Niliwahi kuwa na demu mkali, halafu mambo safi kwao. Siku moja akanikaribisha kwa famlia yao jioni kwa ajili ya chakula, mwanaume nikaoga safi, nikapiga pamba, nikaibuka ukweni. Tukiwa sitting tuanangalia tv, nikagundua watu wananon'gonezana kitu kisha wanaiangalia wanacheka sana kicheko kile cha kuvunja mbavu, dada zake demu na kaka zake na ndugu wengineo, wazazi hawakuwepo. Tukaenda dining kupata msosi, hali ya kicheko ipo pale pale. Nikajua wamefurahi tu miye kuwepo. Ila dem hakuwa na furaha, sikujali, (nadhani simu zingeshamiri kwa kipindi kile angenistua kwa sms). Badae nikaaga, nikasindikizwa ila demu hakuniambia kitu.
Nafika home flesh, stori za hapa na pale mara aunt yangu akaniuliza" hilo shati umevaaje? ".kujicheki kumbe nimeligeuza aisee na nilivaa tai ya kipepeo. Ile mikunjo ya shati kwa ndani imesimama hatari. [emoji849][emoji849][emoji849]. Nikawaza, niksunganisha doti, kumbe ndo mana ukweni walikuwa wananicheka! Nilifedhaika sana[emoji26][emoji26][emoji26], toka siku hiyo na mapenzi na yule dem yalifia pale, sikutaka hata kumuangalia usoni. Ingawa aliumia sana.