na watanzania wengi waliokuwa wapenzi wa kanumba na walioona mchango wake ktk kuitangaza nchi na kukuza tasinia ya uigizaji TZ.
   
 10. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  mleta mada wengi watakubeza lakini nami nimeshtuka katika hili. Cha ajabu zaidi nilimuona hata Prof. Anna Tibaijuka!! ...sijui labda wana urafiki na mama Kanumba!!

  Hapo kwenye red, naomba mwenye uthibitisho juu ya media za nje ya Tanzania zilizolipoti juu ya msiba huu na kwa uzito gani atujuze hili tukubaliane na hiyo hoja ya kusema kuwa mataifa mengi 'yamesikitika' kama tunavyosikia ikisemwa.


   
 11. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hawa viongozi wetu ni WANASIASA. Wao wanauza sura kwenye watu wengi, msiba ule ulibeba WAPIGA KURA wengi ndiyo maana nao wameenda kwa wingi. Umetoa mifano ya siku nyingi mno, kuna mfano wa hivi majuzi alifariki MUIGIZAJI maarufu MZEE KIPARA, sijui kama michango hiyo ilitolewa achilia mbali viongozi kufika huko. Tunaongozwa na hisia zaidi kuliko Sheria, Kanuni na taratibu.
   
 12. m

  mchungusana Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 15
  Kwahiyo ni mfano wa kuigwa? Unachukua watoto kuwafundisha kuigiza unawafundisha na vingine?
   
 13. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Only In Tanzania.
   
 14. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  hoja yako ya pili mkuu imenistua sana. Sikuwa na wazo kuwa ushabiki wao ungefikia hatua hii. Serikali inatoa wapi hiyo hela (kwa kasma/kifungu kipi?). Kwa kigezo kipi. Samahani msinichukulie vibaya kuwa labda namsimanga marehemu ila tuna viongozi wa ajabu sana. Au labda ndo hizo nguvu za 'ajabu'
   
 15. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  'mdanganyika' asilia
   
 16. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka, we ulitaka tukose kura kwenye chafuzi zijazo? hiyo ndo style yetu cc magamba.
   
 17. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu wote tulikuwa tunampenda sana kanumba buti kwa walivyofanya imeonyesha udhaifu wa serikali, Tutatetea mengi sana hata mimi sitaki kumsema vibaya marehemu lakini kufa kwa uzinzi au kwa dhambi yeyote ile ni aibu kubwa!
   
 18. R

  Renegade JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Wadanganyika wenzangu ya Kanumba yamepita, Tuache Maneno tufanye kazi, Binadamu tuna mapungufu mengi, Tuna mapenzi ya watu na vitu, Tukiguswa katika yale maeneo yetu huweza kufanya chochote ndani ya uwezo wetu, Mi naona twende kwenye ile thread ya Husninyo na Home work yake " The Power of Love". Kuna majibu Pia.
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  That only happens in DANGANYIKA land.
   
 20. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu huu ujinga uko Tanzania tu na ndiyo maana nchi yetu pamoja nautajiri wa madini, ardhi yenye rutuba, mbuga za wanyama, bahari na maziwa bado iko katika nchi maskini tatu zilizopata misaada mingi duniani.

  Mungu hawezi kutusamehe jinsi tulivyopoteza muda wetu pale Sinza Vatican na Leaders Club kwa ajili ya kuomboleza na kumzika mtu mwasherati na adui wa watoto (pedophile). Wenzetu nchi za jirani wanatudharau sana kwa upumbavu huu na tutaendelea kuwa maskini.
   
Loading...