Nani atatosha kuwa Waziri wetu wa Fedha baada ya kifo cha Dk. Mgimwa?

Ubinadamu umeenda wapi jamani?? Kama ni mtu mwenye roho nzuri, sidhani hata Rais ameshafikiri hilo la nani atamrithi Dr. Mgimwa. Tuwe na ubinadamu kidogo tu jamani. Akiisha kuzikwa, Rais ataanza kuwaza kuwa nilikuwa na Waziri wa fedha sasa hayuko, nimchague nani amrithi?? Ndipo sasa twaweza kumpa dokezo.
Natamani saana unitaje mimi lakini sio kabla ya Mgimwa kuzikwa tafadhali.

Wizara ya fedha ina manaibu wawili, vyema mmoja ambaye anakaimu nafasi ya Dr Mgimwa, aendelee na majukumu ya wizara mpaka 2015, naona ni gharama wizara moja kuwa na mawaziri 3! Kikwete ana mambo
 
Freemason wanajua kawaulize,si ndio wao wanao itawala Tanzania,sisi tutajuaje.Labda kama na wewe ni Freemason.
Baada ya kifo cha
Waziri wa fedha Dk. william mgimwa mengi yamesemwa ndani na nje ya
jukwaa letu la JF. Kwa wastani threads nyingi zimeonyesha kuwa wengi
wamehuzunishwa na kifo chake jambo linaloonyesha kuwa Marehemu alitimiza
wajibu wake.

Hata hivyo tumesahau wajibu wetu wa kutoa maoni yetu juu ya mtanzania
atakayeweza kutosha kuziba pengo lake bila kujali kuwa Mtanzania huyo
atatoka bungeni (bunge) au nje ya bunge (asiye bunge) ambaye akitosha
atateuliwa kuwa bunge. Tushiriki kutabiri/kubashiri kama watanzania si
kama watoa maamuzi.

Wengi wetu tutapenda kufanya dhihaka/mzaha au kuipuuza thread hii. Taifa
hili ni letu sote ubashiri wetu hapa JF kama utakuwa makini unaweza
kushabihiana na watoa maamuzi ndilo tunalojaribu kulifanya hapa.
Tunataka kuona kama tunaowawazia ndio watakaochukua mikoba ya
Mgimwa?
 
namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kukubali kutuondolea huyu zee Mgimwa mimi sumo katika unafiki Wa kuomboleza mimi ninasherekea kwa sababu Mungu amesikia maombi yangu. Huyo Mgimwa afadha amekufa Sera zake kiuchumi zimetuumiza sana sisi watu wakipato cha wastani na masikini. kodi hadi chooni msalani kitandani na jikoni huyu Mgimwa alikuwa waziri wawalicho nacho. huyu Mgimwa ndiye aliyeleta tozo kwenye simu huyu huyu ndie aliyesababisha mfumuko wa bei. huyu huyu Haiti ndiye tatizo katika uendeshaji biashara kwa machinga wa kariakoo. ninamengi ninayoyakumbuka sana ambayo yamekuwa kero sana kwangu wakati huyu maiti akishikilia widhara ya fedha ila kwakuwa Mungu kesha muondoa kabla hats kikwete hafikiria kufanya hivyo, sioni Baja yakuendelea kuanika madudu yake hapa. as ante sana tena sana Ewe Mola wetu. nakuomba umuweke William Mgimwa mahali pabaya penye mateso mengi asipate hata tone la maji jehanum amen.

Hang over za Viroba hizi! Hatari sana ngoja wakuteulie unaempenda wewe halaf uone ugumu wa hizo deal zako kuwa utazid mara dufu. Afterall sio vizuri kufurahia kifo cha mtu ambaye ametekeleza tu maamuzi yaliyofanyw na wengi. Nadhani ufaham wako ukirud utajiona jins ulivyojitoa ufaham na kuacha kufikiri sawasawa.
 
mm naona Lameck Airo mbunge wa rorya anafaa

kama sio basi hata Lucinde wa mtera pale anatosha kwan nn bhana!
 
Mnajua kinachotutesa hapa ni Mifumo mibovu na dhaifu sasa badala ya kuchagua mtu yeyote tu na akajua hapa natakiwa kuwa smart na kufanya kazi kwa weledi na Uzalendo nikiharibu watanimaliza ama kwa kunyongwa ama kifungo cha maishahapa hilo halipo ndio maana tunapata shida sana kuwapata watakao amua wenyewe wasiibe hilo ni gumu sana na litatupa shida kubwa kwa kizazi cha sasa na wabunge hawa...
 
Mkuu, lakini tuliwahi kuwa na Zakia Meghji kwenye nafasi hiyo na alifanya vizuri tu. tatizo lako mfumo dume umekutawala

nini kilimtoa kwenye uwaziri kama siyo kuchemka mbaya? huyo mama yako zakia anafaa kuongoza mapambio kwenye kitchen parties! hakuna cha mfumo dume wala nini!
 
Zakhia Meghji mbumbumbu ? hujui unachoongea

Unadhani u-mbumbumbu utamtoka kwa sababu wewe hutaki? Ndo ninachokisema kila wakati hapa kwamba kama unaamini anazo sifa, kataa maelezo haya kwa kutaja wasifu wake. Lakini usiniambie eti aliwahi kuwa muweka hazina wa ccm. Au eti alisoma uhasibu. Hatuendi kutunza pesa huko!

nasema tena mama huyu ni mbumbumbu to fit the position.
 
1. Prof Adolph Mkenda
Prof wa uchumi aliyekuwa mkuu wa idara ya uchumi UDSM na sasa naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi.
2. Harry Kitilya aliyekuwa Commission General TRA.
3. Dr Charles Kimei
4. Dr Dau
5.Prof.Samuel Wangwe

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Huyu naye akiwa kwenye list uwanja wa uteuzi unakuwa mpana

[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Samuel M. Wangwe - Globalisation and East Africa Professor Samuel M. Wangwe has a Ph.D from the University of Dar es Salaam (1980), an MA (Economics) from the University of Dar es Salaam in 1973 and a BA (Economics and Statistics) from the University of Dar es Salaam in 1972. Prof. Wangwe has authored eight books, including Economic Challenges Facing the Third Phase Government (with Prof. Van Arkadie), Exporting Africa: Technology, Trade and Industrialization in Sub-Saharan Africa (1997). He has published more than 40 articles. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Among the topical papers that he has written are: "Economic Reforms and Poverty Alleviation"; "The Management of Foreign Aid in Tanzania"; "Capacity Building in Policy Analysis and Economic Management"; and the one he has co-authored with Prof. B. Ndulu, "Managing Tanzania's Economy in Transition to Sustained Development." Prof. Wangwe also has worked extensively as an economic advisor to the government of Tanzania. [/FONT]
 
Wizara ya fedha ina manaibu wawili, vyema mmoja ambaye anakaimu nafasi ya Dr Mgimwa, aendelee na majukumu ya wizara mpaka 2015, naona ni gharama wizara moja kuwa na mawaziri 3! Kikwete ana mambo

Suala la Wizara ya fedha kuwa na manaibu wawili halijaanzia kwa kikwete, kama una kumbukumbu nzur kuna wakati wizara hii imewahi kuwa na makatibu wakuu wawili sijui nalo utasema ni la kikwete.
 
namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kukubali kutuondolea huyu zee Mgimwa mimi sumo katika unafiki Wa kuomboleza mimi ninasherekea kwa sababu Mungu amesikia maombi yangu. Huyo Mgimwa afadha amekufa Sera zake kiuchumi zimetuumiza sana sisi watu wakipato cha wastani na masikini. kodi hadi chooni msalani kitandani na jikoni huyu Mgimwa alikuwa waziri wawalicho nacho. huyu Mgimwa ndiye aliyeleta tozo kwenye simu huyu huyu ndie aliyesababisha mfumuko wa bei. huyu huyu Haiti ndiye tatizo katika uendeshaji biashara kwa machinga wa kariakoo. ninamengi ninayoyakumbuka sana ambayo yamekuwa kero sana kwangu wakati huyu maiti akishikilia widhara ya fedha ila kwakuwa Mungu kesha muondoa kabla hats kikwete hafikiria kufanya hivyo, sioni Baja yakuendelea kuanika madudu yake hapa. as ante sana tena sana Ewe Mola wetu. nakuomba umuweke William Mgimwa mahali pabaya penye mateso mengi asipate hata tone la maji jehanum amen.
Loh! Salalee! Msalie mtume Sheikh wangu Kiruavunjo! ... Huyu marehemu wanamzika tarehe 7 Kijijini kwao Iringa... Upande wa pili wa sarafu najiuliza kuliko ndugu yangu mpaka kumtolea marehemu dua mbaya kiasi hiki? Waliopandisha bei ya Umeme akina Haruna Masebu, Prof Muhongo, Badru masoud, Masele et al si mtawaombea Jahanam ya moto? Je wale wenye kung'oa kucha akina PINDA si mtasherehekea mwezi mzima wakifariki dunia?... Watawa hususan hawa viongozi wa CCM lazima watambue kuwa soon wananchi hawatafagilia Vogue wanazoziendesha wala mavazi yao ya Gucci... Wote mtakufa kifo cha coward kisicho na kilio wala maombolezo...
 
Sitashangaa nikisikia Mgulu Nchemba maana hakuna merit system zaidi ya kujuana kwenye kupeana majukumu mazito ya taifa
 
5.Prof.Samuel Wangwe

Huyu naye akiwa kwenye list uwanja wa uteuzi unakuwa mpana

Samuel M. Wangwe - Globalisation and East Africa Professor Samuel M. Wangwe has a Ph.D from the University of Dar es Salaam (1980), an MA (Economics) from the University of Dar es Salaam in 1973 and a BA (Economics and Statistics) from the University of Dar es Salaam in 1972. Prof. Wangwe has authored eight books, including Economic Challenges Facing the Third Phase Government (with Prof. Van Arkadie), Exporting Africa: Technology, Trade and Industrialization in Sub-Saharan Africa (1997). He has published more than 40 articles.

Among the topical papers that he has written are: "Economic Reforms and Poverty Alleviation"; "The Management of Foreign Aid in Tanzania"; "Capacity Building in Policy Analysis and Economic Management"; and the one he has co-authored with Prof. B. Ndulu, "Managing Tanzania's Economy in Transition to Sustained Development." Prof. Wangwe also has worked extensively as an economic advisor to the government of Tanzania.

I beg ti differ with u Mkuu... Hawa ma-prof waachwe wafanye kazi ya kuandaa wataalam wa nchi hii! Siasa ya Tanzania inahitaji watu jasiri wenye kujua game linalochezwa na mataifa makubwa! Tunataka mtu atakaesema hapana kwa mambo ya kipumbavu kama kupandisha bei ya nishati kunakopelekea kuua uchumi wetu na kutufanya tegemezi kwa kila kitu... Kwenye hii wizara anastahili mjeshi mwenye uelewa wa uchumi na ambaye atatanguliza maslahi ya nchi mbele...
 
Hapana bila uelewa haya bana! kama uchumi siku hizi ni kushika mitutu ya bunduki na namna ya kupanga bajeti ya silaha!
 
Back
Top Bottom