Nani HATAKI/HAWATAKI SERIKALI TATU ???

Nani HATAKI/HAWATAKI SERIKALI TATU ???

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Ukweli utabakia kuwa ukweli kuhusiana na lengo la kuwepo kwa serikali tatu ,inafaa kila Mtanzania ajiulize umuhimu wa uwepo wa serikali tatu ni nini ?

Wapo wanaopenda kuwepo kwa serikali tatu na wapo wanaotetea zibaki serikali mbili ,katika uchunguzi niioufanya kupitia habari zinazoandikwa kwenye vyombo vya habari na hata humu JF ni kwa lile kundi linalotetea kubaki kwa serikali mbili kundi hili ni moja tu nalo hutokana zaidi na wabunge wa CCM ,huwakuti wanaotetea serikali mbili kutoka chama kingine cha upinzani ,Huwa najiuliza ni kwa nini wabunge hawa wanahitaji kwa hali na mali kulinda kubaki kwa serikali mbili ?

Huwa sipati jibu kiurahisi ,ila muonekano wa ndani kabisa uliojificha ni kulinda maslahi yao binafsi na si ya chama wala Taifa ,Kilichokuwa hakipo wazi ni vipi mfumo wa Muungano,Je serikali ya tatu ambayo itakuwa ya Muungano itakuwa na wabunge ?

Tuchukulie wabunge wa Bunge la Muungano watatokana na Bunge la Zanzibar na Bunge la Tanganyika ,vipi wabunge hao watapatikana na idadi yao ni wangapi ? Tuseme Bunge la Tanganyika litachagua wabunge watakaowakilisha ndani ya bunge la Muungano na Kwa upande wa zanzibar Bunge la Zanzibar (Baraza la Wawakilishi) nalo litachagua wa kwao.
Tuseme idadi ya wabunge wa bunge la Muungano ni 30 au chini ya hapo(Zanzibar 10 na Tanganyika 20 au nusu nusu 15/15).

Hivyo utaona idadi ya wabunge wa Zanzibar watokanao na CCM itapungua na hivyo hivyo kwa upande wa bara ukilinganisha na ilivyo sasa ,kwa ufupi wengi wa walio CCM watapoteza hali waliyonayo sasa ,halikadhalika katika ngazi za serikali zaidi kwa upande wa Tanzania bara ,wote waliopo serikalini wanatokana na CCM ,uwepo wa serikali ya Tanganyika,CCM itapoteza nafasi zote walizonazo sasa ndani ya serikali ya Muungano na kuwawacha wengi wao wakipoteza nafasi hizo ,sababu inayowafanya walinde uwepo wa serikali mbili na kwa Zanzibar hali ni hiyo hiyo ni lazima watetee serikali mbili.

Kwa upande wa wananchi wasiofaidika na maslahi wayapatayo wabunge na viongozi wengi walio serikalini ,wao wanataka serikali tatu ,wakitumaini serikali ya Tanganyika itakuwa ndogo na yenye msisimko mpya.

Hofu iliyowajaa CCM sasa hivi na kwa muda huu wa mchakato wa KATIBA MPYA ni kuja kwa serikali Tatu ,hofu hii imewajaa viongozi wote wa CCM na haswa wale waliomo ndani ya mfumo wa kimaslahi kila wakimsikia mtu anahitaji serikali tatu wao huwa ndie adui yao nambari moja.Wataibua hoja lukuki zisizo na kichwa wala miguu alimuradi wanahakikisha Muungano wa serikali mbili hauguswi wala kuyumbishwa.

Inakisiwa piya kuwa kuja kwa serikali tatu ndio mwisho wa ukiritimba wa CCM na huenda ukawa ndio mwisho wa CCM kushika madaraka ya nchi hii kila baada ya miaka mitano na ndio mwanzo wa utawala mzuri utakao heshimu haki za binadamu.
 
Hakuna umuhimu wa serikali tatu, mimi hapa sitaki serikali tatu.
 
chadema wanataka serikali tatu ili watawale bara kwa sababu hawakubaliki zanzibar. cuf nao wanataka serikali tatu kwa sababu hawakubaliki bara.ili watawale znz. janja ya nyani kula hindi bichi, tumewatambua na tumestuka.
 
Hilo neno nalo, serikali tatu hazikwepeki. Wawaachilie wananchi waamue kuhusu katiba.
 
Wasiotaka serikali 3 ni VIONGOZI wa CCM.

Aidha kuhusu Wabunge wa JMT watapatikanaje na kwa idadi gani kati ya Tanganyika na Zanzibar nakushauri usome rasimu ya pili ya katiba ya Judge Joseph Warioba.

Inaelekea ni mtupu sana hujaisoma hiyo rasimu ya katiba mpya.
 
Panga Pangua, Sunami ya Serikali 3 inakuja na hayupo wa kuizuia!
 
Wasiotaka serikali 3 ni VIONGOZI wa CCM.

Aidha kuhusu Wabunge wa JMT watapatikanaje na kwa idadi gani kati ya Tanganyika na Zanzibar nakushauri usome rasimu ya pili ya katiba ya Judge Joseph Warioba.

Inaelekea ni mtupu sana hujaisoma hiyo rasimu ya katiba mpya.

mimi sio kiongozi wa ccm ila sitaki serikali nyingi
 
Wasiotaka serikali 3 ni VIONGOZI wa CCM.

Aidha kuhusu Wabunge wa JMT watapatikanaje na kwa idadi gani kati ya Tanganyika na Zanzibar nakushauri usome rasimu ya pili ya katiba ya Judge Joseph Warioba.

Inaelekea ni mtupu sana hujaisoma hiyo rasimu ya katiba mpya.

Iyo rasimu sijaiona husoma zipandezipande tu ,ipo webu embu weka link hapa !
 
chadema wanataka serikali tatu ili watawale bara kwa sababu hawakubaliki zanzibar. cuf nao wanataka serikali tatu kwa sababu hawakubaliki bara.ili watawale znz. janja ya nyani kula hindi bichi, tumewatambua na tumestuka.
akili za lumumba hizo ndo zinawasumbua
 
Hakuna umuhimu wa serikali tatu, mimi hapa sitaki serikali tatu.

Serikali tatu ni ya WARYOBA na siyo mawazo ya watanzania wa kule Rorya, watanzania wa Manzese, watanzania wa kule Makunduchi, watanzania wa kule oldonyo Sambu.
 
heri kufilisika kiuchumi kuliko kifikra na mawazo
yaaaaaani bora kufa kuliko kuishi hali u-chizi, hawa wa selikal mbili hoi
 
Back
Top Bottom