Nani huwapatia pingu shirikishi?

Nani huwapatia pingu shirikishi?

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
0cfb57309cd28238a466ceafbf3ea433.jpg

​
Imekuwa ni kawaida katika jamii kuwaona watu ambao hujiita askari shirikishi
Wakifanya kazi yakuwakamata raia katika mitaa ya Dar Es salaam na maeneo mengineyo katika nchi ya Tanzania.

Pamoja na rais wa jamhuri kukemea uwepo wa jesshi hili halamu lakini bado limeendelea kufanya kazi pasina kuteteleka na maagizo ya rais wa jamhuri ya Tanzania.

Kulingana na utafiti nilioufanya katika mkoa wa Dar Es salaam na Mwanza hakika hawa shirikishi wapo katika ofisi zote za maafisa watendaji KATA

Nimejaribu kujitahidi ili kuweza kufahamu ambae huwapatia PINGU askari hawa hakika sijaweza kugundua japo hawa jamaa hutembea na hizo pingu kiunoni mwao na wamekuwa wakizitumia kama nyenzo Muhimu katika kuwatishia raia ili wawape pesa pindi wanapo ona mazingira yanaruhusu..

Pamoja na uwepo wa wizara ya mambo ya ndani ambayo inaongozwa na Mwigulu Mchemba.. Na uwepo wa Kamanda Siro mpambanaji lakini wameshindwa kuliondoa Jeshi Shilikishi.. JS

Shilikishi wanabambikia watu kesi na police wanakuwa partner katika issues hiyo lakini haijulikani ni nani ambae huwapatia hawa jamaa PINGU.. Sababu PINGU ni zana ya kazi ya Jeshi la police na inapaswa kutumiwa na mtu aliepewa dhamana ya kuwalinda RAIA ambae ni askari wa Jeshi la police..

Naamini kupitia wana Jamvi naweza kumjua ambae huwapatia PINGU shirikishi...
 
hawa wapo karibia tanzania nzima, nilisikia tetesi kuhusu uwepo wao, na baadae nikasikia tetesi tena kwa tutaendelea kuwa nao, tatizo lao hawa jamaa wana matatizo sana na wananchi, hasda katika suala la kuwakama bodaboda
 
Back
Top Bottom