Nani atatumbua majipu ya Sector ya Kilimo hasa Tumbaku?

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,826
1,730
Waungwana kwanza nimpongeze mh Rais kwa kauli mbiu yake ya '' Kutumbua majipu'' ambayo imempatia umaarufu chanya ndani na nje ya nchi, hata hapa Uganda nilipo. Mimi ni mzaliwa wa Tabora. Kule kwetu zao kuu la biashara ni Tumbaku. kule kwetu hili zao japo ndio zao tegemezi lakini kuna shida kweli upande wa Pembejeo, Bei ya tumbaku na utunzani wa mazingira .. kubwa kuliko wakulima huko bado wanalia kilio cha madeni, madeni , madeni, na urasimu mwigi na ujanja ujanja kwa makampuni kiasi kuwa hali ya kiuchumi kwa mkoa wangu hasa wilaya ya Urambo ni mbaya kweli kweli ... namuomba mh. Rais kwa kupitia wataalam wake... atupie jicho kwetu huko ... umasikini umetopea na mazingira yameharibika sana.....wale wa Tabora kama mimi ni mashahidi jinsi wazazi wetu na vijana wenzetu walivyo masikini. Majibpu ya mjini tumeyaona tumbua na ya vijijini hasa kwenye kilimo.
 
Back
Top Bottom