Nani atawafuta Machozi Yao?

Nani atawafuta Machozi Yao?

Milonji

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
171
Reaction score
524
Wapendwa Ndugu zangu wa JF salaam...

Baada ya salamu naomba niombe radhi kwa kutoleta Mrejesho wa yule RTO anayehujumu Mapato ya Serikali, hili ni kutokana na kuwa Nje ya Mkoa wa Dodoma na kupata Jukumu Jipya kwa sasa. Nina - ahidi nitawaleta Mrejesho huo.

Sasa naomba kwenda kwenye Mada husika. (Kutoka kwa Muathirika)

Mwaka 2018 Mwezi 9 TANESCO ilitwaa Eneo kwa ajili ya Ujenzi wa SUB-STATION, Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Dodoma Mjini, Kata ya Msalato, Shina la Catherine Mwakajoka(Samahani kama nitakuwa nimekosea kidogo Jina).

Jiji la Dodoma lilihusika katika Uthaminishaji wa Eneo wakishirikiana na TANESCO ambayo iliwakilishwa na Engineer Tabu.

Mwaka 2019 Mwezi April Mthamini Mkuu alipitisha JENDWALI LA MALIPO kwa ajili ya TANESCO Kufanya Malipo.

Kupitishwa kwa JENDWALI LA MALIPO Kuna maanisha kuwa TANESCO walitakiwa kulipa fidia Ndani ya Miezi 6 bila RIBA au kulipa Ndani ya Miaka 3 lakini ikiwa ni Pamoja na RIBA ya uecheleweshaji Malipo.

Baada ya JENDWALI kupitishwa Watanzania wenzetu hao waliotwaliwa Ardhi Yao walifanya kila Juhudi ya kulipwa Fidia bila Mafanikio. Walifanya Juhudi hizo kwa Kuona Moja kwa Moja na Mkurugenzi wa Jiji na Meneja wa Mkoa (TANESCO) na kwa kuandika barua pia, lakini walicho ambulia ni hewa.

Mh. Antony Mtaka (Samahani kama nimekosea Jina) alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa DODOMA, alikutana na Malalamiko haya pia na kwa weledi wake alikabidhi suala hili kwa Kamishna wa Ardhi Mkoa wa DODOMA ambaye naye pia alishindwa kutatua Changamoto hii baada ya TANESCO kushindwa kujibu Barua alizokua amewaandikia.

Mwaka 2022 Mwezi Aprili ilitimia Miaka 3 baada ya JENDWALI kuidhinishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali. Baada ya hapo yaani Kuanzia Mei 2022 kwa Mujibu wa Sheria iliwalazimu TANESCO;

i. Kufanya uthamini upya kama bado Wana uhitaji na Eneo hilo au

ii. Kurudisha Eneo kwa Wahusika (Barua ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa DODOMA inaeleza).

Wahanga hao walichukua Jukumu la kuwasiliana na Kamishna wa Ardhi Mkoa wa DODOMA kwa njia ya Barua ili Kipengele (i) au (ii) hapo juu kizingatiwe kwa Sababu muda umekwisha pita. Jambo la kushangaza barua yao haikujibiwa na hata walipojaribu kumfuata mara kadhaa.

Safari ya wahanga hao haikuishia hapo, waliona ni vema kuonana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ambaye aliwaelekeza kwa Kamishna. Kamishna wa Wizara ya Nishati na Madini alikabidhi suala lao kwa Ndugu COSTA ambaye ni Financial Manager (Samahani kama nimekosea CHEO chake).

Ndugu Costa aliahidi kuwalipa fedha zao Mwezi 7 au kama atachelewa basi watalipwa Mwezi wa 8.

Muathirika huyu ananieleza wametumia muda mrefu kutafuta haki hii na Mwenzao Mmoja ametangulia mbele ya haki pasipo kushika chochote.

Nilipo muulize kwa nini wanakubali kulipwa Fedha kwa uthamini uliokwisha muda wake?

Muathirika anasema, "Tulipoenda kwa Kamishna wa Ardhi Mkoa wa DODOMA alituambia hawezi kuandika barua kwa Sababu, kama TANESCO bado wanalihitaji Eneo hilo na yeye ikaonekana aliandika barua ya kulirudisha kwa Wananchi basi atapata shida hivyo anaogopa Kufanya Maamuzi", anaendelea, "Kwa Kamishna wa Wizara ya Nishati na Madini tulikubali kwa sababu alisema process ikianza upya itachukua muda mrefu na Mimi nikiangalia Kuna mwenzetu hatunaye na Mungu amemchukua bila kushika pesa yake ya fidia tukaona bora kuchukua tu".

Nilipo muulize kama walipeleka barua huku wakiwa na ushahidi kuwa barua husika zimepokelewa, yeye alisema, "Kila tulipopeleka barua tulihakikisha aliyepokea amesaini".

Nilipo muomba kitabu husika alisema aliyenacho hawezi kutoa, pia alikataa kunitajia Muwakilishi wao.

Nilifanikiwa kuziona barua takribani 6 ambazo waliandika kuhusu madai yao ya fidia huku nakala zikielekezwa Ofisi mbalimbali lakini bila Mafanikio ya Malipo.

Nimefanikiwa kupata barua Moja tu ambaye nimeambatanisha hapa.

Maswali fikirishi juu ya sakati hili.

1. Je unaweza kulipwa Fidia ya Ardhi ikiwa uthamini umekwisha pita muda wake?.

2. Je Serikali ipo juu ya Sheria?.

3. Je Malipo haya yakifanyika, yatakuwa halali au si halali Kisheria?

4.NANI ATAWAFUTA MACHOZI WAHANGA HAWA?

NB
a. Nipo nje ya DODOMA kwa wiki 1 sasa, wiki ijayo nitarudi ili kupata muendelezo wa nini kimejiri

b. Tuwafute Machozi Ndugu hawa kwa ku-share taarifa hii.

Cc:

1. WAZIRI WA NISHATI

2. WAZIRI WA ARDHI

3. KATIBU MKUU - WIZARA YA NISHATI NA MADINI

4. KATIBU MKUU - WIZARA YA ARDHI

3. MBUNGE - JIMBO LA DODOMA MJINI

6. MKURUGENZI JIJI LA DODOMA

NB
Huyu Mfanyakazi wa TANESCO anafahami vizuri Sana kuhusu hiki nilicho andika.

JINA: CONSTATINE RUBAGUMYA

MAWASILIANO: 0784 69 35 64

Nawasilisha.View attachment 2342042
 
Ndugu Mteja

Tafadhali onesha namba yako ya simu kwa ufatiliaji na hatua zaidi
 
Hili sakata halijaanza leo, Kuna mdau anaitwa "Chaliko" alishawahi kuliuliza humu na mkasema mnalishughulikia.

Binafsi "Chaliko" ni source of my information.

Kama mliahidi suala hili mnalishughulikia sasa muda wote huo mlikuwa mnashughulikia nini.

Nimesearch na nimepata kile ambacho mliwasiliana na "Chaliko" kwenye Jukwaa la TANESCO. Ushahidi ni huu hapa;

TANESCO Specia Thread

JIBU: Post Namba 7788 February 17, 2020.

SWALI: Post Namba 8036 Juni 10, 2020.

JIBU: Post Namba 8039 Juni 11, 2020.
 
Kwani nyie hamulifahamu hili tatizo, namba ya nini? Nazani kila kitu mnakifahamu na hili suala mnalifahamu cha msingi litoleeni ufafanuzi wenye mashiko.
Asante Mkuu Lutandagula,

Hapo juu nimeonyesha Mtaa, Kata, Wilaya na Mkoa. Namba za Wahusika wa TANESCO nimeainisha pia. Anahitaji nini tena kwa ufuatiliaji.
 
Hili sakata halijaanza leo, Kuna mdau anaitwa "Chaliko" alishawahi kuliuliza humu na mkasema mnalishughulikia.

Binafsi "Chaliko" ni source of my information.

Kama mliahidi suala hili mnalishughulikia sasa muda wote huo mlikuwa mnashughulikia nini.

Nimesearch na nimepata kile ambacho mliwasiliana na "Chaliko" kwenye Jukwaa la TANESCO. Ushahidi ni huu hapa;

TANESCO Specia Thread

JIBU: Post Namba 7788 February 17, 2020.

SWALI: Post Namba 8036 Juni 10, 2020.

JIBU: Post Namba 8039 Juni 11, 2020.
Tafadhali onesha ushirikiano wa taarifa sahihi kwa hatua zaidi
 
Kwani nyie hamulifahamu hili tatizo, namba ya nini? Nazani kila kitu mnakifahamu na hili suala mnalifahamu cha msingi litoleeni ufafanuzi wenye mashiko.
Mkuu Lutandagula,

Hata Mimi nimejiuliza wanataka Namba ya nini?

Post # 13 nimewapa Jina, Mawasiliano na nimeambatanisha barua aliyo andika Mfanyakazi wa TANESCO kuwajibu Watu wa Msalato Mwaka 2019.

Nasubiri Swali au Request nyingine kutoka TANESCO.
 
Dodoma ni wajinga sn miaka yote hawajawahi kuwa na mbunge wa upinzania hata wa dawa, acha CCM iwanyooshe
Kuna wakati tunaisema vibaya CCM kwa sababu tu ya uzembe wa Mtu Mmoja.

Nimeliweka hili wazi ili wanaofanya uhuni wa namna hii wapate kushughulikiwa na Wananchi wapate haki yao.
 
Back
Top Bottom