Nani atalipa damu za watu hawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atalipa damu za watu hawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MR NDEE, Aug 12, 2011.

 1. M

  MR NDEE Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Habari zenu enyi watanzania wenzangu mlio ndani na nje ya Tanzania,watanzania ambao kila uchao wanaona afadhali ya jana kulliko ya leo.japo serikali mekuwa ikijisifu kuwa Tanzania inakua kiuchumi na sifa hizi wanazipata ndani na nje ya Tanzania lakini wananchi wake wamekua katika lindi la umaskini na imefikia wengine kula mlo mmoja tu tena usio kuwa bora na wengine wamediriki kutuma watoto wao kuombaomba fedha za kujikimu, sasa wanadai wapigiwe makofi bungeni kwakile kinachodaiwa eti uchumi umepanda,serikali ambayo wawekezaji wake wanajeuri ya kutowauzia watanzania wanyonge katika nchi yao mafuta,serikali mabayo imeshindwa hata kuzowa taka zinazizozalishwa kila siku.

  Kimsingi sina nia ya kujadili yaliyotangulizwa hapo juu ilia ni ngazi ya haya yanayofuatia,watanzania kwa kuliona hili waliamua kuadhibu serikali kwa kutoichagua bahati tu kura hazikutosha kuiondoa madarakani kidemokrasia lakini ahueni ilipatikana kwa baadhi ya halmashauri na manispaaa kutwaliwa na upinzani tena kwa kishindo ile iwe funzo kuwa wanachi tumechoka,mathalani katika sehemi ninayotoka chama cha CHADEMA kilitwaa manispaa katika baraza la madiwani kwa ushindi wa kimbunga pamoja kiti cha ubunge ni huko MOSHI,tunashkuru hapa kutokea vurugu na maafa japo upigaji wa mabomu ya machozi katika kipindi ama mchakato wa kuhesabu kura ama kumtangaza mshindi hatukushtuka sana kwani sasa jeshi linatupa ujasiri kwani sasa tunatembea na chupa za maji kutoa muasho labda waanze kuja na maji ya kuwasha na tutatafuta mbinu ya kuyakabili.

  Hali katika jiji la Arusha haikuwa hivi mgogoro mkubwa wa umeya uliibuka jambo lililopelekea vifo vya raia wachapa kazi na chachu ya maendeleo pamoja majeruhi wenye mchango mkubwa wa kuifikisha Tanzania mahala pazuri na salama,naibu meya aliyechagiliwa kwa mizengwe Michael Kivuyo alijiuzulu akidai kuwa hawezi kuongoza sehemu iliyomwaga damu za watu,mgogoro huu ulisababisha maandamano makubwa yaliyokuwa yawe ya amani lakini yaligeuka kuwa majonzi.

  Kimsingi wananchi wa Arusha walikuwa wakitaka kuonesha hisia na fikra zao kuwa hawako tayari kudhulumiwa haki yao ya kimsingi ya kumpata kiongozi aliyechaguliwa kihalali na kwa misingi ya kidemokrasia,viongozi wa CHADEMA waliwaunga mkono,mbunge wao aliwaunga mkono madiwani kadhallika hatimaye waliingia barabarani kutoa hisia zao,polisi walivunja maandamano haya waliyoyaita haramu kwa nguvu na halii hii ilisababisha vifo na majeruhi kadhaa.

  Miezi michache baadaye baadhi ya madiwani waliibuka na kudai mchochezi wa muafaka kutofikiwa ni Godbles Lema(mbunge wa Arusha mjini) na hataki kuona maendeleo ya wana Arusha na kwamba ni mbabe wa maamuzi hivyo waliingia katika muafaka bila ya baraka ya CHADEMA,kamati kuu ilikaa na kiliangalia hili la muafaka bila ya kuomba na kupata baraka uongozi wa juu litatatuliwaje,chini ya Mabere Mrando madiwani wali walihojiwa wakuomba msamaha waliomba na waliogoma gamba waligoma na kamati kuu iliwavua uanachama.

  Uongozi wa CHADEMA ulidai kuwa suala la muafaka limeshaanza kushukhulikwa na waziri mkuu MH MIZENGO PINDA hivyo madiwani wale hawakupaswa kulizunumzia na kufikia muafaka hewa,kwa mshangao mkubwa waziri mkuu alilikana hilo bungeni na akashauri wale madiwani waende mahakamani kama wanapenda,inawezekanaje hili la uongozi wa CHADEMA na waziri mkuu wanatafuta muafaka halafu wakanwe bungeni?je ni kweli hapakuwa na maridhiano?uongozi wa CHADEMA wanakumbuka kuwa VIFO VILITOKEA?madiwani wanakumbuka hili?je haya ndio malipo ya damu iliyomwagika na vifo vilivyotokea?haya yaliyopo sasa ni kwa ajili ya politcal interest au socal interest hili ni swali langu na omba enyi waungwana mnijibu mapema
  SUKRANI KWA KUSOMA NA UNIJIBU NA MSAADA WAKO NI CHACHU KWA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAYE.
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mungu ndiye anajua usihukumu usije hukumiwa
   
 3. M

  Mzee wa Posho Senior Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa,Mbowe,Lema,Ndesamburo,Maaskofu wa Arusha.........lazima watailipa damu hiyo
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kikwete, pinda,Vuai,makamba,mwema,andengenye,zuberi
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  dawa ya maji ya kuwasha ni kujipaka oil..
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo hizo posho ulizopewa...? au..?
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  siasa ni gharama
   
 8. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siasa ni mchezo mchafu pale zinapochafuliwa.
   
 9. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Damu iliyomwagika na vifo vilivyotokea wakati watu wanadai haki yao ya msingi ni sawa na ngano iliyopandwa ikaota na kuvunwa kwa wingi,thus penye kudai haki ni laazima damu itamwagika ili haki iliyokosekana ipatikane!!!!!Hakika haki ya mtu haiwezi nunuliwa kwa fedha!!!lazima ipatikane.Pinda kwa alichokifanya bungeni ni dhahiri damu ya watu iko mikononi mwake kama waziri mkuu asiyekuwa na msimamo wa kutoa kauli thabiti ya serikali,he is a betrayer
   
 10. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani unaposema Pinda ni sawa na kusema JK. wote ni kama ukiona njingi utadhania njege. damu ya watu iliyo mwagika na itakayo mwagika na iwe juu ya JK na Pinda wasiyo weza chukua maamuzi ya haraka kwa maslahi ta Taifa.
   
 11. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mzee wa Posho,

  Unawazimu.
  Maana posho ulizo pewa na mwigulu zimekulevya. Yaelekea pia wewe ni miongoni mwa watu wanao fikiri kwa kutumia makali badala ya kichwa. Tumia bongo bwana mdogo. katika hili damu za watu hao naziwe juu JK wako, pinda, andengenye, mwema, na vuai wasiyo juwa wajibu wao.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Je waliowatuma polisi kujafanya maandamano ya amani kuwa yafujo na taharuki kwa watu Arusha na pia kung'ang'ania madaraka watalipa nini? huoni ata hii kutoelewana ndani ya ccm ni moja ya hizi damu zinalipwa?kazi kwenu sasa CCM kuangalia alama za nyakati
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na huu ni wakati wakupata uhuru wa kweli na sio wa jina kama ulivyo
   
 14. s

  samoramsouth Senior Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jk damu ile ii mikononi mwake
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kikwete na sirikali yake
   
 16. M

  MR NDEE Member

  #16
  Aug 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  At least nmenza kupata mwanga kidogo,ninacho amini kuna wasaliti wanaotaka kudhulum damu ya wanaharakati wale,kimapinduzi na kiharakati dhambi ya usaliti ni KIFO, wanaosaliti rasilimali za wanyonge lazima wafe,kufa kwenye ni kwa namna mbili,wafe huku wanatembea au wafe kihalisia tunaeza kuwaua watu hawa kisiasa wasisikike tena,wasiheshimiwe tena,halafu la kufa kihalisia kwa sasa ni jukumu la muumba,MSIMAMO WANGU KWA SASA WASALITI NI MADIWANI WALIO SALITI NA KUKIMBILIA MUFAKA BILA YA RUHUSA YA MASHUJAA WALE KIFUPI WAMEWATUKANA MAREHEMU,damu zao zilikuwa rutuba ya maendeleo leo hii wamemwaga acid ili mazao yasimee,hata hivyo viongozi wa juu watuambie alichosema MH PINDA yaani serikali kina ukweli kisi gani au ilikua ni political rally ya mheshimiwa serikali
   
 17. M

  Mzee wa Posho Senior Member

  #17
  Aug 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />

  Hata magwanda kufukuzana udiwani Arusha ni mwendelezo wa malipo ya damu hizo!
   
 18. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  &lt;br /&gt;<br />
  Josephine Mshumbusi,Lucy Owenya,Halimaa Mdee,Rose Kamili na Mchungaji Msigwa! Hawa pia damu ina walilia! Hukumu yao itatokea hapa hapa duniani!
   
 19. M

  Mzee wa Posho Senior Member

  #19
  Aug 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema wote hii damu lazima mtailipa kwa gharama kubwa!
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Ndesamburo, a loser Dr Slaa, Lema, Mbowe, hawa wamechangia kupoteza maisha ya vijana wetu.
  Mwezi ujao wamewambia vijana wajitokeze tena kwenye maandamano wakavamie ofisi za Manispaa ya Arusha
   
Loading...